3.1 C
London
Wednesday, January 22, 2025
HomeLifestyleArt & CultureTamasha Ya Muziki.

Tamasha Ya Muziki.

Date:

Related stories

Why Emotional Literacy Matters for Children

Building a Strong Foundation: Why Emotional Literacy is Essential...

Mind Management, not Time Management.

The Illusion of More Time: Why Mind Management Trumps...

Behaviour Management in Children

Understanding and Guiding Children's Behaviour: A Practical Approach Raising children...

What’s New in the Latest ChatGPT: Enhanced Features and Capabilities

The latest version of ChatGPT, powered by GPT-4, has...

The Silent Revolution: How Tech Schools Are Transforming Lives in Nairobi’s Slums

In the heart of Nairobi’s bustling informal settlements, a...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Wakuza mitaala wa humu nchini wamejadili vilivyo jinsi ya kuboresha elimu .Ndipo wakasisitiza mageuzi , bali na mitaala ya kawaida,kuwe ma mitaala shiriki. Baadhi ya mafunzo yaliyoorodheshwa kwenye elimu shirikishi ni kama kwata, muziki, uchoraji na kuigiza .Wizara ya elimu ilipendekeza vilivyo kuwe na mashindano yasiyohusiana na masomo haya.Katika kaunti ya Mombasa sanaa ya uchoraji imekita mzizi wasichana wanafunzi wamefundishwa kuchora wakitumia henna wakati wa sherehe za ramadhani, Sanaa hii inatumika kama kitega uchumi. Ili kuvutia zaidi lazima kina dada wachore mitindo mbalimbali

Ujio wa “C.B.C ” almaarufu elimu ya umilisi hukuza talanta hii kwa mapana na marefu .Waziri wa elimu mheshimiwa Ezekiel Machogu amepiga jeki Sanaa hii. Kuna baadhi ya waigizaji nchini kenya kama vile Erick Omondi.Ni wazi kuwa kuigiza imekuza Talanta za vijananchini..Waigizaji husisimua hadhira kwa kutoa mafunzo , pia nia njia moja ya kuburudisha watu ikiwa Wana uchovu kupita kiasi.
Ukitembeleea angatua ya Jomokenyatta almaarufu ” air port ” . Utawapata wanamuziki wakicheza ngoma.Wanariadha walioshinda kama vile Faith Kipyegon, Lilian Obiri, wakati wanarudi nchini, wanamuziki hawa huwachezea Ngoma wakiwakaribisha kwa shangwe na nderemo. Ni bora kufahamu kuwa Muziki unahitaji ala za muziki. Watu wa Afrika mashariki hutumia ala za muziki ambazo zinafanana sana. Kuna ala za nyuzi kama vile Gita, zeze, kimbi na udi Piano pia ni aina ya nyuzi ingawa nyuzi zake zimefichika ndani.
Piano hutumika kanisani, shuleni ili kutumbuiza hadhira.Hadhira ni watu ambao husikiliza muziki kwa makini. Ala nyingine hutoa sauti kwa kupulizwa upepo.Ala hizi ni kama vile kipenga ambacho pia hutumiwa na refa.

Katika mashindano lazima refa awe mwangalifu. Mashindano ya kandanda huwa ya kutumia nguvu zaidi.Waziri wa michezo mheshimiwa Ababu Namwamba ametia bidii katika masuala ya Talanta hela. Wachezaji kutoka kaunti arobaini na saba wameshiriki katika mashindano ya chapa Dimba, mashindano haya hufadhiliwa na “Safaricom,” kote nchini.

Ngoma na muziki ni njia ni njia moja ya watu kujipatia ajira. Hoteli nyingi huajiri wanamuziki na wachezaji Ngoma, ili kuvutia wateja katika hoteli hizo. Kuna Ngoma ambazo huchezwa uwanjani na huangaliwa na watu wote. Ngoma hizi ni kama zile za kusherehekea mavuna au sikukuu za Taifa au kumbuuiza wageni mashuhuri. Ala zingine za muziki hutoa sauti kwa kutikiswa , kwa mfano ala hizi ni kama njuga,kayamba, tari na manyanga.

Muziki hutoka pembe zote za nchi. Ama kwa hakika utamaduni wa Taifa hii unaendelezwa.Magharibi wanajulikana vilivyo kwa Ngoma ya isikuti, nao wenzao kutoka nyanza walionyesha ubabe wao wa kusakata Orutu.
Bonde la ufa nao hawakuachwa nyuma, bali hucheza kimenge’nge ‘ kisawasawa. Kaunti ya Mombasa hujulikana zaidi kwa kutumia chapua na zumari.Matumizi ya kipenga na njuga yalidhihirika miongoni mwa washirika.Nao wale wa kutoka eneo la kaskazini mashariki hujikakamua kwa parapanda na msondo.

Katika tamasha ya muziki vyakula vya kienyeji huandaliwa. Katika jamii ya kalenjin huwezi ” Mursik”. Nayo jamii kutoka mlima Kenya hushabikia “mokimo” tamasha ya muziki huwa na vifigo na nderemo. Waimbaji huvalia mavazi inayoitwa makeba .Maleba huvaliwa ili kusisimua hadhira iliyoko jukwani. Ni vyema kuwahusisha vijana katika tamasha ya muziki, tukifanya hivyo bila shaka watakuza vipaji vyao maishani. Dunia ni kubwa sana ,Kuna mahali pengi ambapo watu wangependa kufika lakini hawawezi, aidha hawajui mahali penyewe palipo au hawana pesa ambazo zinaweza kuwakifikisha huko.

Mwanafunzi akizamia muziki kama sanaa hitajika, ataweza kufika mbali maishani.Mwanamuziki. Kelvin Bahati ametambulika kupitia muziki wake. Faida nyingine inayopatikana kwa muziki ni utangamano na wengine. Katika shule za msingi chama Cha kuungana, kufanya, kusaidia kenya kimethibitisha ukweli huu. Ili kufanikiwa katika jambo fulani maishani ni bora kuungana.
Kama vile waswahili husema umoja ni nguvu , utengano ni udhaifu.Kuna baadhi ya wanamuziki ambao hufanya kazi kwa pamoja, almaarufu “collabo” mfano bora ni “msanii music group” wao huimba kwa vikundi mbalimbali.

Isitoshe shuleni hufuzwa kujitegemea,ikiwa umemaliza shule na hukufanikiwa kupata pesa.Unaweza kujitegemea mwenyewe.Vitu ambayo watu hufuzwa ili kujipatia riziki ni kama muziki , kushona nguo na kutengeneza vitu kama kama meza,kwa hivyo lazima vijana watia bidii katika masomo.na vile vile nje ya darasa. Wakati wa tamasha za muziki,watu hufurika ili kujionea utamaduni mbalimbali.Mila na desturi hutusaidia kujifunza mambo uzalendo wetu .

Hata hivyo mwacha Mila ni mtumwa.Watoto wadogo hufunzwa mambo mengi kwa kukariri kuiga, kuiga na kufuatikia hadithi kwa picha miongoni mwa mbinu nyingine ili kufanikiwa katika kuwaandikia , sharti mikakati hiyo ya utunzaji izingatiwe. Vijana wanalia hawana kazi , lakini hawajagundua kuwa muziki hulipa.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img