25.9 C
London
Monday, June 24, 2024
HomeCommunitySABABU YA AJALI BARABARANI

SABABU YA AJALI BARABARANI

Date:

Related stories

A Day of Collaboration: Youth Future Lab and Mojatu Women Meet with FIDA

On June 10th, representatives from Youth Future Lab (YFL)...

Youth Future Lab Attends Launch of Artisan Showroom Platform in Nyeri County

Youth Future Lab recently had the honour of attending...

Empowering Kenyan Women, How Female Entrepreneurs are Driving Economic and Social Change.

In the vibrant entrepreneurial landscape of Kenya, a remarkable...

Bridging the Divide, Kenyan Youth Transcend Ethnic Boundaries.

In a country as diverse as Kenya, where over...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Ukitembea mjini Nairobi . Utashangaa kwa Nini watu wengi wanafuraha.? Biashara imenoga kote mjini. Je, mbona magari yamejaa pomoni? Bila shaka jawabu ni kuwa sherehe za Christmasi zimeshika Kasi . Watu wengi wanaelekea mashambani kwa sherehe za Noeli. Si ajabu kusikia kando na sherehe Kuna ajali nyingi za barabarani zilizotokea.

Yafuatayo ni sababu kuu ya ajali barabarani . Hali ya hewa na chombo Cha usafiri. Hali ya mazingira inaweza kuwa chanzo Cha ajali . Mfano uwepo wa ukungu au upepo mkali. Wakati mwingine chombo chenyewe kinaweza kuwa sababu ya ajali . Mfano barabarani breki ya gari huweza kufeli au steering kungooka , au gurudumu kupasuka kwa bahati mbaya .

Matumizi ya vilewa. Kunywa pombe na kifurahia maisha ni jambo la kawaida na Wala si kosa. Lakini unapolewa kupita kiasi basi jambo hili hutambuliwa kuwa ni makosa . Zaidi ya hayo inaweza kusababisha vifo vingi. Pombe huondoa hofu na kupelekea mtu kufanya jambo lolote. Ni bora madereva kuepuka pombe wakati wanaendeshaji gari.

Vizuizi kwa dereva pia ni sababu ya ajali barabarani. Hutokea nje au ndani ya chombo. Kwa mfano wakati dereva anatumia simu wakati anaendesha gari. Sehemu kubwa ya mazungumza huhamia kwenye simu, hatimaye kusahau anaendesha gari. Jambo hili hatimaye husababisha ajali barabarani. Mwende wa Kasi . Magari ya mwendo mkubwa mara nyingi ndiyo ambayo hupata ajali na madhara yanayotokea Huwa makubwa kuliko ile ambayo ingewapata wale wanaoendesha kwa mwendo mdogo. Kadri mwendo wa gari inavyokuwa mkubwa vivyo hivyo hatari pia Huwa kubwa. Gari linaloendeshwa kwa mwendo mkubwa huhitaji umbali mrefu ili huweza kusimama yaani umbali wa kushika breki.

Gari linaloendeshwa kwa mwendo mdogo husimama haraka na kwa umbali mfupi wa breki. Kupuuza za taa , alama na michoro ya Barabara . Imekuwa ni mazoea siku hizi madereva kupuuza taa za barabarani na kukatiza bila kuzitilia maanani . Lengo la taa za barabarani ni kuongoza magari kusimama na kutoa mfano huo mbaya na mwishowe kupelekea ajali barabarani mara nyingi kwenye makutano ya Barabara upuuzaji wa taa za barabarani husababisha msongamano wa magari na foleni isiyoyalazima.

Kutofunga mkanda wa usalama na kutovaa kofia ngumu. Ni kwa matakwa ya Sheria kuwa ni sharti kufunga mkanda wa usalama na kuvaa kofia husaidia kupunguza majeraha na hata vile maafa makubwa endapo ajali itatokea. Mtu akivaa kofia na kufunga mkanda wa usalama ana nafasi ya kunusurika na maumivu na maafa ukilinganisha na yule ambaye hajafunga mkanda au kuvalia kofia ngumu.

Kubeba mizigo unayozidi uwezo wa chombo . Hiki ni kitendo Cha magari kubeba mzigo unayozidi uwezo wa chombo. Inafahamika kuwa gari Ina kiasi maalum Cha uwezo wake wa kubeba mizigo. Mabasi ya kibinafsi yanakuwa na kiwango maalum Cha idadi kupelekea ajali kutokea.

Kwa mfano kitendo Cha bodaboda kubeba idadi ya watu nne badala ya wawili inafaa kupigwa. Kubeba mzigo mkubwa kuliko uwezo wa gari hupelekea ajali kwasababu wakati mwingine dereva hushindwa kutawala chombo wakati wa Hali dharura huongeza ajali kutokea Barabarani .Ajali zinatokana na wamiliki kutozingatia Sheria na wamiliki kutozingatia Sheria kwa mfano wanajaza sana gari kupita kiasi. Na ufisadi kuuingizwa katika uendeshaji wa Barabara nzima. Hongo kwa wanausalama , unapata gari ikimbia sana na hawafanyi lolote.

Vyanzo vya ajali humu nchini ni kama Barabara ni mbovu na kuwa nyembamba sana , vile vile madereva wanaendesha gari bila kujali maisha ya watu ,na magari mabovu, ikijumuusha usimamizi mbaya pia watembea kwa mguu nao wanachangia ajali za barabarani.
Watu wengi hawana uzoefu wa kuendesha gari kwa mwendo mrefu ,mwisho wa siku wanachoka na kusababisha ajali lakini kingine ni watu kupuuza Sheria za usalama barabarani.

Kufuatia matukio ya ajali za barabarani kufululiza kwa siku hizi hivi karibuni ,magari yapige nyimbo za injili mwanzo hadi mwisho.ikiwa ni pamoja na kuweka mahubiri ya watumishi wa Mungu yaani wachungaji wanaohubiri injili ya kweli ya yesu kristo. Hapa tatizo la ajali barabarani litapungua kwa kiasi kikubwa kama siyo kukosa kabisa .
Katika kupambana na kidhibiti mwendokasi, serikali iweke mikakati katika kujenga miundo misingi wa Barabara zenye kupunguza mwendo wa Kasi kadri inavyofaa.

Pia endapo dereva akibainika kusababisha anyanganywe leseni na asipewe Tena kutokana na ukubwa wa tatizo baada ya trafiki kutambua. Wadau mbalimbali wanafaa kutoa elimu kwa watumiaji wa Barabara . Katika kuziwezesha kukabiliana na tatizo la ajali barabarani. Ni bora kutahadhari kabla ya hatari.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_img

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here