9.2 C
London
Wednesday, December 25, 2024
HomeEducationSababu Wanafunzi Wanahamia Shule za Umma

Sababu Wanafunzi Wanahamia Shule za Umma

Date:

Related stories

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities In the...

Challenges Facing the Kenya’s Current Socio-Political Landscape

Kenya's current socio-political landscape is shaped by a series...

A Global issue about Female Genital Mutilation

Female Genital Mutilation (FGM), also known as female circumcision,...

Faida Ya Kupanga Uzazi

Upangaji uzazi ni muhimu sana katika familia, inahusu wanandoa...

Madhara Ya Vita Katika Jamii

Hali ya majonzi ilitanda katika kaunti ya Tana River....
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Elimu ni sehemu muhimu kuinua watoto na kuwaandaa kuishi maisha Bora. Shule za umma ni ambazo hufadhiliwa na serikali ilhali shule za kibinafsi humilikiwa na mtu au mkurugenzi. Ni jambo la kushangaza kuwa wazazi wengi wametoa watoto wao katika shule za kibinafsi, Kisha hatimaye kupeleka katika shule za umma.

Kuna sababu kadhaa ambazo huchangia jambo hili kama ifuatavyo.wazazi waliokuwa wakimudu kwa urahisi elimu katika shule za kibinafsi sasa wamejipata wikingangana kutokana na misikosuko kazini , mishahara Yao ikipunguzwa , mfuko ikiwa na upungufu mkubwa sana.kutokana na Bei ya bidhaa kupanda kupita kiasi.

Idadi ya wanafunzi waliohamia shule ya kibinafsi kuenda shule za umma ni kubwa mno , idadi hii imeongezeka kwa asilimia Tano katika shule za mjini Nairobi. Sababu kuu ni kuwa wazazi wanalazimika kuhusu ongezeko ya karo, pia wameshindwa kununua vitabu ilhali katika shule za umma wanapatiwa vitabu bila kulipa yoyote kila Wakati.

Ukosefu wa miundomsingi. Miundomsingi ni kama ujenzi wa madarasa , maabara na msala.ikiwa shule itakosa miundomsingi bila shaka wazazi watakuwa na changamoto.lengo kuu ya wazazi kuhamisha watoto wao mwezi wa januari ni ukosefu wa miundomsingi.familia zinalalamika kubadilisha matumizi Yao ya fedha huku gharama ya elimu ikibadilika kuwa suala la kutilia shaka zaidi.

Maliliaoni ya madeni. Wasimamizi wa shule za kibinafsi wamesema kuwa wazazi Wana madeni chungu nzima .wazazi Hawa wanarai mkurugenzi wawaruhusu watoto wao wasome Kisha watalipa pesa baadaye .Hii ni kwasababu wamejadiliana na walimu wakuu kuwa watalipa pesa wakifanikiwa katika biashara zao za kila mara.

Ni jambo la kuvunja moyo katika muda wa miezi miwili pekee, katika shule ya msingi ya Bungoma “DEB” imepokea zaidi ya wanafunzi mia tatu wapya waliotoka katika shule za kibinafsi almaarufu “academy”
Magonjwa kadha. Ugonjwa wa COVID-19 mwaka wa elfu mbili na ishirini wazazi wa Edna bi Jacinta manthi na Geoffrey manthi . Ni baadhi ya wazazi waliohamia kuishi kanisani kupata hifadhi ya muda.waliposhindwa kulipa Karo na Kodi ya nyumba.

Wazazi wa precious, bi Miriam na bwana Peter muendi na Boniface mumo hawana kazi , familia zote mbili zilipitia magumu baada ya wazazi wa pande zote mbili walifutwa kazi kutokana na ujio wa janga la korona , kwa hivyo watoto wao wameenda kusomea shule za umma.malalamiko ya wazazi kuhusu Hali ngumu ya maisha inayowapelekea wazazi wao kutoweza kuwapeleka watoto wao shuleni kusoma . Bei ya juu ya vitabu vinavyotakikana shuleni , kulingana na gharama hii, Karo ya juu na ukosefu wa fedha ya mahitaji mengine yamekuwa vizuizi kwa wazazi hao kuweza kutoa watoto wao katika shule za kibinafsi. Ili hizi fedha zitumiwe katika mahitaji mengine muhumu kama chakula.

Janga la ujamzito. Bali na ukosefu wa karo, wanafunzi wengine wamekosa kurudi shuleni baada ya kupatwa na ujauzito ana wengine kuolewa mapema , kwasababu ya Hali ngumu ya maisha . ujamzito huu ulichangiwa na janga la korona ambapo wanafunzi wengi walikuwa nyumbani.

Ukosefu wa walimu wa kutosha. Ukosefu wa walimu wakutosha .suala la kutokuwa na walimu ni changamoto, kwani walimu wanalazimika kuwasihi wazazi kuongeza kiasi Cha karo ndipo waweze kuajiri walimu wengi. Madarasa yapo lakini walimu ni wachache, kwa hivyo wazazi wanahofia watoto wao hatakosa masomo.

Msongo wa mawazo.kulingana na utafiti, wazazi wengi wamekumbwa na msongo wa mawazo . walisema gharama ya juu ya maisha imekuwa na athari kwa uhusiano wao wa kibinafsi. wazazi wengi wamekuwa na tatizo la kiafya huku wengine Wana matatizo ya kiakili.jambo hili huwafanya wazazi kutumia hela nyingi kwa matibabu huku wakishindwa kugharamia karo ya kulipia elimu.
Ukubwa wa madarasa katika shule za umma. Katika shule za umma madarasa ni kubwa na hutosheleza wanafunzi vyema. Ikichukua idadi ya wanafunzi kati ya ishirini hadi thelathini.wakati shule nyingi za kibinafsi zikiweka ukubwa darasa zao kuwa wastani na wanafunzi Huwa na idadi kumi hadi kumi na Tano.

Pia ni muhimu kutambua kwamba shule za kibinafsi zinasambaza wanafunzi kwa uwiano na walimu , kwa kuongeza au wakati mwingine hutenga wanafunzi kulingana na kiwango Cha jinsi wanavyoelewa mambo.kuna makundi mbalimbali wale ambao huwaelewi mambo hudharauliwa na kutengwa.katika shule za umma kila mwanafunzi ni muhimu na Kuna usawa wa kiwango katika masomo.

Shule za kibinafsi ni rahisi kufugwa. Hii ni wakati wazazi wamelemewa na mzigo wa karo.ili shule za kibinafsi zinawiri vyema . Wazazi wanafaa kuchangia kwa kiwango kikubwa kulipa karo kwa wakati.shule za umma hufadhiliwa na serikali kwa hivyo si rahisi kufungwa kwa haraka wakati Kuna janga .kwa kijumla wazazi wameathirika na janga kama kupanda kwa bidhaa sokoni,mafuta ya diseli na petroli na nauli zimewapiga chenga.gharama ya elimu nchini imekuwa ghali mno.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img
Previous article
Next article