19.2 C
London
Friday, May 17, 2024
HomeCommunityHaki Za Mgonjwa Wa Kifua kikuu

Haki Za Mgonjwa Wa Kifua kikuu

Date:

Related stories

Why women struggle to take climate cases to court and how to correct it

By Pedi Obani A study in Nigeria and South Africa...

Calling off UN regional climate weeks exposes rich nations’ lack of goodwill

Funding these essential meetings would cost little to rich...

Don’t gaslight Africa: We need genuinely clean cooking solutions

The IEA summit, where oil and gas execs are...

Kenya: Adding up the costs of the floods amid an economic crisis

The devastation from the floods in Kenya have been...

Can We Use ChatGPT for Global Goods Software Development?

At IntraHealth, where our mission is to support health workers...
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes

Nchini kenya katiba inalinda haki yako au ya kila mkenya kupata matibabu ya hali ya juu kabisa. Wakenya hupata matibabu katika hospital za kibinafsi au hospitali za umma.Waziri wa afya anaitwa mheshimiwa Susan Nahumicha. Ili kuwa na afya bora, ni vyema kutembelea kituo Cha afya kila mara ili ujue hali yako ya mwili. Ugonjwa wa kifua kikuu huwa na dalili zifuatazo, kukohoa, kutoa jasho jingi usiku, joto mwilini na kutokuwa na hamu ya kula chakula, ni vyema kutembelea kituo Cha afya.

Unapofika hospitali ni haki yako kuuliza ili mgonjwa apewe ushauri kikamilifu. Hata ikiwa una kifua kikuu sugu, ama virusi vinavyosababisha ukimwi. Kila mgonjwa ana haki kupata ushauri wa kupambana na kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu wa kifua kikuu hasa kwa watoto. Ikiwa kila mgonjwa atajitolea kikamilifu kupambana na Ugonjwa huu, bila shaka jamii itaishi kwa amani.

Kuna baaadhi ya wananchi ambao wanahofia kuwa tiba ya kifua kikuu ni bei ghali. Siri ni kuwa katika hospitali za umma hakuna malipo yoyote kwa matibabu ya kifua kikuu, ni haki ya kila mkenya kupata huduma kwa heshima na bila ubaguzi, ni vyema kufahamu kuwa Kenya ina makabila arobaini na mbili. Unyanyapaa si jambo la busara wakati daktari wakati wanapotoa huduma.

Wakati mgonjwa amelazwa hospitalini ni furaha, kwake kutembelewa na wageni, Kuna wale ambao huja kumwombea na wengine humletea chakula. Kwa hivyo mgonjwa ana haki kutembelewa akiwa hospitalini. Mgonjwa hupewa habari kikamilifu kuhusu huduma zilizipo.

Daktari bora ni yule ambaye halazimishi matibabu. Ukiwa mgonjwa una haki kuuliza kama Kuna matibabu mbadala. Huenda dawa ulizopewa zimekuathiri mwili, bila shaka si vyema kupuuza jambo hili , mweleze muhudumu wa afya haraka, ukifanya hivyo basi suluhisho ya haraka itapatikana.

Huduma na heshima katika kituo cha afya. Ni haki ya mwananchi kupata hudumu bila malipo na haki zao kukiukwa. Kuna baadhi ya madaktari ambao hufichua Siri ya mgonjwa. Kwa mfano ikiwa mgonjwa ana Ukimwi, usitoe Siri yake kwa marafiki zako. Jambo hili linaweza kumfanya mgonjwa kujitia kitanzi, bila kutarajia lengo lake ni nini.

Siri ya mgonjwa haifai ifichukiwe bila idhini yake, mgonjwa ana haki kuchagua mtu ambaye atamweleza kuhusu Ugonjwa wake,hali ya kujieleza ni muhumu zaidi. Kuna nafasi ya kutoa malalamishi iwapo mgonjwa hakuhudumiwa ipasavyo. Daktari mkuu anafaa kutilia manani malalamishi ya wagonjwa na hatimaye kuyashughulikia kikamilifu.
Kuwa mgonjwa si mwisho wa maisha, Kuna baadhi ya waajiri ambao humwachisha kazi mtu ikiwa anaugua kupita kiasi. Hata walemavu wana haki zao za kimsingi, hawafai kubaguliwa kwasababu ya maumbile yao.Usalama kazini ni jambo la kutilia mkazo. Mgonjwa wa kifua kikuu ana haki ya kurudi kazini, huku akiendelea na matibabu. Lishebora au virutubisho ni muhimu katika afya ya mgonjwa kila wakati.

Wagonjwa wa kifua kikuu hupitia changamoto chungu mzima, huenda wengine wao hukosa fedha za matibabu, ikiwa hali hii hutokea kwa mgonjwa. Ni vyema kutafuta msaada kwa mashirika yasiyo ya kiserikali ili kupata kupata huduma. Si bora kumtenga mgonjwa wa kifua kikuu bali kufanya mjadala na wale ambao wanaugua Ugonjwa huu.

Bima ya afya wakati mwingine haitoshi kugharamia matibabu ya mgonjwa wa kifua kikuu. Ni wazi kuwa la Ugonjwa wa kifua kikuu kuenea zaidi. mgonjwa wa kifua kikuu anafaa kulindwa na raia. Kifua kikuu ni Ugonjwa hatari lakini una tiba .Kila mkenya ana jukumu la kuhakikisha kuwa umemkinga mwenzako dhidi ya kuambukizwa kifua kikuu.

Wahusishe walio na dalili za ugonjwa huu kutafuta matibabu mara moja. Tusiwadhulumu wagonjwa hawa bali tupigania haki ya wanaougua kifua kikuu. Naam,Kuna tofauti gani kati ya kifua kikuu na Ukimwi? Magonjwa haya mawili yana uhusiano mkubwa kwani kifua kikuu ni Ugonjwa wanaoambukizwa sana, kwa hivyo mtu anayeugua Ukimwi huweza kushambuliwa na kifua kikuu kwa urahisi sana.

Magonjwa mengine yanayohusiana na Ukimwi ni yale ya zinaa hasa kaswende na kisonono. Kwa zaidi ya mwongo mmoja uliopita, ulimwengu mzima uliathiriwa na masaibu ya kifua kikuu, kwa kiwango Cha kuogofya kiasi kwamba katika mwaka wa elfu moja mia kenda tisini na tatu. Shirika la afya duniani almaarufu (W.H.O.) lilitangaza

Ugonjwa wa kifua kikuu kuwa ya dharura. Ongezeko la visa vya kifua kikuu vilitokana na kuchipuka kwa viini vinavyosababisha maradhi hatari ya Ukimwi na magonjwa yanayoambukiza, viini vya Ukimwi vilishuhudia visa vya maradhi ya kufua kikuu.
Bara la Afrika ndilo lililoathiriwa na Ugonjwa wa kifua kikuu na ukimwi.Kulingana na utafiti, unakadiriwa kuwa mmoja kati ya wagonjwa wawili au watatu Wana virusi vya Ukimwi, watapata kifua kikuu wakati mmoja katika maisha yao.

Ni bora kushughulikia mgonjwa wa kifua kikuu , kwasababu yeye pia ni mwanadamu , ujenzi wa Taifa hutuhusisha sisi sote, kama vile umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_img

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here