15.2 C
London
Thursday, May 2, 2024
HomeCommunityPOMBE HARAMU KIRINYAGA

POMBE HARAMU KIRINYAGA

Date:

Related stories

Henry Chakava (1946 – 2024): The publisher who pricked the people into consciousness

BY WALTER BGOYA Henry Chakava’s passing is, without a doubt, the...

Battling the Torrent: Flooding from Kenyatta University to Kahawa Sukari Area!

The regions encompassing Kenyatta University and extending towards Kahawa...

Supporting Reading ‘Windrush Generationers’ on Compensation Scheme

People who have had problems because they couldn't prove...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes


Pombe haramu ni pombe ambayo inazalishwa kinyume Cha Sheria nje ya michakato ya uzalishaji , iliyoidhinishwa na kudhibitiwa na watengenezaji waliosajiliwa . Kwa kiasi kikubwa Haina chapa na haizingati viwango vinavyohakikisha Ina usalama wa bidhaa. Ilikuwa ni majonzi na masikitiko kule kirinyaga wakati Gavana alihudhuria mazishi ya waathiriwa wa pombe haramu, walipokuwa wanazikwa .

Watu sita walifariki, na Tano waligeuka kuwa vipofu kwa wakati moja , idadi hii ikiendelea kuwa juu kila kucha. Waliofariki walidaiwa kunywa pombe haramu iliyokuwa na sumu ya ethanol ni Bora kufahamu kuwa afisa mkuu wa afya katika kaunti ya kirinyaga bwana George karoki alithibitisha kuwa pombe hiyo waathiriwa walibugia ilikuwa na maafa kwa haikuwa salama.
Mamlaka ya kirinyaga ilikashifu hujuma katika vita dhidi ya pombe haramu . Naibu wa rais bwana Gachagua amekuwa mbioni kuweka mikakati mbalimabali ili kuwahimiza wananchi kuwacha pombe na kujihusisha katika ujenzi wa Taifa yenye uzalendo.

Tusisahau kuwa BI wanjiku Teresia , ambaye ni kamishna wa kaunti ya mwea alikashifu hujuma dhidi ya pombe haramu Katika kaunti ya kirinyaga na viunga vyake.
Ni haki ya kila mwanadamu kutetea haki zake . Hiyo ndio sababu wenyeji walikasirika kupita kiasi wakachoma zizi Hilo ambazo pombe hiyo haramu ilikuwa imehifadhiwa . Pia wenyeji walikashifu polisi kwa kuzembea kazini na kila mara kwa kuchukua hongo , ilhali pombe haramu imesababisha vifo.
Ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa wanakiji wa Kijiji Cha kangai , eneo bunge la kirinyaga, wakati mmiliki wa baa alimakwati . Wanakijiji wanadai kuwa mmiliki wa baa hilo amefikishwa mahakama mara nyingi sana lakini anapotoa hongo, anawachiliwa . Pole kwa familia ambazo walipoteza wapendwa wao, mola awape nguvu.

Waathiriwa wa pombe haramu walifariki katika hospitali ya kerugoya . Watu kadha wanaendelea kupata matibabu , huku kundi la madaktari wakijitolea mhanga kunusuru wale ambao walikuwa katika Hali ya hatari. Hata hivyo ni Bora kufahamu kukamatwa na polisi mara kumi na Kisha baada ya muda Fulani akawachiliwa kuwa huru. ilihali mmiliki wa baa hilo alifahamika kuwa muuzaji sugu wa pombe katika kaunti ya kirinyaga.
Maumivu ya tumbo ilikuwa kero kuu, kwa wale ambao walikunywa pombe kwenye zizi. Inadaiwa kwamba walevi waliingia kwenye baa au danguru hiyo siku ya jumatatu wakipiga gumzo. Walikunywa pombe Kisha kuondoka kwa zamu, baada ya kunywa pombe kwa muda mrefu ubongo Huwa inakua kama kijana aliyebalehe kuwa katika hatari kubwa ya kudhurika na sumu ya pombe.

Soko haramu ya unywaji wa pombe , pia linajumlisha unywaji wa pombe bila kuzingatia Sheria. Kutokana na taarifa ya kuvunja moyo kwenye kaunti ya kirinyaga, naibu rais bwana Rigathi Gashagua amewaamuru wakuu wa usalama kurejea Nairobi.
Lengo kuu hapa ni kufanya uchunguzi ili kubaini kilichosababisha mauti ya watu ishirini na tatu kwa haraka mno. Waziri wa usalama bwana kithure kindiki pia ameteua jopo ili kufanya uchunguzi zaidi kuhusu vifo hivyo vya dharura .

Katika kaunti ya kirinyaga wanjeji waliharibu Mali ya baa hiyo. Chupa na meza zikiwa zimetapakaa .polisi walishangaa sana , walipata Mali nyingi ndani ya baa hiyo ikiwa imeteketea na kuwa majivu .
maumivu ya kichwa ni dalili ya kuonyesha kuwa pombe imewekwa sumu. Ukosefu wa ajira nchini kenya imechangia vijana wengi kunywa pombe haramu. Ni vyema serikali kuwapatia vijana kazi kwa haraka. Si vyema vijana kuaga Dunia kwa haraka sana. Dalili ya mvua ni mawingu , wananchi wanafaa kuchukua tahadhari kabla ya hatari.

Waziri wa michezo , utamaduni na huduma za kijamii wa kaunti ya kirinyaga bwana Dennis maciimi alisema bodi ya kupeana leseni ilipuuza ombi la baa hiyo mnamo Desemba mwaka wa elfu mbili ishirini na tatu. Baa hiyo ilishindwa kutimiza Sheria za kuuza pombe kwa wateja wao.
Pombe haramu inaweza kusababisha hatari kubwa kwa afya ya binadamu, Ugonjwa wa ini hutokana na pombe na hata pia kansa . Uharibifu kwa mfumo mkuu Neva . Inaaminika kuwa karibu asilimia hamsini na Tano ya pombe zote tunazotumia ulimwenguni ni haramu na kunywa pombe kunaweza kufanya mtu awe mgonjwa.

Pombe husababisha matatizo ya mapafu .baada ya watu sita kuiaga Dunia , daktari karoki alisema kuwa wagonjwa hao walipofikishwa hospitali walikuwa na dalili za kuona vimulimuli, ishara ya kumaanisha walikuwa na matatizo ya mapafu na mfumo wa Neva. Pombe imekuwa kero nchini kenya, ni Bora serikali kutangaza pombe haramu, kuwa janga la kitaifa.
Waathiriwa wote kumi na saba wa pombe haramu walizikwa tarehe kumi na saba Februari mwaka wa elfu mbili ishirini na nne kule kirinyaga. Mke wa naibu rais mama Dorcas Gachagua alihudhuria sherehe hiyo akiwa na huzuni chungu nzima .

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_img

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here