10.4 C
London
Saturday, December 21, 2024
HomeCommunityAjali Haina Kinga

Ajali Haina Kinga

Date:

Related stories

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities In the...

Challenges Facing the Kenya’s Current Socio-Political Landscape

Kenya's current socio-political landscape is shaped by a series...

A Global issue about Female Genital Mutilation

Female Genital Mutilation (FGM), also known as female circumcision,...

Faida Ya Kupanga Uzazi

Upangaji uzazi ni muhimu sana katika familia, inahusu wanandoa...

Madhara Ya Vita Katika Jamii

Hali ya majonzi ilitanda katika kaunti ya Tana River....
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes

Ajali ni tukio lisilofaa au hutokea kwa bahati mbaya bila kusudiwa na kwa kawaida huleta madhara , majeraha, uharibifu au hasara kubwa. Watu husafiri kwa kutumia magari, pikipiki traini na hata garimoshi. Kabla safari kuanza katika kituo cha “country buse” wakenya huwa na mazoea ya kuombea safari.Mjini Nairobi utawapata wachungaji wakiomba kabla dereva hajaanza safari rasmi. Lengo kuu ni kuzuia jinamiza ya ajali mbaya barabarani.


Kwa kweli visa vingi vya ajali barabarani vimezidi kutokea humu nchini. Visa hivi havisababishwi na ulevi pekee, bali baadhi ya madereva huendesha magari yao kupita kiasi na Kisha ajali hutokea. Madereva wengi ni vijana na hawajui kanuni za barabarani. Hali kadhalika kuna wale ambao hawajui kutunza magari yao. Wengi hupakia mizigo au kubeba kupita kiasi . Mambo haya yote huchangia jinamizi la ajali barabarani. Mzazi anapompeleka mtoto wake shuleni , kila mara huwa na matumani kuwa atarudi salama salimini. Hata hivyo ilikuwa ni majonzi katika shule ya upili ya chavakali .Tarehe moja au mosi Aprili mwanafunzi mmoja aliaga dunia kutokana na majeraha, Kisha wanafunzi ishirini na mbili walilazwa katika hospitali ya mtakatifu Monica. Ajali hii ilitokea katika Barabara kuu Mbale – Nairobi. Mwimbaji mashuhuri wa Mugithi Mary Wangary Gioche almaarufu Kareh .B. bado anaendelea kuomboleza kufuatia kifo Cha mtoto wake . Joseph Maduli alifarika ajali kutokana na basi ya “Easy Coach” eneo la Mamboleo Kisumu.


Joseph Maduli alikuwa mwanafunzi katika shule ya upili ya wavulana ya chavakali . Zaidi ya watu elfu moja wamepoteza maisha yao tangu Januari . Ni jambo la kusikitisha mno kuwa Joseph Maduli alitarajiwa kufanya mtihani wa kitaifa ” K.C.S.E.” mwaka huu wa elfu mbili kumi na nne . Ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni.Katika maeneo ya Maungu Voi kaunti ya Taita Taveta wanafunzi wasiopungua kumi , wa chuo kikuu cha Kenyatta walifariki katika ajali ya barabarani. Basi hilo lilikuwa linaenda Mombasa kwa ziara ya elimu.

Idadi ya Wanafunzi waliokuwa ndani ya basi walikuwa hamsini na nane. Basi liligongwa na trela katika eneo la Maungu kaunti ya Taita Taveta na kusababisha ajali hivyo .
Shughuli za kawaida za masomo katika chuo kikuu Cha Kenyatta zilikatizwa kwa siku tatu . Lengo kuu ilikuwa ni kuomboleza wale ambao walifariki Naibu Chansela Waceke Wanjohi alitoa taarifa huyo kwa mtandao.


Basi la chuo kikuu Cha Moi limetolewa mtaroni baada ya kuanguka. Wanafunzi wa chuo kikuu walikuwa wanaelekea Mombasa.Ajali hiyo ilitolewa katika barabara ya Nairobi – Nakuru, wanafunzi hawa walinusurika kifo. Wote walitoka katika maeneo ya tukio wakiwa salama salimini. Ingawa wachache walipata wajeraha madogo madogo. Heko kwa dereva kwa kuzuia ajali hiyo hiyo .
Baabaye basi hili lilitolewa kwenye mtaro . Ajali hii ilitokea katika barabara ya Nairobi – Nakuru .Naibu wa kamanda wa polisi wa Lari , Francis Njomo alisema kuwa wanafunzi kumi na mbili walikimbizwa katika hospitali ya Orthodox katika mji wa Kamende.Hata hivyo,si madereva peke ambao husababisha ajali , waendeshaji baiskeli, pikipiki na mkokoteni na hata wanaoenda kwa miguu husababisha ajali, aghalabu kwa kutojali Sheria za barabarani.Kwa hivyo , inampasa kila raia awe mwangalifu zaidi ili kusiwe na ajali barabarani kila wakati.


Kaunti ya kirinyaga ilishuhidia ajali mbaya zaidi, watu tano walifariki papo hapo baada ya matatu ya abiria ya kampuni ya ” Kukena Sacco” kubingiria mara kadha wa kadha .Ajali hiyo ilitokea eneo la koroma kwenye barabara ya Ngaru – Gatuta . Waziri wa uchukuzi bwana Kipchumba Murkomen anawasihi wakenya kuwa waaangalifu barabarani ili kuzuia ajali hizi.


Ajali za barabarani ni jambo ambalo hua tishio kwa watumiaji wote wa barabara . Ijapokuwa hutokea na kujirudia mara kwa mara .Kwa bahati mbaya zaidi ya wananchi hawajajifunza kutokana na makosa yaanayotokea ajali ikifanyika . Utawaona wakichota matuta,wengine wanapora mali ya abiria badala ya kuwasaidia. Nasikitika sana nikitazama wakenya wanapoteza maisha yao.

Ajali zote barabarani zinatokea kwasababu ya madereva hawataki kuwa makini .
Kuna utepetevu wa “NTSA” hawafanyi kazi ya kulinda usalama wetu. Kwa kweli ajali haina kinga wala kafara. Wakati dereva ni makini ndio suluhisho bora, polisi wanafaa kuepuka kuchukua hongo barabarani.


Si raia tu bali viongozi wamehusika katika ajali barabarani. Naibu wa spika katika kaunti ya Embu alisafirishwa kwa ndege hadi Nairobi kwa matibabu.Kisha binti yake alifariki .Kamanda wa polisi Embu Nicholas Maina alithibitisha ajali hii. Ajali haina ubaguzi wa rangi. Mwanafunzi wa chuo kikuu Cha Kenyatta Felix Onyango alisema kuwa ajali iliyotokea maeneo ya Mtito Andei ilikuwa ya kuhuzunisha sana, hakutarajia kuwa atawapoteza marafiki wake wa dhati , dereva wao alikuwa anajaribu kurudi nyuma kwenye njia yake wakati trela , iliyokuwa ikija upande wa nyuma iligonga gari lao.


Isitoshe tarehe sita Aprili Jumamosi , gari ya “Eldoret Express” ilihusika katika ajali . Ajali hiyo ilifanyika katika barabara ya Nairobi – Naivasha katika kaunti ya Kiambu watu watatu waliaga dunia , Kisha watu kumi na moja wakijeruhiwa.Wakazi wa eneo la Muguga walijitokeza kuomboleza wapendwa wao , Ombi langu ni kuwa serikali itachukua hatari kabla ya tahadhari.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img
Previous article
Next article