2.1 C
London
Tuesday, January 21, 2025
HomeCommunityMASAIBU YA PIKIPIKI MJINI BUSIA

MASAIBU YA PIKIPIKI MJINI BUSIA

Date:

Related stories

Behaviour Management in Children

Understanding and Guiding Children's Behaviour: A Practical Approach Raising children...

What’s New in the Latest ChatGPT: Enhanced Features and Capabilities

The latest version of ChatGPT, powered by GPT-4, has...

The Silent Revolution: How Tech Schools Are Transforming Lives in Nairobi’s Slums

In the heart of Nairobi’s bustling informal settlements, a...

The Rise of Kenyan E-Sports Culture: A New Frontier for Youth in Nairobi

When you think about gaming, there's a thought of...

People Turning to Nature for Toilet Paper

In a bid for sustainability, some individuals are cultivating...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Pikipiki ni chombo cha usafiri kilichofana na baiskeli Lakini kinachoendeshwa kwa nguvu za mota . Katika gatuzi la Busia pikipiki zimesababisha vifo kwa wateja . Waendeshaji pikipiki wauwauwa kila siku bila hatia . Ingawa visa hivi vimeripotiwa katika kituo Cha polisi , mjini Busia , bado wananchi wanalalamika kuhusu usalama wao na waendeshaji kwa ujumla.Ni jambo la kuvunja moyo , baada ya kuchukua mkopo na kununua pikipiki mpya, utawaona magenge ya majambazi wakivamia boma lako. Kwa Nia ya kuiba pikipiki yako. Maeneo ya Burumba na marachi imepoteza waendeshaji wengi wa bodaboda kila mara.
Uchukuzi ni sekta muhimu katika nchi . Baadhi ya vyombo vya uchukuzi ni kama vile pikipiki, garimoshi, Meli na matwana . Uchukuzi ni shughuli ya kusafirisha mzigo kutoka sehemu moja hadi nyingine . Pia binadamu husafirishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine kote nchini.

Mwendeshaji wa pikipiki huhitaji kuwa mwangalifu zaidi iwapo pikipiki ltaanguka huenda litasababisha hasara kubwa.usafiri ambao imebainika kuwa maarufu sana siku hizi ni ule wa pikipiki. Almaafrufu kama “bodaboda” awali pikipiki zilimilikiwa na wachache sana, wenye vyao, na matumizi yake yakijikita sana katika mashindano.
Hali kadhalika pikipiki huweza kupenya katika nafasi ndogo kwenye Barabara za miji ambako Huwa na msongamano mikubwa wa magari . Wananchi wanaoraukia kazi zao mapema wanahitajika kuwahi kazini na kujiepusha na hatari ya kumwaga unga.

Pikipiki huweza kumchukua abiria popote hata kama hapana barabara nzuri au kutuo maalum . Unachohitajika ni kupiga simu tu au kusubiri moja ipite.
Mjini Busia pikipiki hizi mara nyingi huendeshwa na magenge ya vijana ambao wakati mwingine huwahangaisha raia bila hatia .kutokana na wapesi wake wa vichochoroni . Wahalifu huzitumia sana kutoweka baada ya kutimiza ada zao. Pikipiki zimewahi kushuhudia visa vingi vya watu wanaofyatua risasi wakiwa kwenye pikipiki Kisha kutoweka.

Visa vya abiria wa kike na hasa wasichana wa shule kudhulumiwa kimapenzi pia vimekuwa vikiripotiwa mjini Busia. Imebainika kuwa wengi wanaoziendesha pikipiki hizi mjini Busia, Huwa hawajahitimu mafunzo ya uzingatiaji wa kanuni za barabarani. Utawaona wakipitia upande mbaya wa Barabara huku wameziendesha kwa Kasi na kupiga honi mithili ya wehu au Hali ya kutokuwa timamu , Hali ya kukaribia uwenda wazimu.

Uendeshaji wa aina hii huwasababisha kuvunjika viungo vya mwili, kuwaumiza abiria wao au watumiaji wengine wa Barabara. Ni ajabu kusikia kuwa polisi wa trafiki hufumbia macho uovu huu.ili kuwa salama kazini , Gavana wa Busia Paul Otuoma , ametia tahadhari kuwa anayeendesha pikipiki Hana budi kuvalia mavazi yatakayomstiri dhidi ya hatari Zinazoweza kumkabili katika kazi yake.
Helmeti hupunguza uwezekano wa kupata majeraha kichwani. Iwapo ajali itatokea . Baridi Kali aidha inaweza kusababisha matatizo ya kitaifa kama vile kifua kikuu. Ipo jaketi maalum la kuakisi mwangaza ili watumiaji wengine wa Barabara, waweze kumwona mwendeshaji kwa urahisi. Kwa hivyo pikipiki zimeimarisha pakubwa sekta ya usafiri nchini. Ni bora serikali na wakishadau wengine kwa kweli hawana budi kudhibiti mambo mbalimbali yanayoutia doa usafiri wa pikipiki.

Ni jambo la kutia aibu sana. Kila abiria ana haki kuwa na starehe wakati wa usafiri. Ni Bora pia waendeshaji wa pikipiki kuweka mavazi Yao kuwa safi. Kufua jaketi, na Kisha kubadilisha mavazi ya wakati wowote . Jambo hili litawasaidia kuvutia abiria wengi barabarani.
Wakati unapoendesha bodaboda yako ni vyema kuepuka vileo. Mwendeshaji wa pikipiki ni Bora kuepuka dawa za kulenya .abiria wengi hufurahia wakati wanafika nyumbani salamu. Kamishna wa Busia amewaonya waendeshaji wa pikipiki dhidi ya kutumia dawa za kulenya. Ni matumani yangu kuwa watatilia manani wito Wake.

Muziki ni mpangilio wa sauti za ala .uimbaji au vyote viwili unaoleta athari fulani kwa kumbe. Ili kuzingatia Sheria Bora barabarani, waendeshaji wa bodaboda wanashauriwa wasiweke muziki kupita kiasi . Muziki wa juu itaathiri mteja wake akiwa ana shida ya masikio . Vyombo vya kusafiria nchi kavu ni kama vile matwana au daladala , tukutuku , teksi , pikipiki, mkokoteni au rukwama , garimoshi au treni na baiskeli.

Waendeshaji wa pikipiki bado wanazidi kuiomba idara ya polisi kuchunguza kiini Cha mauaji , si si ajabu kusikia waendeshaji wa pikipiki wanaishi na uoga sana, kwasababu hawana uhakika wa usalama wao . Biashara ya uchukuzi mjini Busia Ina masaibu ya kuwapoteza wapendwa wao. Nina matumani kuwa kamanda wa polisi katika gatuzi la Busia atashughulikia suala hili za masaibu ya bodaboda haraka. Biashara ya bodaboda inaponoga ni Bora zaidi. Bodaboda wasitumike katika siasa Bali ujenzi wa Taifa Bora. Jambo hili litawasaidia kuanzisha biashara zao na vurugu itapungua na pia uhalifu.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img