15.1 C
London
Monday, April 28, 2025
HomeLifestyleArt & CultureHistoria Ya Tattoo Kama Mapambo

Historia Ya Tattoo Kama Mapambo

Date:

Related stories

Athari Ya Kubeba Mizigo Mizito Mgongoni

Madhara haya makubwa ya kiafya yanatokana na kubeba mzigo...

Je, Kuku Wa Kienyeji Ni Mzuri Kwa Afya Binadamu?

Ufugaji wa kuku wa Kienyeji unahitaji mabanda ya kawaida,...

Ukulima Wa Moringa Makueni

Wakulima Makueni wamezamia kilimo cha dawa ya moringa. Wakulima...

The Ethical Rasing of Hacking and Cyber Security

Introduction In the digital age, the internet is both a...

Spring Detox Trends 2025: Rebooting body, mind, and lifestyle

Introduction The Call for Renewal As winter fades and spring...
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes

Tattoo ni sanaa ya kuchora na ina historia ndefu na tajiri katika tamaduni tofauti humu ulimwenguni. Unaweza kufikiria kuwa asili ya kuchora tattoo ni mazoezi ya magharibi. Watafiti wamebaini michora ya mwilini almaarufu “Tattoo” iliyokuwa kongwe zaidi duniani, iko katika mwili iliyoishi miaka elfu tano iliyopita nchini Misri. Watafiti wanaamini kuwa tattoo zinaashiria ujumbe wa kutokuwa na hofu na ujuzi wa kila mara kustaajabisha.

Imebainika kuwa tattoo ya mwili wa mwanamume sasa unaonyesha kuwa uchoraji wa mwili ulikuwa kila mara unafanywa kwa jinsia zote. Wataalamu wakidhani kuwa ni wanawake peke yake ndio wana tattoo wakati wa miongo iliyopita.

Tattoo zimekuwepo nchini India tangu nyakati za zamani na desturi hiyo ikitumika katika jamii na makabila mbalimbali. Unyanyapaa unaozunguka tattoo unaishi polepole. Ingawa mara nyingi hujulikana kwa kupamba mwili wa binadamu katika jamii ya magharibi, tamaduni za Asia kusini zinaonyesha maana ya ndani zaidi nyuma ya tattoo. Tatoo ni urembo, wanaochora wasibaguliwe na wanaofikiria kuchora waachwe waamue wenyewe kutoka katika nafasi zao na sio kushawishiwa.

Tanzania hairuhusu mtu awe na tattoo, labda kwa kificho mfano katika jeshi mtu hawezi sajiliwa kupata kazi. Tatoo siyo mbaya ila ubaya unaletwa na msingi yetu ya utamaduni na mfumo wa maisha kwa jumla. Pia wanaochora tattoo wawe tayari kihisia ili wasijutie baadaye.

Kwa sasa kumekuwa na wimbi la wachora tattoo mitani, hali inayohatarisha usalama wa afya za wale wachoraji. Ni vyema wachoraji tattoo kuzingatia taratibu za kiafya ili kuzuia miongoni mwa kesi za kansa ambazo hutokana na uchoraji tattoo, tattoo husababisha ulemavu wa ngozi. Kwa sasa kumekuwa na wimbi la wachora tattoo mitaani. Mionzo hupunguza sehemu ya tattoo na kutengeneza lengelenge linalobakia kama kovu.

Kuna baadhi ya tattoo ambazo hazifutiki mara moja bali hufutwa kwa zaidi ya mara tatu ndiyo iishe, mchoraji wa tattoo mkongwe Yusuf Masasi almaarufu Yuzo alisema historia ya tattoo ilianza miaka ya elfu moja themanini sita. Huko barani Asia, kipindi ambapo walichora na kutunza kumbukumbu ambazo zilisambaa katika maabara mbalimbali, ikiwemo Afrika ambako vijana wengi wameingia kwenye uchoraji huo.

Si ajabu kufahamu kuwa tattoo ni njia ya kuzungumza na moyo na humpatia mtu nguvu ya kupambana na changamoto anazopitia kwasababu siku zote kila mara zinamkumbusha kuwa yeye ni imara katika kila jambo.

Tattoo zimekuwa na udhabiti kadhaa na nchi nyingi zimepiga marufuku kabisa kuwepo na tattoo au askari wao kuchora, ni nchi chache zilizo ruhusu tattoo kwa askari wao. Vijana walio na mchoro wa tattoo mwilini waliondolewa kwenye uchaguzi wa N.Y.S. Katika uwanja wa Thika kaunti ya Kiambu, kadhaa walitimuliwa katika shughuli ya kusajiliwa.

Tattoo inahitaji ukamilifu wa kuchora picha za kudumu na muundo kwenye ngozi ya mtu si rahisi wanavyodhania baadhi ya watu. Henry amewafundisha wanawake wengi sanaa ya uchoraji. Anawashauri vijana waepuke lawama za kila mara kwamba kuna uhaba wa nafasi za ajira badala yake wanatumia muda wao kukuza na kuimarisha talanta zao.

Tattoo huwa ghali mno kama vile shilingi sabini na nane elfu. Bei ya chini zaidi huwa elfu mbili. Kwa dunia ya sasa ukichora tattoo ni kama fasheni fulani kwenye jamii, ukienda kuchora tattoo kuna uwezekeno mkubwa sana isitoke maisha yote na hivyo kwa usalama wako ni vizuri ukamuone mtaamu wa tattoo. Kabla hujaamua kujichora tattoo.

Basi ni vyema kujua madhara yake, Kati ya tattoo zote alizokuwa amechora zilikuwa zinauma sana ni za miguuni na kwenye vifundo vya miguuni. Maumivu ni ni jambo la kawaida. Watu hujikinga na madhara mishipa wakati wanachorwa .

Hapo mwanzoni wataalamu walikuwa wanasema hakuna uhusiano kati ya kansa ya ngozi na kujichora tattoo, lakini hivi karibuni tafiti zinaonyesha kuna aina fulani za wino ambazo zinaweza kusababisha saratani zikitumika kuchora tattoo.Watu wengi hupata ” allergies” baada ya kuwekwa tattoo.
Utafiti unaonyesha rangi nyekundu ndiyo inaongoza kwa kusababisha allergy. Mara nyingi allergy hizi huonekana mtu akikaa juani. Mwili unaotambu tattoo kama adui wake hivyo huharibu kuiondoa kwa njia mbalimbali.

Kwa hivyo husababisha makovu ya muda mrefu ambayo yanaweza kuleta magonjwa mengine ya ngozi. Tabia ya kurudia sindano zilezile wakati wa kuchora tattoo kunaweza kusababisha maambukizo. Tatoo nyeusi huwa imetengenezwa na iron oxide ambayo ina chembechembe za chuma. Hii inaweza kuleta changamoto kubwa kwenye vipimo. Wakati mwingine bakteria huvamia sehemu zenye vidonda vya tattoo na kusababisha kutopona haraka.
Dalili huweza kuwa homa kali, maumivu ya kuvimba Sehemu zilizochorwa tattoo. Hali hii husababisha kuvuja kwa damu nyingi chini ya ngozi. Huonekana sana sehemu ambapo rangi ya tattoo imepita na huchelewesha kwa kidonda kupona.
Tattoo ni uwekaji wa wino kwenye ngozi ya ndani na hutiwa ili kubadilisha rangi ya ngozi. Japokuwa wataalamu wanasema maumivu yanayotokana na tattoo ni makali mno, bado watu hupenda kuchora tattoo mwilini mwao.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img