0.4 C
London
Thursday, November 21, 2024

Uzalendo

Date:

Related stories

Why Africa is Still Poor?

Africa, rich in natural resources and cultural diversity, paradoxically...

Kenya’s Journey Toward a Cashless Economy

Kenya has been at the forefront of the digital...

Mau Mau: Mukami Kimathi’s swansong to a city at war

By Jaclynn Ashly 72 years after the Declaration of Emergency...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Uzalendo ni hali ya kuipenda Nchi yako. Anayeipenda nchi yake huitwa mzalendo bali anayeichukia nchi yake huitwa msaliti. Msaliti ni adui ya maendeleo kila mara hutenda mambo mauvu. Je, ni nani anayependa nchi yake? Kuipenda nchi si kwa maneno tu bali kwa vitendo. Muhimu zaidi ni kuwapenda wananchi na kushiriki katika miradi ambayo inaweza kuboresha maisha ya wananchi au kuwafurahisha.

Ni lazima kama ibada kuonyesha uzalendo katika michezo, hapa mtu hujitolea mhanga katika shughuli zozote za kitaifa kama utahatarisha maisha yako. Seneta wa kaunti ya Busia ni mzalendo halisi, kwasababu anapigania haki za wananchi. Isitoshe amewasilisha kesi kadha mahakamani ikiwemo kupinga mswada wa nyumba ya bei nafuu.

Hebu tuangalia michezo. Wananchi wengi ni mashabiki wa timu za ulaya kama vile Manchester united, Arsenal, FC Arusha Tanzania. Utashanga na hata Wakati mwingine mashabiki wa timu pinzani hupigana. Huu si uzalendo hata kidogo. Ni bora kushabilkia timu zetu za kitaifa kama Harambee star’s, Harambee starlets, wakati mchezaji Dogo anafunga bao ni bora kumshangilia. Si ajabu kusikia kuwa mwanafunzi hawezi kukumbuka masomo darasani, lakini wanafahamu wachezaji wote wa timu hizo ilhali hata pengine, wengine wao hawatapata fursa ya kuonana nao maishani.

Unapotembea barabarani, utawapata wananchi wameva jezi iliyochorwa picha ya Ronald, Mesi na hata Neymar. Ni nadra sana kuona baadhi ya vijana wamevali jezi ya Oliech au Mariga. Je, uzalendo wetu uko wapi? Mashabiki wawa hawa waulize kuhusu timu za humu nchini utapingwa na butwaa. Hawana habari hata kidogo. Je, huo ni ulazendo? Furaha ya wachezaji ni kushinda mechi au muchuano uliyoandaliwa. Siku nyingi tumesikia timu yetu ya kitaifa Harambee star’s imekosa tikiti ya kusafiria. Je, wakenya hawana uwezo wa kufadhili timu yao? huu ni ukosefu wa uzalendo katika nchi yetu. Suluhisho ya matatizo yetu yote ni kuwa wazalendo halisi. Madaktari nchini wanegoma kwa zaidi ya siku ishirini na sita. Katibu mkuu wa madaktari bwana Davji Atela alijeruhiwa vibaya sana, Kisha akalazwa hospitalini. kisa hiki kulitokea wakati walipokuwa mjini Nairobi wakifanya maandamano ya amani.

Uzalendo si kuacha wagonjwa wanafariki kwa kukosa matibabu bali ni kuwasaidia ili kuokoa maisha. Kina mama wajawazito wanahangaika kote nchini wakitafuta huduma. Baada ya kupiga kura wananchi walikuwa na matumani chungu mzima baada ya uchaguzi. Sasa hivi mama mboga na baba mboga wamesahulika. Waziri wa afya Susan Nahumicha anadai kuwa serikali Haina pesa za kuwaongezea madaktari wanagenzi.
Hatimaye Rais William Ruto amevunja kimya chake na kusema kuwa serikali haina pesa. Taarifa hizi zimewavunja moyo madaktari. Tafakari ya babu, ni vyema wanafunzi kukosa Karo kwa nchi iliyo na wazalendo? Jibu ni kuwa uzalendo ulitupwa kwa kaburi la sahau.

Sote tutakapokuwa wazalendo kutaacha kufuga mbwa. Hatutajenga mlango wa chuma, hatutakuwa na silaha mkononi, mlango utakapobishwa kutafungua bila kuuliza ni nani? Polisi watakoma kuchukua hongo huku wananchi wakifariki kupitia ajali za barabarani. Tusipofikiria haya na kuwa wazalendo tutaishi jehanamu tuliko sasa. Askari wa “kanjo” au askari kaunti mjini Nairobi wapi uzalendo ukimwaga njugu ya mchuuzi barabarani. Hebu tuwe na utu heshima si utumwa. Kuokoa maisha ya mtu ni jambo la busara.
Afisa wa polisi David Cheshire ni mzalendo. Hii ni baada ya kuokoa wanawake wawili na mtoto mmoja, askari huyu alifariki akiwa shujaa, uzalendo ni mapenzi makubwa aliyo nayo mtu katika nchi yake.

Uzalendo ni nguzo muhimu sana ya taifa. Mzalendo hawezi kutoa siri ya nchi yake hadharani. Utaifa umejengwa kwenye hisia ya mapenzi kwa nchi na utambuzi wa kwamba rangi, cheo, eneo wanaishi kama jamii moja. Nchi moja huweza kuwa na watu wa makabila tofauti. Lakini wana nia na mawazo ainati, huku wakiheshimu Sheria za nchi.

Tamasha za muziki ni muhumu katika nchi. Ikiwa wewe ni mwanariadha, au mwanamuziki unaweza kupata fursa kutangamana na wasanii kutoka ughaibuni. Wakati mwanariadha anajenga shule, yeye hutambulika kuwa mzalendo halisi. Kwasababu shule itakuza elimu kama tujuavyo elimu ni ufunguo wa maisha. Mwanamuziki mashuhuri Akothee amefungua shule yake. Huu ni uzalendo wa hali ya juu, bingwa wa dunia Eliud kipchoge amepigania taji lake kwa muda zaidi na pia kujenga shule ili kusaidia wanafunzi wasiojiweza.

Wakati wa maandamano Erick Omondi alijitokeza kusaidia waathiriwa huku akiwalipia madeni yao. kujilimbikizia mali, pesa na utajiri kupita kiasi si uzalendo bali ni ubinafsi. Tukiwa na uzalendo basi nchi itakuwa na maendeleo kila wakati bila ubaguzi. Ni bora kila kiongozi kujiuliza amefanyia Nini nchi yake alipokuwa Uongozini.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img