
Tokea zamani mwanadamu amekuwa mstari wa mbele kujiimarisha kutoka kiwango kimoja hadi kingine kimaisha.Baadhi ya mambo ambayo mwanadamu ameyafanya ili kuweza kujikuza ni kama vile ufugaji,ukulima na biashara.
- Mbuzi ni mojawapo wa mifugo waliopendelewa sana na binadamu hata katika maisha ya sasa sababu kuu ikiwa gharama yake ya kumtunza si ghali ikilinganishwa na mifugo wengine kama ng’ombe.

- Mbuzi ameonekana kuwa mnyama wa ajabu kwa kuwa ana upekee wake tofauti na wanyama wengine.Ufugaji wa mbuzi una gharama duni kwa kuwa chakula chake kinapatikana kwa urahisi.Ushahidi wa kauli hii ni kuwa katika maeneo ya ukame ufugaji wa mbuzi unafanyika.Mbuzi anakisiwa kula matawi ya miti na hata kuokota matawi hayo yanapodidimika ardhini wakati wa ukame.Jamii za ufugaji zinaeleza kuwa muda mwingi mbuzi uimarika kiafya wakati usio wa mvua.

Mbuzi wana faida kemkem Kwa binadamu.Mbuzi humpa mfugaji maziwa,nyama na hata pesa.Maziwa ya mbuzi yanapendelewa zaidi hasa Kwa kuwalea watoto ambapo inanuiwa kuwa na nguvu zinazohitajika kumuwezesha mwana kukua haraka.
Vile vile, mfungaji anaweza kuuza mbuzi akapata hela za kujikimu kimaisha.Mbuzi wana nyama inayo pendwa na jamii nyingi barani Afrika na hivyo wapo wafugaji wanaofuga mbuzi kwa ajili ya kupata chakula.