Pasaka ni Sherehe ya Kiyahudi iliyowakumbusha jinsi Mungu alivyowakomboa waisraeli kutoka utumwa wa Misri. Mungu aliwaagiza waisraeli wakumbuke tukio hilo muhumu kila mwaka.Pasaka husherehekewa na wakristo makanisa. Mungu aliwapa waisraeli maagizo ya jinsi ya kusherehekea pasaka yao ya kwanza.
Nchini Kenya wananchi walifurika makanisa ili kumshukuru Mola kwa kuwakomboa kutoka utumwa wa misri. Ni jambo la kushangaza mno, kwasababu madaktari wamegoma , kwa hivyo baadhi ya wakenya walisherehekea pasaka wakiwa wagonjwa huku wakikosa kupata hudumu hospitalini. Jumbe ambazo zilitolewa makanisa ilikuwa kumrai Rais William Ruto pamoja na waziri wa afya Susan Nahumicha kuangazia mgomo wa madaktari. Huku kiongozi wa kanisa la Catholic askofu Muheria akisikitishwa na mgomo wa madaktari.Wagonjwa wanazidi kuteseka.
Pasaka ni siku ya furaha kwasababu inawakilisha utimilifu wa unabii wa Agano la kale na ufunuoa wa mpango wawokovu wa Mungu kwa wanadamu wote. Neno pasaka limetokana na neno la kingereza ambalo ni “Passover au Easter” wakati huu serikali huwapatia likizo wafanyikazi kusherehekea siku hii muhimu zaidi. Wananchi wengi husafiri Kijijini ili waweze kusherehekea na jamii zao. Chakula kitamu hupikwa kwa wingi. Wale ambao Wana mapato ya kutosha hupeleka familia zao katika mbuga ya wanyama.
Hata hivyo sherehe ya pasaka ya mwaka huu , kulikuwa na mashindano ya Safari Rally kule Naivasha. Rais William Ruto alishabikia mashindano haya .Watu kutoka sehemu mbalimbali za nchi walifika Naivasha. Kwa kweli ilikuwa sherehe ya kukata na shoka. Yesu Kristo ni Pasaka wetu, yaani ni aina ya sadaka iitwayo pasaka kwetu ili Mungu aitumie damu yake kutusaidia.
Ni rahisi sana watu kusahau sherehe ya pasaka. Kama msisitizo wa wakristo, hii ndio maana tunasherehekea ulimwenguni pote. Mamillioni ya watu wasio wayahudi wanajua kwa kadri fulani kilichotukia kabla ya Pasaka. Huenda walisoma bibilia na kuona sinema inayohusu pasaka.
Pasaka ndicho kilele Cha mwaka wa wakristo kwasababu waamini wa dini huadhimisha ukombozi wao.Ukombozi wa wakristo ni kifo na ufufuo wa mwokozi na Mungu yaani Yesu Kristo toka mwanzo baada ya kujitayarisha kwa siku arobaini za mifungo.(yaani kwaresma) wakristo husherehekea kanisani. Ijumaa na pasaka. Wakristo wanafahamu kuwa Pasaka ni jinsi walivyotoa sadaka ya mwana kondoo na kupaka damu yake mlangoni mwao.
Katika pasaka, Juma la mwisho ambalo huwa Juma takatifu, wakristo huanza sherehe ya matawi. Hapa wakristo huitwa Jumapili ya matawi. Bwana yesu alipoingia kwa shangwe Yerusalemu. Watu walimpokea kwa shangwe wakitandaza mavazi yao na kupeperusha matawi ya mizeituni. Umuhimu wa pasaka kwa wakristo ni kumbukumbu kubwa ya kristo aliyefariki. Wakristo walishinda mapigo mengi na kuhudumu hadi leo katika Imani.
Alhamisi kuu ni muhimu pia kwani wakristo waliadhimisha siku alipoweka daraja na sakramenti ya upadri. Siku hiyo mapadri hurudia ahadi zao za ukuhani.Vilevile huadhimishwa alipoweka sakramenti ya ekaristia takatifu, mwili na damu yake.
Shughuli nyingi hufanyika wakati wa Alhamisi kuu. Mapadri katika kanisa katholiki huosha miguu ya waamini wao kumi na wawili. Je, mbona wakristo walioshwa miguu siku ya Alhamisi kuu,Siri ni kuonyesha upendo na unyenyekevu kila mara, ijuma huwa siku ya kumwabudu kristo aliyesulubiwa msalabani. Wakati huu wa pasaka, serikali imekumbwa na matatizo ya mafuriko mjini Nairobi. Afisa wa polisi David Cheshire alisombwa na maji. Isitoshe katika wizara ya kilimo kulikuwa na sakata ya mbolea ghushi, mambo haya yote huhitaji maombi.
Watu wote hata wale wasioamini, wakati huu wa pasaka ni bora kuiombea serikali, wagonjwa, wenye shida na waamini wote. Katika pasaka Mungu aliwapa agizo wakristo kumbukumbu ya kila mwaka katika vizazi vyao vyote.
Ukumbusho wa Kristo ni tukio la pekee sana kwa mashindano wa Yehova. Mambo ambayo bibilia inasema kuhusu tukio hilo, mwaka wa kanisa ni kama vile majilio, krimasi, Epifania, kipindi Cha kawaida, kwaresima na ijumaa kuu. Mambo haya yote ni husherehekea katika kanisa takatifu la katholiki.
Tuhahutaji kujua pasaka ya wayahudi na jinsi inavyohusiana na amri fulani waliyopewa wakristo wote. Pasaka ilikuwa sherehe rasmi yaani sikukuu.Kuna maswali mengi kuhusu pasaka na mlo wa jioni wa bwana baada tu ya pasaka. Pasaka ilisherehekekewa kwa kutaja mambo yafuatayo, dhabihu, chakula, sherehe, elimu, safari na desturi nyinginezo. Waisraeli walihesabu siku kuanzia jua lilipotua hadi jua lilipozama siku iliyofuata. Kisha walimchinja mwanakondoo dume huyo na kumla. Ni vyema kutafakari kuhusu maisha ya Kristo, Kisha kubadilisha moyo na tabia zetu kwa jumla. Vile kristo alijitolea tunafaa kuiga mfano wake msalabani. Ingawa si jambo rahisi lakini ni Vyema kujikaza. Dini haina mipaka bali usafi wa moyo, tuwaombe madaktari wasitishe mgomo wao.