25.9 C
London
Monday, June 24, 2024
HomeInternationalKENYAUKOSEFU WA USALAMA KATIKA KAUNTI

UKOSEFU WA USALAMA KATIKA KAUNTI

Date:

Related stories

A Day of Collaboration: Youth Future Lab and Mojatu Women Meet with FIDA

On June 10th, representatives from Youth Future Lab (YFL)...

Youth Future Lab Attends Launch of Artisan Showroom Platform in Nyeri County

Youth Future Lab recently had the honour of attending...

Empowering Kenyan Women, How Female Entrepreneurs are Driving Economic and Social Change.

In the vibrant entrepreneurial landscape of Kenya, a remarkable...

Bridging the Divide, Kenyan Youth Transcend Ethnic Boundaries.

In a country as diverse as Kenya, where over...
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes

Ukosefu wa usalama ni nini? Ni vyema wananchi kuishi kwa amani si vita vya kila siku au wakati. Ukosefu wa usalama ni Hali ya kukosa ulinzi , hatari , si salama na hatimaye huchangia mauaji nchini. Watu wakikosa usalama huenda hujilaumu na kunyoshea mkono serikali kuu.

Katika shule ya upili ya wajir , wanafunzi wa kidato Cha tatu walifanya mtihani , lakini sehemu kubwa ya muhula masomo ilikosekana .kwasababu ya utovu wa usalama . Walimu wametoroka maeneo hiyo wakidai wenzao waliuwawa kwa msingi wa kidini . Lakini shida hii bado inaendelea kwa muda.
Vita vya kikabila . Ni jambo la kushangaza mno kuwa bado wananchi wanaishi kwa hofu. Kule migori na Transmara . Kumetokea vita vya kikabila pande zote mbili wanazozana kuhusu mipaka . Baadhi ya vijana wamepata majeraha ya mikuki . Waathiriwa wamepelekwa hospitalini ili kupata huduma ya kwanza , kwasababu ya majeraha ya mikuki.

Ukosefu wa usalama bado inaendelea kushuhudiwa maeneo ya kerio valley watu nane wamepoteza maisha Yao na mifugo kuibwa majuma matatu , baada ya waziri wa usalama nchini kithure kindiki kuzuru bonde Hilo na pia kuwarejesha kazini maafisa wa akiba . Ni Bora kufahamu kuwa Gavana wa kaunti ya elgeyo marakwet wesely Rotich alisema kuwa njia Bora ya kukabiliana na visa hivi ni kuwapokonya wakazi wanaomiliki silaha haramu katika eneo la bonde la kerio.

Ukosefu wa usalama kule Kaunti ya Lamu.Rais Ruto ametoa onyo Kali kwa wote wanaotoa semi za uchochezi kwa wakazi wa eneo hilo. Mgawanyiko kati yao Huwapa fursa magaidi kuendeleza ajenda zao za uharibifu. Utangamano ni muhimu katika jamii nzima. Serikali ya kenya Kwanza inajitoa mhanga kuhakikisha suala la ukosefu wa usalama katika kaunti ya lamu linatatuliwa kikamilifu kwa haraka .
Katika kaunti ya Narok wanakijiji wameshambuliana usiku kucha kutokana na wizi wa ng’ombe . Maafisa wa usalama kufika wamewatia mbaroni mwanamume ambaye anadaiwa kuhusika na wezi wa ng’ombe ambazo zimechangia mapigano haya.

Wanasiasa watatu wa eneo la bonde la ufa wamehojiwa na kitengo Cha upelelezi wa jinai huku Nakuru kufuatia mashambulizi na ghasia ya mashambulizi haya ni kati ya makabila mbalimbali na kusababisha utovu wa usalama.
Jamii mbili huko Samburu na Baringo wanaishi kwa hofu mno. Mbunge wa Tiaty William kamket na wenzake wa Sigor peter Lachakapong na seneta wa pokot magharibi Julius Mugor wamehojiwa kuhusu mashambulizi ya jamii mbalimbali.

Sekta ya majani chai imekosa ladha kadha. Wanasiasa na wafanyibiashara wanachochea ghasia na uharibifu wa Mali katika mashamba ya majani chai. Waziri wa usalamu bwana kithure kindiki amesema tayari serikali imepata majina ya wahisika . Pia amewahimiza viongozi wa samburu na Bomet wadumishe amani na kuacha uharibifu wa Mali za kampuni za majani chai . Ni Bora jamii kutangamana ili kudumisha amani kwa vile umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.

Usalama wa walimu wakuu imekuwa ya kutilia shaka mno . Pindi tu baada ya waziri wa elimu Ezekiel Machogu kutangaza matokeo ya mtihani wa kitaifa almaarufu ” KCSE” ilikuwa karaha badala ya Raha . Katika kaunti ya Uasingishu wazazi pamoja wa wanafunzi wakiandamana kwasababu ya matokeo duni .
Mwalimu mkuu wa shule ya mafuta alifurushwa kutoka ofisini . Wazazi wakibeba mabango huku wakionyesha gadhabu Yao. Haki hii ilifanya wizara ya elimu kuwahamisha walimu wote walioajiriwa na serikali.
Isitoshe hali hii ilitokea katika kaunti ya kakamega . Katika shule ya isongo , pia wazazi walikasirika kuhusu matokeo duni ya mitihani ya kitaifa. Mwalimu mkuu alifukuzwa huku akibebwa juu juu . Matokeo ya mtihani imekuwa chanzo Cha ukosefu wa usalama kwa walimu wakuu . Ni matumani yangu kuwa wazazi wangekumbatia majadiliano badala ya kufanya maandamano ili kupata suluhu.

Utovu wa usalama kwenye kaunti ya Busia ni kero .Hii ni baaada ya ofisi ya seneta wa Busia okia omtata kuharibiwa , vifaa vya kielekroniki vikaibwa katika uvamizi wa usiku. Wezi waliharibu na kuiba vifaa mbalimbali, mwendo wa saa mbili asubuhi Jumapili.

Ugomvi katika familia si Bora, wapenzi au wanandoa wanafaa kuishi maisha ya upendo , Huku wakitangamana . Ni ajabu mno katika kaunti ya kiambu visa vya mauaji vimekithiri . Hii ni baada ya Grace Wangari mwenye umri wa miaka ishirini na nne alifariki baada ya kuvuja damu nyingi. Mama huyo wa mtoto mmoja alidungwa kisu kichwani na bwana clinton mwangi kufuatia ugomvi.
Katika kaunti ya kiambu eneo bunge la lari , Stephen maina alikuwa mwalimu wa shule ya udereva . Ndoto ya kuboresha familia yake ilizimwa na wahalifu Hawa Kijijini. Aliuawa na watu wasiojulikana na mwili wake kutupwa karibu na mochari. Ni matumani yangu kuwa baada ya kufanya uchunguzi wa kina, haki itapatikana katika familia ya marehemu kwa haraka.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_img

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here