26.3 C
London
Monday, June 24, 2024
HomeEducationMATATIZO YA LUGHA YA KISWAHILI

MATATIZO YA LUGHA YA KISWAHILI

Date:

Related stories

A Day of Collaboration: Youth Future Lab and Mojatu Women Meet with FIDA

On June 10th, representatives from Youth Future Lab (YFL)...

Youth Future Lab Attends Launch of Artisan Showroom Platform in Nyeri County

Youth Future Lab recently had the honour of attending...

Empowering Kenyan Women, How Female Entrepreneurs are Driving Economic and Social Change.

In the vibrant entrepreneurial landscape of Kenya, a remarkable...

Bridging the Divide, Kenyan Youth Transcend Ethnic Boundaries.

In a country as diverse as Kenya, where over...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Lugha ni chombo muhimu Cha mawasiliano . Kila jamii Ina lugha yake inayotumia katika shughuli zao za kila siku . Kwa mfano wa kupasha habari. Kuwasiliana ili kuelewana vyema. Changamoto ni Hali au jambo linalotia ari .lugha ya kiswahili Ina changamoto chungu mzima si shuleni tu bali kote nchini. Kwa mfano kasumba kuwa lugha ya kiswahili ni duni . Hii Ina maana kuwa wale ambao hutumia lugha ya kiswahili katika mawasiliano hawajasoma, watu wengi nchini kenya wanadharau lugha kiswahili sana. Wengi hupenda kuzungumza lugha ya kingereza Wanapofanya hivyo ni wazi kuwa lugha ya kiswahili inakosa umaaarufu kila mara.

Si kila mmoja anatumia lugha ya kiswahili huwa makini. Kama tujuavyo kila lugha Ina Sheria zake au kanuni zake. Lugha ni chombo Cha mawasiliano . Ni ajabu kuwa kiswahili hukosa kuwa mufti kila wakati. Wale ambao wanazunguma kiswahili hawazingati kanuni yaani ngeli. Nia Yao ni bora wamewasilisha ujembe. Hata hivyo jambo hili ni athari kwasababu malengo ya kiswahili haitatimia .
Kuvuruga kiswahili kwa kutumia “sheng ” mbona tuvuruge kiswahili, vijana wengi katika shule za upili hupenda kutumia lugha ya “sheng” . Wao huongeza maneno kama ” Ali pass away” “nilimsend’ ” Mimi nataka kusleep” matumizi ya maneno haya huathiri lugha ya kiswahili. Wanahabari wanafaa kuzingatia Sheria za kiswahili mufti , kama wasemavyo wahenga mwacha Mila ni mtumwa . Tusiwe watumwa wa kuiga lugha za kigeni na hatimaye kusahau lugha yetu rasmi .

Ni Hali ya kushangaza sana nchini kenya , kuwa uchapishaji wa magazeti hatilii manani kiswahili. Magazeti yote mawili ” standard newspaper” na ” Daily nation ” yote huandikwa kwa lugha ya kingereza. Jambo hili limedunisha kiswahili. Mara nyingi wasomaji wengi huchangamkia kingereza zaidi. Tatizo hili limefanya wanafunzi kuwa na shida katika kujibu maswali ya ufahamu . Hawajui kutafuta jawabu sahihi. Wao Wana uzembe wa kusoma taarifa kwa makini.
Katika shule za kibinafsi kiswahili hupigwa vita zaidi kuanzia Jumatatu hadi alhamisi . Hii inamaanisha kiswahili hutengewa siku ya ijuma pekee. Ukipatikana unazungumza kiswahili bila shaka unaadhibiwa. Jambo hili linawafanya wanafunzi kuishi kwa uoga. Hata walimu wa kiswahili hawana sauti . Ni Sheria duni sana ambayo imedunisha kiswahili na kulifanya kuchukiwa na wanafunzi. Wengi wao mara kwa mara hatimaye, husema kiswahili si somo la maana , hakina umuhimu kama kingereza.

Uhaba wa walimu wa kiswahili humu nchini imebainika kuwa walimu wa kiswahili ni wachache mno. Tatizo ni kuwa wengi wao hawapendi kiswahili hata hivyo , wengi wao husema kiswahili ni kigumu sana ” mbona kiswahili kina msamiati mingi sana ? Utawapata wakijiuliza maswali magumu . Ikiwa watafahamu ngeli katika kiswahili , basi kiswahili kitakuwa rahisi . Lugha Huwa rahisi ikiwa utazungumza , kusoma, kuandika na kusikiliza kwa makini.

Uhaba wa vitabu vya kiswahili. Unapotembelea maduka za kuuza vitabu , ni wazi kuwa vitabu vingi huchapishwa kwa lugha ya kingereza . Vitabu vya kiswahili ni haba mno. Wanafunzi wengi hupenda kusoma Hadithi za lugha ya kingereza . Ni bora wazazi kuwahimiza watoto wao kupenda kiswahili. Shuleni pia wanafunzi watunge shairi, nyimbo na Hadithi wakitumia lugha ya kiswahili . Huko bungeni kiswahili ilipoidhinishwa kama lugha rasmi. Hadi leo jambo hili limepuuzwa . Imekuwa vigumu pia kuwa na Baraza la kiswahili nchini kenya. Tukiwa na nia bila shaka kiswahili kitapata umaarufu zaidi nchini kenya.
Baadhi ya suluhisho kuhusu changamoto ya lugha ya kiswahili ni kama ifuatavyo
Wizara ya elimu kuajiri walimu wengi wa kiswahili. Ikiwa tunataka kiswahili kuwa maarufu zaidi . Ni lazima wizara ya elimu kuvalia njuga suala la kuongeza walimu wengi. Kuajiri walimu wengi kwa njia ya kandarasi si suluhisho. Ni bora walimu Hawa kuajiriwa moja kwa moja. Jambo la kuajiriwa baaada ya miaka mbili itawavunja moja walimu Hawa zaidi.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_img

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here