7.1 C
London
Wednesday, April 24, 2024
HomeCommunityViwandani

Viwandani

Date:

Related stories

Delegates Convene for Talks on Plastic Pollution

Delegates during the official opening of the Third Session...

Government and Doctors Nearing Deal as Talks Extend to Tuesday

In an encouraging update, Head of Public Service Felix...

Plastic Bag Ban Extended to Garbage Collection By NEMA

In a recent announcement, the National Environment Management Authority...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Binadamu huhitaji amani ili kuendesha shughuli zake za kila siku inavyotakikana. Hakuna jambo lolote la manufaa ambalo linaweza hutokea katika mazingira ambayo hayana amani.Hivyo basi Ipo maana ya kukuza amani na utulivu katika maeneo ambayo tunaishi. Hii ni kwasababu ukosefu wa amani husababisha gharama kubwa ambayo haiwezi kulipa kwa urahisi. Kwa mfano vita, ubomozi , chuki na hata ukatili Kijijini.

Watu hupoteza maisha Yao , huharibiwa Mali na vilevile kukiuka haki za binadamu. Jambo Hilo hufanya wengi wao kutofuata Sheria kikamilifu. Isitoshe maendeleo katika maeneo yasiyokuwa na amani hutoweka kama Moshi angani. Katika kaunti mbalimbali nchini maendeleo huhitajika utangamano. Vita vya kikabila hurudisha nyuma miradi ya ufanisi.

Jamii zinazozana ni kielelezo Cha matokeo ya ukosefu wa amani maishani. Hapo nchini tatizo la wizi wa mifugo limekita mizizi maeneo ya Baringo.Nazo athari zake Huwa hatari katika jamii. Ili kuepuka maafa zaidi ni Bora jamii zihamia sehemu ambazo Zina amani.upweke na ukosefu wa furaha na utulivu zaidi, hufanya wanchi kuishi kwa hofu mno. Kule katika kaunti ya Baringo na samburu. Wakazi wanaomba serikali kuwapatia usalama.

Amani huleta maendeleo ya viwanda. Viwanda ni muhimu kwa kuwa ndivyo vinavyovigeuza malighafi inayopatikana na kuwa bidhaa zinazotumiwa na watu. Bidhaa hizi kama sabuni .Dawa ya meno na hata karatasi Shashi, katika nchi zinazoendelea ambazo hazina uwezo mkubwa wa pesa za kuanzisha viwanda au biashara .. Bidhaa nyingi hutengenezwa kwa kutumia mkono.
Viwanda hivi vidogo Huwa na uwezo wa kuajiri wafanyikazi wengi kwa kuwa, hawana uwezo wa kugharamia Kununua mashine .Hii ndio maana waziri wa elimu bwana Ezekiel Machogu, anapiga jeki, sekta ya jua Kali , wanafunzi wengi wanahimizwa kujiunga na chuo Cha ufundi.

Uajiri wa wafanyikazi wengi katika chuo Cha ufundi ni suluhisho Bora, ya sehemu ambayo ukosefu wa kazi ni tatizo kubwa. Kuwepo kwa viwanda vidogo huchangia kusambaza kwa viwanda mbalimbali kule mashambani. Hali hii inahakikisha kuwa Kuna mapato kwa wananchi. Mapato husaidia kuboresha maendeleo nchini.

Ingawa viwanda ni Bora pia Huwa na athari zake. Uchafuzi wa mazingira ni miongoni mwa masuala ambayo yamekashifiwa na wakazi wengi kwa mazingira na wanalia. Mawingu ya Moshi yanayotoka viwandani hayatishi tu afya zetu Bali, hufanya mazingira kutopendeza .Moshi hii uingiapo katika mapafu yetu huyachoma na kusababisha magonjwa kama pumu na saratani ya mapafu.

Kuna baadhi ya viwanda ambayo hutengeneza dawa za kemikali mbalimabali ambayo huigeuza mito na maziwa yetu kuwa majaa ya Kurundika taka zao. Kitendo hiki hasa huwaua wanyama wa baharini kama vile samaki.Isitisho mafuta ya vyombo vinavyovuja kutoka kwa vyombo vya baharini huendelea na maangamizi ya viumbe hao.

Vyombo vya ufundi ni kama vile msasa , randa , nyundo,keekee. Vyombo hivi vyote Huwa na kazi Yao maalum. pictureKama vile musumeno ni kifaa chenye menomeno Cha kukatia mbao kwa kukereza. Pimamaji ni chombo Cha kupimia usawa na unyookaji wa sakafu. Nyundo ni kifaa cha kogongomea misumari.

Katika sekta ya jua Kali Kuna baaadhi ya shughuli ambazo hutendeka kama vile kutengeneza vitu vya sanani . Sanani ni vitu ambavyo hutengenezwa kwa mbao kama vile viti , dawati , meza na kadhalika.viwandani pia Kuna cherehani ambayo hutumiwa. Kutengeneza nguo. Kuna kiwanda hitajika kama vile “E. P.Z.” ambayo mara nyingi hujulikana ketengeneza nguo.
Ufuaji wa vyuma.Huo ni ufundi wa Hali ya juu. Kuna baadhi ya madirisha ambayo hutengenezwa kwenye viwanda. Mafundi Hawa hutumia umeme ili kutekeleza kazi yao. Ni Bora kufahamu kuwa serikali imetia fora kuboresha elimu ya “C.B.C.” hii ni mojawapo ya ujuzi inayofanyika katika sekta ya viwanda. Viatu ni baadhi ya bidhaa ambazo hutengenezwa viwandani kwa kutumia ngozi . Ngozi inaweza kutengeneza Ngoma, mikanda ya kuvalia kiunoni na kadhalika.

Kuna viwanda ambavyo huendeshwa na serikali na zile za kibinafsi . wanafunzi ambao huenda vyuo vya ufundi Wana ujuzi zaidi ukilinganisha na wale walioenda katika chuo kikuu.wazazi wengi hudharau vyuo vya kiufundi bila kujua kuwa ni Bora zaidi katika kuboresha uchumi wetu.

Kabla kuanzisha kiwanda ni lazima uwe na leseni hitaji kutoka kwa serikali kuu . Pia utalazimika kulipa ushuru, waswahili hawakukosea kusema kuwa ukilipa ushuru wewe ni mjenga nchi daima katika eneo ya thika katika kaunti ya kiambu Kuna kiwanda hitaji Cha Delamote, kiwanda hiki husifika kwa uuzaji wa nanasi.

Kiwanda hiki pia huwadhulumu wale ambao hutumia njia ya mkato kuiba mananasi. Kila mkenya anafaa kutia bidii katika kilimo, usitegemee vitu vya bure, tutumia malighafi kutengeneza bidhaa nyingi siku zote.katika somo la sayansi ya nyumbani, almaarufu “home science” wanafunzi wanapata ujuzi wa kutengeneza bidhaa kadha, wanapomaliza shule, wataweza kupata kazi kule viwandani.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_img

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here