Asali unafahamika kwa muda mrefu kama chakula muhimu ambacho husaidia kupambana na magonjwa mbalimbali. Asali imehusishwa na manufaa ya kiafya kama vile uponyaji wa jeraha , afya ya moyo.Ni bora kutumia asali ili kuchukua nafasi ya aina nyingine za sukari.Asali huhifadhiwa katika sega la asali ili kutoa chakula kwa nyuki.Ni bora kufahamu kuwa asali hutengenezwa na nyuki.
Nyuki hutoa huduma ya uchavushaji kwa mamilioni ya mazao , huboresha uendelevu na bioanuwai.
Angalau thuluthi moja ya chakula cha binadamu hutoka kwa mazao na mimea. Nyuki huishi kwenye mzinga . Vilevile asali ilitumika kama Kinga ya kuzuia uvimbe unaosababishwa na viini vya bakteria,ili kuharakisha mchakato wa kupona na majeraha madogo na vidonda vya tumbo na vya kuugua , asali mbichi ambayo haijachemshwa , kuachachishwa au kuchunjwa huwa ina virutubisho, kuliko Ile inayochakatwa kwa mara nyingi hupoteza virutubisho vingi katika mchakato huo wa kuvunwa .
Kila asali imetengenezwa na aina mbili ya sukari kama vile glucose na fructose.Ambazo kila mara huvuta maji kwenye kidonda na kuzuia kukua kwa bakteria na utando.Binadamu hutumia asali kama chakula, dawa na katika kiwanda cha tumbaku huhifadhi harufu na unyevu, katika vipodozi kama matibabu huhifadhi maji na kulainisha ngozi vyema.
Chavua hutumika kama chakula, dawa na vipodozi. Lishe katika asali inapokuwa mbichi , asili huwa na amino acid. Asali hutengenezwa na nyuki.Hali hii hutokana na mkusanyiko wa vimiminika vyenye sukari nyingi itakayo kwenye mimea.Huhifadhiwa katika sega ili kutoa chakula kwa nyuki.
Ufugaji Wa Nyuki ni shughuli muhimu ya kilimo yenye utamaduni wa muda mrefu .Nyuki hutoa sumu wanapouma kama njia ya kujilinda .Sumu ya nyuki hutumiwa kama dawa mzio unaosababishwa na kuumwa kwa nyuki.
Ufugaji wa nyuki ni kazi inayoleta mapato ikiwemo rasilimali ya misitu,hata hivyo sio anayepata kipato kutoka kwa ufugaji wa nyuki. Bila shaka nyuki anaweza kuwa mtetezi wa uhifadhi wa rasilimali ya misitu.Nyuki Wana madhara kwa binadamu kama vile wanaweza kukushambulia kwa ghafla.
Mazao kutoka kwa ufugaji kwa nyuki ni mengi kama vile asali ya nta, chavua, propolisi , jeli , sumu na malkia .Propolisi ni mchangangiko wa nta ya nyuki anayetengeneza asali kutoka kwa mimea haswa maua. Propolisi hutumiwa kutengeneza vipodozi dawa na katika teknolojia ya vyakula.Mzinga yenye fremu (mizinga ya ghorofa) hutumiwa kufuga nyuki .Hii hutumiwa kuzalisha asali maradufu kila misimu na kupunguza usumbufu kwa koloni ya nyuki .
Nyuki wengi huwekwa katika mzinga.Wakati wa msimu wa maua hifadhi ya asali huwa kwa haraka zaidi. Mizinga ya kitamaduni ni Ile ambayo imetengenezwa nchini kwa kutumia vitu tofauti, magogo yenye shimo kwa Sehemu ya ndani ama chungu, lakini unapotoa asali , nta nyuki wengine huuwa .Vifaa vingi vya vifaa vinavyohitajika kwa ufugaji mdogo wa Nyuki.Vinaweza kutengenezwa na mafundi vijijini.
Zaidi ya haya, watoto wote wenye chini ya miezi kumi na mbili hawapaswi kula asali mbichi, hii inaweza kusababisha sumu ya chakula ndani yao inayoitwa botulism.Kuna mifumo mkuu mitatu inayotumika katika uzalishaji na masoko ya mazao ya nyuki.Ni bora kufahamu kuwa wafugaji nyuki wengine hufanya kazi , peke yake bila kupata msaada wa vitendeakazi na namna ya kufikisha mazao kwenye masoko.
Wafugaji wa nyuki hujiunga katika vikundi pamoja na vyama vya ushirika. Vyama hivi hutoa misaada mingi ikiwa ni pamoja na usafiri na vifaa vya kuhifadhi mazao ya nyuki. Kuna waekezaji wakubwa wa kibinafsi huwapa wafugaji nyuki huduma zote, ambazo wanazohitaji ili wazalisha asali yenye kiwango cha juu .Asali ya nyuki wadogo Ina faida nyingi mwilini, husaidia kutibu maradhi mwilini , husaidia kutibu maradhi kama vile ukosefu wa nguvu za kiume na vidonda vya tumbo. Asali huvunwa mwisho wa msimu wa maua .
Mfugaji wa nyuki huchagua masega yenye asali iliyokomaa.Hifadhi ya asali huwa kwa haraka wakati wa misimu wa maua . Ufugaji wa Nyuki ni bora zaidi, kwasababu imeleta utangamano.
Wakulima wengi katika jamii wamepewa mafunzo kufanya kazi kwa pamoja. Faida za afya hutegemea jinsi ilivyochakatwa pamoja na ubora wa maua ilipokusanywa . Ufugaji wa Nyuki ni kilimo bora hata hivyo huwa changamoto chungu nzima.Kama vile ukosefu wa ujuzi i na jinsi ya kupata vifaa na mbinu bora ya kutunza nyuki. Pia mazao ya Nyuki ni duni kutoka kwa wafugaji wengi.
Isitoshe hakuna utaratibu dhabiti wa ukaguzi wa ubora wa mazao. Wafugaji wa nyuki hukosa taarifa za masoko ya ndani na nje ya nchi. Ili kupata mazao zaidi mfugaji wa nyuki ni vyema kuhakikisha kuwa wadudu wanaharibifu kama vile sisimizi, mende na wengineo wanadhibitiwa ili wasiathiri uzalishaji wa asali. Hakikisha unavuna kitaaalumu ili kuepuka upotevu wa asali, ikiwa nyuki watatunzwa vizuri na kwenye mazingira mazuri unaweza kuvuna asali mara tatu kwa mwaka.