Furaha ya wananchi ni kuishi maisha ya Raha na starehe. Mwananchi mzalendo ni yule anayependa nchi yake na kupigania. Si ajabu nchini kenya mambo ni tofauti. Je, mbona wakenya wengi wanasafiri nchi za ng’ambo? Nini huchangia wao kusafiri. Hata idadi ya wengine wamefariki kule Saudi Arabia wakifanya kazi za nyumba. Jambo hili limewashangaza watu wengi nchini kenya. Ifuatayo ni sababu wakenya wengi wamesafiri kuenda ng’ambo kwa muda Fulani.
Kujiendeleza kielimu. Elimu ni njia moja ya kujipatia maarifa zaidi . Si ajabu kusikia wakenya wamehamia nchi za nje. Baada ya kupata shada na pia stashahada, ikiwa mtu angependa kujiendeleza kielimu, bila shaka atasafiri. Hata hivyo ikiwa amepata ufadhili wa kugharamia masomo yake. Ili kufanikisha lengo lake kimasomo, ni Bora kukata kauli na kuenda ng’ambo.
Nchini kenya kupata kazi imekuwa vigumu mno. Baada ya wanafunzi kukamilisha masomo Yao. Imekuwa kibarua kigumu kwa wao kupata ajira Hali hii imewafanya kuishi maisha ya mahangaiko. Pia kazi ambazo hupatikana ni duni Sana. Familia zao zimeishi maisha ya kuhagaika. Ili kujipatia kazi ya malipo Bora kuenda nchi za ng’ambo kama Amerika, Saudi Arabia au hata Tanzania. Mfano nzuri ni mwanadada anayeitwa Rose . Baada ya kufanya kazi vyema, aligonga vichwa vya vyombo vya habari.
Raha ya kazi ni malipo Bora. Kuna baadhi ya waajiri ambao wanawatesa wafanyikazi sana. Mshahara wao kila mara huchelewa. Wale ambao hufanya kazi katika sekta za kibinafsi wanalia sana. Mtu anawezafanya kazi miezi tatu bila kupewa mshahara wake. Malipo haya pia kwa wakati mwingi Huwa ni kidogo sana. Haiwezi kutosheleza mahitaji ya familia zao. Ili kuboresha maisha ya familia Yao ya baadaye wao huamua kusafiri ng’ambo.
Ni jambo la kushangaza mno nchini kenya. Eti mwalimu baada ya kufuzu, lazima afanye kazi ya kandarasi miaka mbili kabla kuajiriwa. Je, nani Yuko tayari kuvumilia miaka hizi zote ? Na iwapo utavumila mshahara ya elfu kumi na saba ni kidogo mno. Kila mtu ako mbioni kuboresha maisha yake . Tamaa ya kuajiriwa mapema hufanya watu wengi kusafiri kuenda ng’ambo ili kupata kazi kwa haraka.
Wakimbizi wa kisiasa. Nchi nyingi Huwa na shughuli tofauti kama vile siasa au hata sherehe za kitaifa , baada ya uchaguzi wa mwaka wa elfu mbili ishirini na mbili . Kuna baadhi ya makamishina wa tume ya uchaguzi nchini kenya.waliamua kusafiri kwasababu ya kuhofia usalama wao. Ikiwa pia Kuna vita katika nchi. Bila shaka utawaona wageni wakisafiri ili kuepuka janga hili. Pia ukame huchangia watu kusafiri.
Umaskini ni hali ya kukosa mahitaji muhimu. Kama vile lishebora , elimu na hata makazi Bora . Huku mjini baadhi ya wakenya wanaishi katika mitaa duni kama vile kibra na korokocho.maisha ya wakazi Hawa ni magumu sana. Vile kuboresha Hali ya maisha Yao pamoja na familia zao. Utapata wasichana wengi kutoka mtaa duni hizi wameenda ng’ambo ili watoke katika Hali hii ya umaskini. Si kina dada pekee ambao huenda ng’ambo pia wanaume.
Kuna watu ambao hupenda sifa tele.maishani mwao wao wangependa kutambulika. Hata ikiwa Wana utajiri wa Mali au masomo.bado Wana tamaa ya kuenda ng’ambo. Utawapata wanauza Mali Yao yote na kuhamia ng’ambo.ndoto Yao pia ni kuwa watoto wao wasomee ulaya. Juhudi zao zote huwafanya kupanda ndege na kusafiri ili waanze maisha mapya.
Afya ya binadamu ni muhimu zaidi . Bila afya maisha yetu huwa na matatizo mengi. Umri wetu unapozidi na tunapozeeka, Kuna baadhi ya magonjwa kama saratani au kisukari huathiri miili yetu.sababu za watu kuhamia mataifa ya nje ni kupata matibabu Bora . Nchi za ng’ambo Huwa na matibabu Bora lakini yenye Bei ghali .
Kuna haja kutafakari kuhusu ushuru wa juu nchini kenya . Wanabiashara wanapitia maisha magumu sana . ” mbona tuongeze ushuru? Wakenya wengi wanajiuliza maswali mengi akilini. Waekezaji pia wanashangaa na hatimaye kufanya kampuni zao. Wale walioathiriki ni wakenya kwasababu watakosa ajiri.kutokana na ushuru wa juu ni sababu tosha watu kuhamia mataifa ya nje. Lengo kuu ni kuanzisha biashara zao huko.
Mchezo ni muhimu kwa mwili ya binadamu. Kuna aina mbalimabali ya michezo kwa mfano mbio, voliboli kandanda na hata mpira wa kikapu . Ni jambo la kushangaza kuwa baada ya wanariadha kushinda na kutetea nchi Yao sifa . Wengi wao hulipwa pesa kidogo sana. Maisha Yao Huwa ya kutilia shaka. Itawabidi kuhamia mataifa ya nje ili walipwe vyema. Mfano Bora ni eliud kiprop ambaye ni mkenya lakini ,yeye hukimbilia nchi ya Uganda.
Ni matumaini yangu kuwa , Rais William Ruto ataboresha maisha ya wakenya, kwa kufufua uchumi, ili kuwavutia waekezaji zaidi nchini kenya. Anapofanya hivyo idadi ya wakenya kuhamia mataifa ya ng’ambo itapungua kabisa .