Huduma kwa jamii ni Hali ambapo watu hufanya mambo mbalimbali kwa watu wa jamii ili wanufaike. Kuwatibu wagonjwa bila malipo na kuliwaza watu waliofiwa , kuwalisha watu, kufyeka miji mbalimbali na kutunza mazingira.
Aliyekuwa rais mstaafu uhuru Kenyatta ndiye mwanzilishi wa mradi iitwao kazi kwa vijana. Lengo lake kuu ilikuwa kuwasaidia vijana ambao hawakuwa na ajira.Baada ya kazi kwa vijana rais William Ruto alizindua ” hustler fund” ambapo vijana wanashauriwa kuchukua mkopo ili wafanye biashara.wanafunzi vile vile wanaweza kuhusika katika huduma za jamii wakiwa bado shuleni ili wapate ujuzi kamili ya kufanya kazi mbalimbali.wanapofagia darasa , kufyeka nyasi wanajihusisha katika huduma katika shule zao.
Wanaweza kufanya huduma haya kwa kuwatembelea watu wasiojiweza wanaoishi karibu na shule na kuwapa misaada kadha wa kadha misaada hiyo inaweza kuwa kusafisha nyumba zao.kuwafulia nguo zao, kuwapatia chakula na kusafirisha maboma Yao. Wanafunzi Wanapofanya haya, wanapata fursa ya kuwa watu wenye kuwajibika katika kuwa jamii.
Huduma kwa jamii ni muhimu kwasababu inaimarisha mshikamano wa jamii na wa Taifa. Taifa lenye watu wanaosaidia hukua kwa Kasi na kwa upendo mkubwa sana. Watu pia wanaposaidia katika jamii , hupata baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu.kwa hivyo wanafunzi wanapaswa wawe watu wanaohusika katika kuhudumia watu wa jamii ili wakue wakiwa watu wenye nidhamu na mshikamano.mshikamano ni Hali ya kufanyakazi kwa pamoja na kukuza Talanta kupitia Talanta hela mtaani.
Kumbuka kwamba unapomsaidia mtu katika jamii , si lazima msaada huo uwe wa gharama ya juu mno. Msaada wowote ule ni muhimu katika jamii.hata ingawa ukawa kidogo zaidi kupita kiasi ni Bora kushinda bure. Hii ndiyo maana Mpesa foundation kupitia Radio citizen inawachangi watoto ambao hawajafaulu kujiunga na kidato Cha kwanza , wapate masomo. Ni muhimu kwa mtu ambaye anahitaji kutoa ni moyo usambe ni utajiri.kwa hivyo tusaidiane katika jamii ili tuishi maisha mema kila wakati.
Ni vyema kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta utangamano.
Hali ya utangamano hujitokeza wakati wanafunzi kutoka jamii mbalimbali.wakati wa michezo wanafunzi hukusanyika kama kama jamii moja . Katika grade ya tatu mtaala huu wa umilisi yaani”c.B.c.”wanafunzi waliende kufagia soko, Hali hii ni utangamano.wakati wanakua watu wazima watajifunza jinsi ya kuishi kama jamii moja na kuepuka vita vya mara kwa mara.
Ukuzaji wa Talanta kupitia sayansi ya nyumbani, ambapo wanafunzi wasoma vyakula kadha wa kadha, na mbinu za kupika chakula kule jikoni.
Pindi tu wanapokamilisha masomo Yao watakuwa na ujuzi wa kukabiliana na Hali ngumu ya maisha.kufanya huduma kwa jamii ni kujitolea .mfano Bora ya huduma katika jamii ni vijana wa huduma kwa Taifa almaarufu ” N.Y.S.” kikundi hiki hukuza vijana huku wakijifunza kazi na Sanaa mbalimbali kama vile ujenzi wa nyumba , uchoraji , uhandisi na pia kuwa mhunzi. Baada ya kupata ujuzi wao hutoa huduma kwa Taifa kama vile kuchimba mitaro ya maji , kusaidia polisi kuboresha usalama Wakati wa uchaguzi Kijijini. Miji yetu wakati mwingine Huwa chafu mno , watu hutupa takataka ovyovoyo, vijana wa huduma kwa Taifa hutumiwa kusafisha miji yetu.wanapofanya hivyo wanadumisha uzalendo.
Waziri wa afya Bi. Susan Nahumicha ametia bidii kuwaajiri wahudumu wa nyanjani . Wahudumu Hawa wamewasaidia wanchi katika jamii kupata matibabu.kwa wale ambao hawawezi kufika hospitalani .watu ambao ni wazee hawana nguvu ya kutembea hata kituo Cha afya. Rais William Ruto pia amepiga jeki jambo hili kwa kuwaajiri wahudumu wa nyanjani ili kuwasaidia wagonjwa. Huduma ya kwanza humwacha mgonjwa na matumaini. Wahudumu wa nyanja husaidia kuepuka vifo vingi katika jamii na kuokoa maishi. Wale wagonjwa ambao wanahudumiwa bila shaka wanapatiwa dawa.
Shuleni kilabu Cha masksuti huchangia katika kusafisha mazingira.wao huhakikisha kwamba mazingira ya shule ni safi na hayana vifaa ambavyo vinaweza kuhatarisha usalama wa wanafunzi shuleni. Vitu hivi huweza kuwa mashimo na mianya ya maji inayoteremka. Masksuti pia huokota takataka shule, kama vile Ganda la ndizi ni hatari mno , Huwa ni telezi, unapoikanyaga bila kujua, ajali inaweza kutokea, ni vyema tuwe makini kila mara.
Wanaskauti hutoa huduma ndogo ndogo wanapokuwa shueni kwa wanafunzi waliozirai, wanaskauti Huwa wamefunzwa namna ya kutoa huduma ya kwanza kuhusu matukio ya kuzirai. Pia Kuna baadhi ya wanafunzi hutokwa na damu baada ya kukimbia , hutokwa na damu puani. Ni jambo la kutia moyo kuwa wanaskauti huwasaidia wanafunzi Hawa. Vilabu shuleni ni muungano wa wanafunzi walio vijana lengo lao ni kusaidia jamii.
Ni Bora wanafunzi kutoa huduma katika jamii kwasababu wao ndio viongozi wa kesho . Bali na wanaskauti chifu pia hutoa huduma kwa jamii wao hupasha polisi kuhusu pombe haramu, tusisahau wazee wa mtaa ambao wamekuwa ngunzo muhimu kuboresha usalama Kijijini. Tukitia bidii kusaidia chifu kutoa huduma, basi pombe haramu itapungua kabisa