Ilikuwa siku ya furaha mno wakati wakenya waliamka asubuhi na mapema kupiga kura zao. Kila mmoja alikuwa na matumani chungu mzima. Shule zilifungwa mapema ili kupisha uchaguzi mwaka wa elfu mbili na kumi na mbili. Kampaini zilipanda moto kupita kiasi, hii ilikuwa thibithisho ya kupata viongozi wapya na mabadiliko.
Mwaka wa elfu mbili na ishirini ta tatu ilikuwa mwaka wa ajabu sana na matatizo chungu mzima kama ifuatayo. Kipindi Cha maandamano. Matokeo ya uchaguzi ilileta utata. Mrengo wa azimio ulikataa kutambua rais William Ruto kama rais , baada ya jaji kutoa kauli ya mwisho kuwa, mrengo wa kenya kwanza ilishinda uchaguzi . Mrengo wa azimio walianza maandamano katika mji wa Nairobi . Jambo hili lilisababisha uharibifu wa Mali na pia shule zikafungwa huku biashara kusitishwa mjini Nairobi.
Mswada wa fedha . Ilikuwa jambo la kusikitisha wakenya wengi mwaka wa elfu mbili na ishirini na tatu . Baada ya bajeti kusomwa, kulikuwa na mswanda kuhusu ujenzi wa nyumba kwa kila mkenya. Ingawa wakenya wengi walitoa maoni Yao na kukataa mswada wa ujenzi wa nyumba, wabunge wote wa kenya kwanza waliunga mkono . Wale wa azimio walijaribu kupinga, . Lakini idadi Yao ilikuwa chache mno. Hatimaye mswada huu ukawa Sheria. Kila mwezi sasa hivi walioajiriwa na serikali wanakatwa hela hizo za ujenzi wa nyumba.
Uzinduzi wa Talanta hela . Waziri wa michezo Ababu Namwamba alizindua kikundi maarufu kwa vijana yaani, “Talanta hela” kijana yeyote aliye na ujuzi alipata fursa kujitokeza . Makocha wengi wakiandaa timu zao katika Kaunti arobaini na saba. Hatimaye wachezaji maarufu kama kibet walichipuka , kuchezea klabu zao . Jambo hili lilisisimua wengi hadi kenya ikaandaa mashindano ya “Cecafa”katika gatuzi la Kisumu .mabigwa wa Cecafa walikuwa waganda, baada ya kushinda wakenya , kwa mabao mbili kwa moja.
Matokeo ya utata ya ” kcpe” wanafunzi walitia bidiii zaidi katika kujianda vyema, wakiwa na matarajio baaada ya kusoma miaka nane, watapata matokeo Bora. Waziri wa elimu bwana Ezekiel Machogu alipotangaza matokeo Yao, kuwa tofauti zaidi, wengine walikosa baaadhi ya masomo , badala ya kuwekewa somo la kiswahili , ni ajabu kuwa wengine waliwekewa, ” sign language” yaani lugha ya ishara. Pia gredi za alama hizo zilikuwa na hitilafu chungu nzima, baadhi ya shule ziliamua kuwasilisha kesi kuhusu matokeo Yao. Hata wanafunzi wengine kuwasilisha kesi mahakamani.
Giza nchini kenya. Nchini kenya katika anga tua la Jomo Kenyatta wasafiri wa kuenda ngambo waliteseka sana. Kila mahali kulikuwa na Giza Totoro. Ukosefu wa umeme uliwafanya wasafiri kuchelewa kufika nyumbani , Kuna baadhi ya wafanyibiashara walipata hasara hasara chungu nzima, nyama, samaki ziliharibika kwenye ghokofu, jambo hili lilimfanya waziri wa Barabara kipchumba murkomen kuwaachishwa baadhi ya viongozi kazi.
Wagonjwa ambao walikuwa katika chumba Cha upasuaji walipata shida mno. Ni vyema kufahamu kuwa umeme ulipotea mara tatu kote nchini kenya mwaka wa elfu mbili ishirini na tatu . Tatizo hili bado lipo katika gatuzi la lamu.
Mhubiri tata Paul Mackenzie . Dini ni Mali ya roho. Kila mkristo huenda kanisani ili kupata chakula Cha roho. Ni jambo la kushangaza kisikia kuhusu majonzi kule kilifi. Waumini wa kanisa la ” New life international ” walipigwa na na butwaa , hili ni baada kanisa hili kudaiwa kunyonga na kuua wakristo wengi , kutoka maeneo mbalimbali za nchi. Watoto wengi na kina mama walifariki . Jambo hili lilimfanya mhubiri Paul Mackenzie na washirika wake kutiwa mbaroni , hadi sasa kesi Yao inatatuliwa . Waumini wa kanisa hili walinyimwa chakula na hata maji ya kunywa wakidai wanafanya maombi ya kufungua . Ni jambo la kuvunja moyo, kuwa hata baada ya mhubiri huyu kukamatwa anawaambia askari kuwa ,”mnachokichezea hamjui nyinyi nini , hatimaye kitawaramba”
” The word coin” leo ni leo asemaye kesho ni mwongo. Mjini Nairobi ilikuwa imefirika na maelfu ya wakenya wakiwa na furaha moyoni. Ujio wa ” world coin” iliwasisimua zaidi, shughuli kuu hapa ilikuwa kupigwa picha wakenya kwenye mboni ya macho. Wabunge walikashifu sana dhana hii ya wakenya kupewa pesa baada ya kupigwa picha . Pia data za wakenya zilihifadhiwa kwenye mitambo hizo. Ilibainika kuwa ukosefu wa ajira nchini kenya , iliwafanya wakenya kunaswa katika mtego wa “world coin” .
Bei ya mafuta kupanda .kila abiria ana haki kufika nyumbani mapema kila wakati . Madereva walijipata taabani baada ya Bei mafuta kupanda maradufu . Uchukuzi ilikubwa na tatizo chungu mzima, nauli iliongezwa si ajabu kisikia. baaddhi ya wakenya walishindwa kusafiri nyumbani kwa sherehe za Christmasi Imekuwa ni mwaka mgumu sana kwa wakenya, kwa jumla . Waliopwa pikipiki za umeme wameshindwa na kuendesha pikipiki hizo wakidai kuwa kuongeza moto ” “battery ” huwapotezea muda zaidi .Wengi wao wanadai wameshindwa kulipia mkopo. Buriani mwaka elfu mbili ishirini na tatu , karibu elfu mbili mbili ishirini na tatu .