6.3 C
London
Monday, December 23, 2024
HomeCommunityAsili Ya Sheng Nchini Kenya

Asili Ya Sheng Nchini Kenya

Date:

Related stories

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities In the...

Challenges Facing the Kenya’s Current Socio-Political Landscape

Kenya's current socio-political landscape is shaped by a series...

A Global issue about Female Genital Mutilation

Female Genital Mutilation (FGM), also known as female circumcision,...

Faida Ya Kupanga Uzazi

Upangaji uzazi ni muhimu sana katika familia, inahusu wanandoa...

Madhara Ya Vita Katika Jamii

Hali ya majonzi ilitanda katika kaunti ya Tana River....
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Kenya Ina kaunti arobaini na saba. Kila kaunti Ina kiongozi ambaye ni Gavana.Tuna makabila arobaini na mbili. Hata hivyo Kenya inatambua lugha tatu rasmi, kiswahili, kingereza na lugha ya ishara mtawalia. Mimi ni mzalendo halisi kwasababu ninapenda nchi yangu.Uchaguzi nchini Kenya hufanyika baada ya miaka tano. Nchini Kenya Kuna demokrasia halisi hii hutokea wakati vyama mbalimbali hushiriki katika uchaguzi.


Sheng ni kifupisho Cha kiswahili na kingereza. Ni mfumo wa mawasiliano ambao umesanifiwa na vijana hasa wale wanaoishi katika sehemu za mjini. Mfumo wenyewe hufuata muundo wa sarufi ya kiswahili na lugha nginginezo, za bantu ili kutumia maneno mengi mapya ya kubuniwa na ya mkopo kutokana na lugha nyingine kiafrika.


Sheng ni tukio la kitamaduni ambalo linafungamana sana na mwanzo wa fikra au hisia na matakwa ya watumiaji wake. Maelezo kuhusu Sheng yalitolewa na wasomi kadha .Mkanga , Ogechi na Shitemi wanaokubaliana na maoni mbalimbali kuhusu Sheng. Wazungumuzaji wa Sheng walitambuliwa kutokana na mazingira na hali ya kifukara katika mitaa ya jamii yenye mapato ya chini,hawangeweza kupata mawasiliano. Elimu hutumia mawasiliano kupitia kiswahili au kingereza unaohitaji mfumo halisi . Kuna nadharia mbalimbali zinazojaribu kuelekeza chimbuko ya Sheng.

Nadharia mbili kuu inahusu nadharia ya uhuni na nadharia ya msimbo wa vijana .Nadharia ya uhuni ilibuniwa na kuibuka kutokana na wahuni au wakora jijini Nairobi.Vijana waliunda Sheng kutokana na baadhi ya maneno kutoka nyuma kuelekea mbele badala ya muundo wa kawaida wa neno.


Nadharia inahusisha kubuniwa kwa Sheng na hoja ya wahuni kuwasiliana kwa lugha ambayo watu wengine hawangeweza kufahamu.Sheng iliibuka miaka thelathini jijini Nairobi.Ijapokuwa wafanyikazi hawa pamoja na jamii zao walilazimika kutumia kiswahili katika mawasiliano baina yao, wengi walichukia kiswahili kwa vile kilikuwa kimedunishwa sana na sera za ukoloni kama lugha ya mashambani.


Lugha ya vibarua au maboi wa huwatumikia na wazungu.Hata hivyo wafanyikazi hao hawakupendelea Wakati wa kutumia kiswahili kila wakati.
Kiswahili na kingereza vilitambuliwa kama lugha za nyumbani,mengi yamezungumzwa na kuundwa kwa Sheng . Wataalamu wa lugha wametoa utafiti mbalimbali ambayo bado haijashughulikiwa .Jambo la kuzingatia ni kwamba lugha ya Sheng kilisambaa kwa utaratibu wa awali uliozingatiwa kuhusu kanuni za lugha.


Sheng pia ni utohozi wa maneno mawili ambayo Kiswahili na kingereza. Ni jambo la kusikitisha sana kuwa wanafunzi wengi, hawawezi kujibu maswali ya ufahamu katika kiswahili.Jambo hili husababishwa na uzoefu wa kutumia au kuzungumza lugha ya sheng .Maneno katika lugha ya sheng hauchukui maneno ya kiswahili na kingereza pekee . Maneno mengi ya kikabila yameingizwa kwa msamiati wa sheng na kukifanya kiwe na utatu zaidi .Lugha hii pia huwa na utaratibu mahususi unaofuatwa katika uundaji wa maneno ndiposa kimesheheni utata mwingine.


Ni bayana pia kwambe lugha,kama zilivyo asasi zingine za jamii hukumbwa na matatizo mbalimbali.Mabadiliko haya huweza kufaidi asasi hiyo au huweza kuleta athari mbaya ikazorota na kuchukua sura mapya kinyume na matarajio ya wengi katika jamii husika. Kuna baadhi ya wazee ambao siku hizi hujitosa katika matumizi ya Sheng. Utawasikia wanasiasa wakiongea Sheng huku wakidharau kabisa kanuni ya hadhira bila kujali .Hii si mfano bora kwa watoto ambao wanaopambana na lugha iliyo sahihi kisarufi.


Walimu wengi pia wamechangia kudumisha kiswahili sanifu , wao wanatumia Sheng darasani.Hapo ndipo ni wazi kuwa kiswahili imefika kwenye njia pande kwani idadi kubwa ya watu hawawezi kupambanua matumizi bora ya lugha . Suala la kuchanganya ndimi pia imechangia katika upotovu wa matumizi ya lugha yasiozingatia utamaduni wa kijamii.


Nafasi ya kiswahili humu nchini kwa jumla ni duni ikinganishwa la lugha za kigeni kama vile kingereza na kifaransa , uduni huu inatokana na sababu nyingi ambazo haziwezi kujadiliwa kwa kirefu hapa.Bali na lugha ya Sheng ,Kuna athari ya mama, wengi wanatumia lugha ya kiswahili Huwa na lugha ya mama kwa hivyo kiswahili huwa ni lugha yao ya pili au hata ya tatu .Hivyo watu wengi huwa wamezoea kutumia lugha yao kwanza na hivyo katika jitihada za kujifunza lugha ya pili, athari hujitokeza.


Vile vile Kuna mpangilio wa sauti katika lugha ya Kwanza ukawa na mgongano na ule wa kiswahili.Kuna ukosefu wa kutoelewa masharti au kaida za matumizi ya lugha ambapo mtu mkubwa kiumri anamwamkua mdogo wake kiumri kwa kutumia maamkuzi shikamoo.Hisia mbalimbali wakati mwingine husababisha kuweka makosa .


Sheng huonyesha mabadiliko yaani namna utamaduni wa kigeni unavyoiathiri jamii na jinsi jamii inavyojaribu kupambana na athari mbaya za utamaduni mpya, sababu kuu ya wanafunzi kufeli ufahamu ni athari za kuzungumza Sheng. Si ajabu kusikia wanahabari pia wanazungumza sheng.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img
Previous article
Next article