Shuleni ni mahali ambapo wanafunzi huenda ili kupata elimu. Wanafunzi wakipata elimu yakutosha bila shaka watakuwa kioo cha jamii. Si kila mwanafunzi huwa na lengo kuu masomoni. Kuna baadhi yao ambao hufuata sheria za shule kikamilifu, darasani wao hutumia Kamusi katika kudurusu, nilipotembelea mwalimu Wambua katika afisi yake mjini Nairobi, alinielezea kuwa Kamusi ni kitabu cha marejeleo chenye maneno yaliyopangwa kialfabeti na huelezewa maana yake.
Msomaji hupata neno analotafuta kwenye Kamusi kwaupesi iwapo atafungua moja ukurasa wenye maneno yanayoanza kwa herufi moja na neno analotafuta. Maneno ya mwanzoni huanza kwa herufi A Kisha hufuatwa na yanayoanza kwa herufi B na huendelea hivyo kialfabeti hadi mwishoni mwa kamusi ambapo huwa na maneno yanayoanza kwa herufi Z.
Mbali na maana ya neno, fasili mbalimbali za neno hutolewa.Vitawe vya neno hutambulishwa kwa tarakimu zinazoandikwa juu baada ya neno hilo kwa maandishi madogo, Kwa mfano fua. Hii ina maana kuwa neno ” fua ” Lini maana tatu tofauti.Mifano ya matumizi ya neno ya neno katika sentensi hutolewa ili kufafanua maana zaidi.
Licha ya kuzingatia herufi ya mwanzo huhitajiki kutilia maanani herufi ya pili, ya tatu na zile zingine za neno kwa vile mfuatano wa herufi zote huwa umezingatiwa katika kupanga maneno kwenye Kamusi. Mathalani, neno baba hupatikana kabla ya neno beba kwa vile herufi a hutangulia herufi e katika abjadi. Kadhalika, neno bahasha litapatikana kabla ya neno baiskeli maadam herufi ya tatu ambayo ni h hutangulia i katika alfabeti.
Kuna kamusi za aina mbalimabali. Kuna zile za taaluma mahususi na zile zinazolenga wanafunzi. Kamusi za taaluma ni kama vile kumusi za matibabu, ya sheria na za dini. Kuna Kamusi zinazolenga wanagenzi wa shule za msingi zale zinazonuiwa kutumiwa na wanafunzi wa shule za upili au vyuo. Kamusi zinazohusu somo la kiswahili ni chungu nzima.
Zile zinazojulikana sana ni kamusi za maneno ambazo zineleza maana ya msamiati wa kiswahili miongoni mwa kamusi za maneno ni Kamusi ya kiswahili inayoelezea maneno kwa kiswahili, Kamusi ya kiswahili – kiingereza. Kamusi kama hizi ni johari katika tafsiri. Umuhimu wa kamusi ni kuonyesha muundo wa neno kwa wingi. Mara nyingi huandikwa katika mabano mathalani Juma( majuma) Baadhi ya Kamusi haziandiki neno kamili bali huandika silabi ya kwanza ikifuatiwa na kistari kama vile Juma. Ngeli ya nomino vilevile hutajwa katika mabano.
Msomaji anaweza kutumia Kamusi pia kuthibitisha maendeleo ya neno na hata matamshi ya neno hilo. Kuna Kamusi ya lugha ya kiswahili ambazo hujikita katika uwanja maalumu. Hizi ni kama vile Kamusi sanifu ya isimu na lugha, Kamusi ya fasihi, kumusi ya visawe, Kamusi ya misemo, kumusi ya methali na kamusi ya videndawili na mafumbo. Kamusi pia zaweza kuainishwa kutegemea ukubwa au udogo mathalani Kamusi kibindo ya kiswahili (kumusi ndogo ya mfukoni).
Kamusi nyingi hutaja aina ya neno aghalabu kwa kutumia italiki kuonyesha kategoria ya neno hilo. Hii hutuonyesha iwapo neno ni nomino, kivumishi, kiwakilishi, kitenzi, kielezi, kiunganishi, kihusishi au kihisishi.
Kamusi za wanafunzi hulenga wanafunzi wa shule za msingi au upili, kumusi hizi huwa na idadi ndogo ya maneno zilinganishwa na kamusi za kawaida ambazo hulenga, watumiaji wa lugha ya kawaida. Kama tujuavyo Kamusi za kawaida hulenga watumiaji wa kawaida. Kamusi husaidia jinsi ya kuendeleza neno fulani kwa njia ifaayo yaani kwa njia sahihi maneno mbalimbali.
Huonyesha maana ili kumsaidia mwanafunzi katika utumiaji kupanua ujuzi wake wa lugha hiyo.
Kamusi hubainisha ngeli za nomino na hivyo hutuelekeza katika upatanisho wa kisarufi. Muktadha kama vile dini, ushairi na baadhi ya msamiati wa kamusi ya mwanafunzi hutumia Kamusi kujifunza upatanisho wa kisarufi katika lugha rasmi. Kamusi hutumia lugha mbili almaarufu vidaa vinaweza kuwa katika kiswahili halafu pia huelezewa katika lugha ya kiingereza. Sifa za Kamusi ni pamoja na ukubwa, marudio ya tafsiri na kiwango cha matumizi ya kamusi ambayo inaweza kuathiri utendaji wa urejeshaji katika taarifa za lugha tofauti.
Miongoni mwa madhumuni muhimu ya kamusi ni kumsaidia mtumiaji wa Kamusi kujua maana za maneno. Kwa hali hiyo maneno yanapata kipaumbele cha kuingizwa katika Kamusi ni yale yanayowakilisha dhana fulani. Kuna baadhi ya Kamusi ambazo huangazia uwanja fulani kama vile Kamusi ya sanifu ya biolojia, fizikia na kemia. Ensaiklopidia hurejelea taarifa nyingi sana kuhusu uwanja wa uchumi na pia luhga za fasihi ambazo hazipatikani katika Kamusi za lugha ya mwanafunzi. Bora ni yule ambaye hufanya utafiti zaidi kwa kutumia Kamusi ili kuelewa maana zaidi ya maneno. Hata daktari hutumia kamusi ya kiingereza ili kujua matumizi ya dawa mbalimbali.