4.3 C
London
Wednesday, January 22, 2025
HomeCommunityUMUHIMU WA DINI KATIKA JAMII

UMUHIMU WA DINI KATIKA JAMII

Date:

Related stories

Why Emotional Literacy Matters for Children

Building a Strong Foundation: Why Emotional Literacy is Essential...

Mind Management, not Time Management.

The Illusion of More Time: Why Mind Management Trumps...

Behaviour Management in Children

Understanding and Guiding Children's Behaviour: A Practical Approach Raising children...

What’s New in the Latest ChatGPT: Enhanced Features and Capabilities

The latest version of ChatGPT, powered by GPT-4, has...

The Silent Revolution: How Tech Schools Are Transforming Lives in Nairobi’s Slums

In the heart of Nairobi’s bustling informal settlements, a...
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes


Dini ni Imani inayohusiana na mambo ya kiroho kwamba Kuna muumba ambaye aliumba ulimwengu, huu na kwamba ndiye mtawala . Dini pia ni mfumo Fulani wa Imani hii na njia ya kuabudu ,kusali au kuheshimu na kutii muumba. Dini Ina majukumu ya kuweka uadhilifu wa rasilimali katika jamii , kuzigawa haki za jamii. Dini isiyo ya kueneza afyuni , kwa hivyo huleta uhusiano katika jamii mbalimbali. Dini Ina majukumu ya kuwaongoza wanadamu katika neema , kwa hivyo ikiwa watu watajitetea kutokana na hatari . Dini na miundo inayohusiana kijamii na kitamaduni imekuwa na sehemu muhimu katika historia ya mwanadamu.

Kama miundo ya kiakili , huathiri jinsi tunavyoona ulimwengu . Unaotuzunguka na maadili tunayokubali au kukataa. Hata hivyo Huwa na hasara chungu nzima. Baadhi ya mafundisho ya dini ni hatari kwa jamii kama, ndoa za utotoni , kafara za wanyama wa mkumbuke Abraham kuchinja .watu wasiofuata dini ili kujipatia thawabu. Pamoja na kusababisha kelele mtaani nyakati za ibada .
Dini inadhohofisha uwezo wa watu kiutendaji kwa kuumanisha kuwa yupo mungu atakayetenda kila jambo . Matokeo watu wanakimbia majukumu Yao na kumwachia huyu asiyethibitika kama yupo. Dini Ina mafundisho yenye utata na ukiuliza maswali unapewa ” mixer” ya vitisho , jukumu na majibu yasiyo ya kweli Yaani ” fake”.

Dini inatengeneza matabaka kwenye jamii kwa kuamini kwamba Kuna watu watakatifu waliopewa mamlaka na mungu ya” kudominate” watu wengine ilihali watu wote ni sawa. Pia mwanamke amewekwa kwenye daraja la chini katika dini. Kwa mara nyingi kuna baadhi ya makanisa ambazo haziruhusu wanawake kuhubiri kwenye madhabau. Dini haichochei maendeleo ya kiakili ya watu . Ni kawaida ya kutokuwa na maswali mengi au la nchini mwetu. Hii ni baaada ya janga la vifo kutokea . Watu walijiuliza Maswali baada ya mahubiri au mawaidha.

Matokeo yake wafuasi wengi wa dini wamekuwa na uelewa mdogo wa kiakili. Dini inawanyonya wanyonge hasa pale watu wachache wanadai fedha kutoka kwa wanyonge kwa kigezo Cha kwamba ni sadaka au mchango .
Dini Ina madhara ya kuongezeka kwa umaskini wanapopoteza muda na fedha zao bure ili hali wachache wakinufaika na jasho lao. Umewahi kumwona Mungu petroli station au kwenye duka la jumla au “supermarket”. Dini husababisha mafarakano kwenye jamii. Jamii Ina dini nyingi na makanisa kadhaa ambapo kila mtu anaamini kuwa yeye ni sawa zaidi , matokeo yake ni vita , ugomvi , mapambano na mauaji. Dini inaharibu tamaduni za watu , kwa mfano tamaduni za kiafrika zimeharibiwa na dini na kuleta matokea kadha , waafrika wameiga tamaduni za kigeni kama mavazi ,majina na hata pamoja na chakula kwa jumla .

Dini zinaagiza watu wasiishi watakavyo Bali wafuate Sheria za dini kadha ili kuandaa Maisha ya peponi ,mbona hatukujiandalia masiha haya duniani kabla kuzaliwa? Dini Huwapa watu vitisho kama vile kuenda motoni siku ya kiama kwa kutenda mabaya , lakini dini hizi hazitoi ushahidi kuwa kama jehanamu Ipo.
Ni jambo la kusikitisha mno kule kilifi ,dini ilisababisha vifo vingi mno. Katika kanisa la mhubiri tata Paul Mackenzie iitwayo kwa majina almaarufu “ New life international” baadhi ya wakristo walipoteza maisha Yao bila kupata fahamu .Imani hii potovu iliwafanya kuuza Mali Yao, kuacha kazi zao mjini , kuuza mashamba pamoja na magari ya kifahari , hatimaye kushiriki maombi ya kufunga bila kula au kunywa maji , matokea yake ilikuwa ni vifo vingi mjini kilifi , hivi sasa wakenya wengi bado wanajiuliza maswali mengi vinywani mwao. Na bado hawajazika wapendwa wao.

Pia wakati wa mkesha wa mwaka, watu hukusanyika katika maombi Lengo lao ni kutarajia uponyaji , utafikiri ni siku za mwisho wa Dunia , ajabu ni kuwa wengi wao huaga badala ya kuponywa .katika kanisa la mhubiri nabii Owuor jambo hili hufanyika kila mwaka. Eti walemavu , vipofu na hata viziwi watasikia na kuponywa . Baada ya maombi kukamilika wao husalia vivyo hivyo . Dini imekuwa kigezo Cha uongo ili watu wajipatia sifa na pesa nyingi.
Masharti makali sana . Kila kanisa Ina kanuni zao. Dini imewachanganya sana wakristo . Katika dini zingine humu nchini , kwa mfano wakorino hufunga vitamba kichwani ambazo huitwa vilemba , katika kanisa la legio maria wao huvaa kanzu yenye rangi tofauti tofauti wakati wa maombi. Bila kufanya hivyo , hata huenda hutaombewa, kanisa la salvation army , mara nyingi wao huvaa Kama polisi, huku wakiwa na bandi maarufu, kila mara wao hupiga bendi. Si ajabu iwapo ni lazima kuvalia mavazi haya kabla kushiriki maombi, itawafanya wakristo wengine kukataa kwenda kanisani.

Si ajabu kusikia Kuna baadhi ya makasisi ambao hawana maadili . Mara nyingi utasikia mchungaji amebaka mwanafunzi au hata mjane . Maovu haya huleta aibu si tu kwenye kanisa Bali jamii nzima. Kwa mfano kule Nyandiwa , mchungaji wa kanisa la SDA bwana Shadrack Orony kuyu alipatikana na hatia ya ubakaji.
Ni Bora kujali masilahi ya watu unapojenga kanisa lako. Wananchi wengi wamelalamika kuhusu kelele za juu . Utafikiri kelele hizo ni maombi . Inakuwa vigumu kulala chumbani ikiwa maombi itaanza. Kelele hizi hufanya mtu kuchukia baadhi ya dini. Pia dini imefanya makasisi kupigania mamlaka , na hatimaye kusababisha vita kanisani. Heshima si utumwa , tusiwe watumwa wa dini Bali tupende dini zetu , kama tujuavyo dini ni Mali ya roho.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img