4.9 C
London
Sunday, December 22, 2024

MIKASA

Date:

Related stories

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities In the...

Challenges Facing the Kenya’s Current Socio-Political Landscape

Kenya's current socio-political landscape is shaped by a series...

A Global issue about Female Genital Mutilation

Female Genital Mutilation (FGM), also known as female circumcision,...

Faida Ya Kupanga Uzazi

Upangaji uzazi ni muhimu sana katika familia, inahusu wanandoa...

Madhara Ya Vita Katika Jamii

Hali ya majonzi ilitanda katika kaunti ya Tana River....
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes

Je, Mikasa ni nini katika jamii? Mbona kila wakati Mikasa hutokea katika miji mbalimbali. Serikali Ina mikakati ipi ili kukabiliana na Mikasa hii? Hata hivyo Mikasa ni matukio au mambo ya kutisha yanayotokea,matukio haya hutokea kwa ghafla bila kutarajiwa.mikasa haya yanaweza kuwa na madhara makubwa kwa binadamu.Baadhi ya Mikasa ni kama vile ajali ya ndege , mlipuko wa gesi , moto , mlipuko wa bomu , maporomoko, mlipuko wa volkano na zilizala.

Ajali barabarani hutokea iwapo madereva watakiuka Sheria za barabarani.Pia wakati gari ambalo dereva hutumia Ina matatizo chungu nzima. Kama vile ukosefu wa breki , dereva kuendesha kwa mwendo wa Kasi ama dereva anapokiuka Sheria za barabarani, huko maeneo ya Busia katika sehemu ya Mundika kulitokea ajali ambapo trela ilichomeka na kugongana na gari ya Tacmed. Watu wengi walijeruhiwa na wawili kuaga dunia.

Katika kivuko Cha Likoni ferry kulitokea ajali ambapo mwanamke kwa majina Miriam kaghendu na Binti yake Amanda Mutheu walifariki baada ya gari lao kutumbukia majini. Wapigambizi kutoka Afrika kusini waliwasili nchini kwa makundi wawili ili waanze kazi ya kutafuta miili ya wapendwa wawili Hawa. Mkurugenzi mkuu wa shirika la Ferry nchini kenya bwana , Gowa , alisema ni Bora abiria wapate mafunzo kuhusu ferry ili kupunguza baadhi ya ajali hizi kabisa.

Wakati abiria wanapanda ferry ni Bora kuhakikisha kuwa milango iko sawa.Tukifanya hivyo itakuwa vigumu sana kwa mtu kutumbukia ndani ya maji .pia wananchi wakiingia ndani ya ferry ni Bora wazime magari Yao. Kwasababu gari linaweza kutumbukia ndani ya maji.
Kunapaswa kuwa na watu ambao wako pale kila wakati, ikiwa mtu ataanguka baharini, wanaweza kupiga mbizi na kumwokoa lazima kuwe na ( drill ) yaani majaribio kila mara ili watu wawe na uzoefu. Aidha wataalamu wanakiri kuwe na boti za kutosha na mabaya ya kujiokoa wakati wa ajali.

Kivuko cha Likoni ferry kimekuwa na ajali za kushangaza mno.kuna mwanamke ambaye alijaribu kumptupa mtoto wake ndani ya maji . Baadaye wapigambizi walijitolea mhanga Kisha wakaokoa mtoto huyo . lnadaiwa kuwa mwanamke huyu alikuwa na shida ya kiakili . Hatimaye alikamatwa na maafisa wa polisi . Likoni ferry Imewasaidia maabiria wengi kupata usafiri ili kuendelea na shughuli zao za kila siku.

Feri ni mahali ambapo abiria, mizigo, au magari hubebwa kwa boti kuvuka mto , ziwa , mkono wa abiria au sehemu nyingine ya maji .Bahari Huwa na hewa safi pia .Inaweza kuwa nzuri Kwa afya ya binadamu pamoja na kuwa hatari ndogo ya kuendeleza Hali usafiri Bora.

Bali na ajali kumeripotiwa visa ambazo hutokea ndani ya Likoni ferry ambazo hukera mno.Wanaume kadhaa wamepatikana na hatia na kufungwa jela kwasababu ya kuwavuzia na kuwashika abiria wanawake makalio.mtu mmoja anahudumia kifungo jela baada ya kupatikana na hatia katika kivuko Cha Likoni ferry. Isitoshe mwanamume mmoja alipigwa na abiria alipojaribu kumpiga busu mwanamke ndani ya feri.

Ni Bora kuvalia jaketi ili kujisaidia wakati wa ajali. Japo ajali Huwa ni jambo la dharura. Bali na wapigambizi jamii Ina maoni tofauti kuhusu ajali ya ferry. Wanasema kuwa ” bahari Ina wenyewe” wenyeji wa pwani ambao wanadai kwamba janga kama la ajali likitokea , sala maalum inapaswa kufanywa ambayo inahusisha kuchinjwa kwa mnyama na Kisha damu yake kumwagwa kwenye miili ya tukio ili kusababisha miili ya waathiriwa kujitokeza adharani.


Mlipuko wa gesi .Mlipuko huu ni janga ambalo limewaacha watu na maswali mengi mioyoni. Hata hivyo ni Bora kufahamu kuwa ajali Haina Kinga. Katika eneo la Embakasi kulitokea mkasa wa mlipuko wa gesi .Watu wengi wakijeruhiwa, Kisha wengine kuiaga Dunia kutokana na majeraha mbalimbali. Ni Bora serikali kufanya utafiti wa wakutosha kabla kusajili , kampuni kuanza biashara. Wakifanya hivyo Mikasa itapungua.

Mafuriko ni Hali ya maji kujaa kupita kiasi katika sehemu Fulani. Katika kaunti ya Mombasa kumeshuhudiwa mafuriko zaidi. Hii ni baada ya mvua kunyesha kupita kiasi.Barabara nyingi zilikuwa na shida ya usafiri. Mwaka wa elfu mbili ishirini na tatu .Wakazi wa Mombasa walipitia maafa mengi kwasababu ya mvua nyingi. Watu waliamua kuhamia sehemu mbalimbali baada ya mto Ramisi kuvunja Kingo zake. Mvua Huwa na faida kwa wakulima na pia hasara wakati Mikasa hutokea.

Katika kaunti ya Busia eneo la Budalangi wakazi wemeshuhudia janga la mafuriko. Watu wengi wamehama katika majumba Yao kisha kupata hifadhi katika shule na makanisa . Natumai kuwa serikali itashughulikia jambo hili ili suluhisho ya kudumu ipatikane kwa haraka. Ikiwa jumba halitajengwa vyema itasababisha maporomoko.Maporomoko ni Hali ya jumba kubomoka.kaunti ya Nairobi imeshuhudia maporomoko ya vyumba kuanguka ,kisha kusababisha vifo na uharibifu wa Mali ya wananchi. Zilizala ni tetemeko la ardhi au mtetemeko. Ili wananchi kuepuka baadhi ya Mikasa ni Bora wawe makini zaidi kila wakati.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img