19.8 C
London
Monday, April 28, 2025
HomeCommunityAthari Ya Kubeba Mizigo Mizito Mgongoni

Athari Ya Kubeba Mizigo Mizito Mgongoni

Date:

Related stories

Je, Kuku Wa Kienyeji Ni Mzuri Kwa Afya Binadamu?

Ufugaji wa kuku wa Kienyeji unahitaji mabanda ya kawaida,...

Ukulima Wa Moringa Makueni

Wakulima Makueni wamezamia kilimo cha dawa ya moringa. Wakulima...

Historia Ya Tattoo Kama Mapambo

Tattoo ni sanaa ya kuchora na ina historia ndefu...

The Ethical Rasing of Hacking and Cyber Security

Introduction In the digital age, the internet is both a...

Spring Detox Trends 2025: Rebooting body, mind, and lifestyle

Introduction The Call for Renewal As winter fades and spring...
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes

Madhara haya makubwa ya kiafya yanatokana na kubeba mzigo mzito mara nyingi si rahisi kutibika. Baadhi ya athari ni pamoja na kuleta matatizo mbalimbali ya kiafya yanayoweza kujitokeza na kuanza kuonekana katika kipindi kifupi japo nyingi ni baada ya muda mrefu.

Kwa mfano utapata uchovu wa mwili mzima, kuumwa na mgongo, kusagika kwa uti wa mgongo, maumivu ya mabega, shingo kiuno na miguu kushindwa kusimama vizuri na kupinda mgongo, tatizo la mfumo wa upumuaji, mishipa ya fahamu na kupata msongo wa mawazo.

Madhara haya makubwa ya kiafya yanatokana na kubeba mzigo mara nyingi si rahisi kutibika.Pia hutumia muda mwingi sana kuyatibu na fedha nyingi na kuongeza mzigo kwa familia na serikali katika ndoa au familia na serikali katika kutoa huduma za kiafya kwa wananchi. Mabegi yanabeba daftari zote, karatasi, vitabu, kalamu, mikebe, rangi za kuchorea na kwa baadhi ya wanafunzi yana vyakula na vinywaji. Wengine huweka nguo hasa sweta na viatu pamoja na sare za michezo.

Ni nini madhara ya watoto wadogo kubeba mabegi makubwa na mazito kila siku? Athari zipo nyingi hasa kwa watoto wadogo wenye miaka chini ya kumi na nane, watoto hawa hupata usumbufu mkubwa na huwa na mizigo mizito muda wote kuanzia nyumbani.

Kwenye daladala mpaka darasani. Wote ni mashahidi jinsi wanafunzi wenye mabegi makubwa wanavyopata shida kwenye vyombo vya usafiri. Iwe kwenye hata kwenye daladala au magari ya mwendo wa kasi na kwenye pikipiki. Wakienda darasani nako bado wanaendelea kuteseka na mabegi makubwa na mazito. Vilevile wanafunzi wanapewa elimu ya athari za kiafya wanazoweza kupata kama watabeba mikoba mizito na kuelekeza njia nzuri na salama za kubeba mikoba yao.

Wakati umefika kwa wataalamu wa wizara ya elimu na afya kuingilia suala hili kwa undani na kutoa miongozo juu ya uzito wa mkoba wa wanafunzi kwa kuanzia na wale wa chekechea.

Hii ina athari nyingi kwa mwanafunzi kiasi cha baadhi ya nchi kutunga sheria na kuweka miongozo ya kiwango cha mwisho cha uzito wa mkoba kulingana na umri na uzito. Katika kuhakikisha sheria inafanya kazi kama inavyotarajiwa, mkoba wa kila mtoto huwa unapimwa uzito kila mwanafunzi anapofika shule kabla ya kuingia darasani.

Vilevile wanafunzi wanapewa elimu ya athari za kiafya wanaweza kupata kama wakibeba mikoba mizito na kuendelezwa njia nzuri na salama za kubebe mikoba yao. Hii itasaidia mwanafunzi kuacha nyumbani vitabu ambayo somo lake halitafundishwa siku ile na kupunguza uzito wa mkoba wake.

Suala hii inafaa kuangaliwa kwa umakini na kufundisha utaratibu wa kuwa na ratiba ya kuhakikisha ni masomo yapi yako kwenye ratiba ili kupunguza mizigo na mkoba wa mwanafunzi. Uchunguzi katika nchi nyingi unaonyesha wanafunzi ambao wanaobeba mikoba mizito hubadili hata mwendo wao wa kawaida na kuwaweka katika hatari ya kuanguka wanapopanda ngazi au wakati wanapopita kwenye utelezi.

Tatatizo lililopo ni kukua kwa teknolojia na kubadilika mfumo wa maisha hivyo kusababisha wanafunzi kuwa na vitabu vingi vya masomo na kubeba vitu vingine. Utafiti unaonyesha mzigo mzito unasababisha maumivu ya shingo, mabega au mgongo.

Madaktari wanashauriwa mtoto abebe mkobo wenye uzito kati ya asilimia kumi hadi kumi na tano ya uzito wa mwili wake lakini ni vizuri zaidi ikiwa si zaidi ya asilimia nane.

Madaktari wanasema si vizuri kwa uzito wote wa mkoba kuwekwa juu ya bega moja kwasababu ukifanya hivi inaweza kusababisha maumivu ya bega na shingo.
Kumwona mwanafunzi amebeba mkoba mzito hata kushindwa kukimbia imekuwa ndiyo mtindo wa kisasa, wachache wanaokwenda na mkoba mepesi huonekana kama hawajaendelea.

Wanafunzi wengi, hata wanasoma shule za chekechea hubeba mkoba mzito na vitabu na vifaa vya masomo wanapokwenda na kurudi shule kuliko uwezo wa migongo yao kuhimili uzito huo. Kwa bahati mbaya suala hili limekuwa kwa mara nyingi likifumbiwa macho kama vile halina athari zake kwa maisha hapo baadaye hazizungumzwi hadharani.

Wazazi na walezi lazima wawasaidie watoto kutambua kuwa kuna madhara makubwa ya kiafya yanayoweza kuwapata kutokana na kubeba mzigo mzito. Hivyo kuwa na mabegi makubwa na matatizo kila siku waendapo shuleni ambayo huathiri afya zao sasa au hapo baadaye siyo jambo njema.

Ubebaji wa mabegi makubwa miongoni mwa wanafunzi ni tamaduni unaonekana kuchipuka nchini. Watoto siku hizi wanabeba mifuko mizito ya shule migongoni mwao, uzito huo utavuta mwili unaosongo mbele ili kuweka usawa mkoba mzito wa shule unaathiri afya.

Athari zake huenda zisionekana, wanafunzi huumwa na mgongo na miguu na hiyo hutokana na uzito wa mabegi wanayobeba wakati wa kwenda shule. Chanzo cha maumivu anayolalamikia mara kwa mara kutokana na kubeba begi zito migongoni. Watoto wenye umri wa kati miaka kumi na nne hadi kumi na saba wanalalamikia maumivu ya mgongo.

Unachangia kuwapo kwa shida hiyo ni mifuko na mabegi mazito ya shule mara ni mfuko na mabegi mazito ya shule. Shule zinapaswa kuwa na makabati ya wanafunzi ambayo wanaweza kuweka vitabu vyao vya ziada.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img