Maziwa hufanya mambo mengi mazuri kwa ajili ya afya yako. Wataalamu wa afya wamebaini kuwa maziwa huzuia magonjwa. Magonjwa au hali hizi ni kama vile shinikizo la damu. Gavana wa Transnzoia bwana George Natembeya ana mpango wa kuanzisha mradi wa kuwapatia maziwa watoto wachekechea. Lengo kuu ni kuwasaidia wanafunzi kuwa na afya bora shuleni. Gavana wa Machakos Wavinya Ndeti alizindua mradi wa ” Maziwa ya mama” tarehe kumi na tisa Januari mwaka wa elfu mbili ishirini na nne.
Chifu wa kaunti hiyo alitoa taarifa zaidi kuhusu mradi huu. Alidai kuwa kuna baadhi ya wananchi ambao walikuwa wanapinga mradi huu. Hayati Rais Daniel Moi ndiye wa kwanza kuanzisha mradi wa Maziwa. Maziwa yote ya ng’ombe yana karibu asilimia kumi na tatu iliyobaki ina proteini, mafuta, wanga, vitamini na madini. Inaaminika kuwa kunywa maziwa mbali na thamani yake ni lishebora. Kunywa maziwa ya Ng’ombe kunaweza kutoa kingamwili dhidi ya maambukizo. Wale wanaofuga mifugo hupatikana na magonjwa kama vile kimeta.
Maziwa ni muhimu kwa watoto wachanga wanaonyonyeshwa. Maziwa yana aina ya sukari inayoitwa “lactose” ni tofauti na sukari inayopatikana kwenye matunda na vyakula vingine vya sukari. Utafiti inaonyesha kuwa wanawake wanaokunywa maziwa hupunguza uzito zaidi kuliko wale wasiokunywa. Maziwa huleta hamu ya kula chakula. Ni bora kunywa maziwa wakati wa chakula cha jioni au unapokula matunda.
Maziwa ni chanzo bora Cha madini ya kalisiamu, hivyo basi maziwa ndicho kitu halisi kinachohitajiwa na meno yetu. Maziwa huzuia kutoboka au kuoza kwa meno. Ni vyema kila mtu kujitahidi kunywa maziwa kwasababu ina vitamini “D”. Vilevile maziwa huondoa msongo wa mawazo. Baada ya kazi nyingi za siku.unashauriwa kunywa angalau glasi moja ya maziwa. Hii itasaidia kukuondolea msongo katika misuli na neva zako za fahamu. Hebu fikiria kuhusu vitamini na virutubisho vilivyoko kwenye maziwa. Maziwa huondoa kiungulia ya kila wakati.
Kiungulia husababisha na asidi zinazopatikana tumboni. Utanda hutengenezwa kutoka kwa maziwa. Utanda hupambana na asidi zilizo tumboni. Maziwa hujenga ubongo wa mwanafunzi. Watoto wa chekechea wakinywa maziwa watakua na akili, ambayo itamsaidia kufanya vizuri kwenye masomo, hivyo ni bora kunywa maziwa mara kwa mara. Wazazi wana jukumu la kuweka mpango mzuri ili kuhakikisha watoto hawakosi kuhudhuria masomo. Afya ya wanafunzi ni bora zaidi wakiwa darasani.
Maziwa huzuia maumivu ya hedhi kwa wanawake. Wanawake wengi mara kwa mara wanakabiliwa na maumivu wakati wa hedhi. Maziwa yamedhibitishwa kuzuia na kupunguza maumivu haya kwa kiasi kikubwa. Ni kweli usiopingika kuwa watoto wanahitaji kunywa maziwa ili kuimarisha ukuaji wao. Ni kweli pia watu wazima wanahitaji kunywa maziwa ili, kulinda na kuimarisha mifupa yao dhidi ya maradhi haya huzuiliwa kwa kalisiamu ipatikanayo kwenye maziwa. Aidha maziwa husaidia kupunguza upungufu wa damu na matatizo mengineo, hatimaye, mafuta hayakusanyiki katika mwili wa mtoto. Kwa ujumla kunywa maziwa ni nzuri Kwa afya na ustawi wa watoto.
Maziwa hufanya ngozi mwili kuwa nyororo, huimarisha meno na mifupa kutokana na vitamini zilizomo. Kampeni ya unywaji maziwa shuleni kila siku, itasaidia wanafunzi kiafya. Wakiwemo wanaokwenda shule wakiwa hawajapata mlo wowote kutoka nyumbani kwao. Si kila familia huwa na uwezo wa kupata chakula. Heko kwa wazazi ambao Wana uwezo wa kununulia watoto wao maziwa kila wakati. Wanadamu wa awali hawakuweza kunywa maziwa ya wanyama wengine. Lakini huenda mambo hubadilika. Kwa nini watu walikumbatia mabadiliko. Maziwa ya wanyama ilikuwa na ushindani mkubwa. Kuna maziwa mbadala iliyotengenezwa kutoka kwa mimea ya soya yalizidi kupata umaarufu.
Maziwa mbadala yalitumika na watu walioathiriwa na maziwa ya wanyama na wasiokula nyama. Ni jambo la busara kujizoesha kunywa maziwa kila wakati, kwa ndivyo inavyohitajika kwa kila binadamu. Bilauri moja ya maziwa kila siku ina manufaa kwa afya yako. Kunywa maziwa huzuia aina ya saratani, je, unafahamu Cleopatra? alikuwa ni malkia wa Misri anayesifiwa kwa ubora wake, watu wengi walishangaa kuhusu maumbile yake. Inaaminika uzuri wa Cleopatra ulitokana na tabia yake ya kunywa maziwa mara kwa mara, jibini hutolewa kutoka kwa maziwa kupitia mchakato wa uchachushaji. Miaka elfu kumi iliyopita,hakuna mtu aliyekunywa maziwa mara chache tu.
Watumiaji wa awali wa maziwa walikuwa wafugaji na wakulima. Kuna baadhi ya wanyama ambao hutupatia maziwa kama vile ng’ombe, mbuzi na ngamia. Mtu akinywa kiasi kingi Cha maziwa anaweza kuendesha, kina mama kule magharibi mwa kenya huweka maziwa ndani ya mboga, wao hawawezi kula mboga za kienyeji bila maziwa. Wakati unakosa mboga nyumbani, basi wanaweza kutumia maziwa kama kitowe.
Gavana wa Embu Kawira Mwangaza, aliwapatia wananchi ng’ombe wa maziwa. Lengo kuu ilikuwa kusaidia jamii kuwapatia ng’ombe wa gredi, ng’ombe hawa Huwa na maziwa mengi lakini gharama yao ni ghali mno.