17.4 C
London
Saturday, June 15, 2024
HomeInternationalKENYAMADHARA YA KUTOTII SHERIA YA BARAZA

MADHARA YA KUTOTII SHERIA YA BARAZA

Date:

Related stories

spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes


Katika kaunti arobaini na saba nchini kenya . Kuna Sheria mbalimbali ambazo mwananchi anafaa kuzingatia ili maisha yake yawe ya kuvutia na kujivunia. Binadamu wa kawaida ana haki za kimsingi , pia watoto Wana haki zao katika jamii.kwa hivyo ni Bora kuheshimu haki za kila mmoja ili Sheria ifuatwe vyema ipasavyo katika jamii husika .

Kuna mambo ambayo yanaweza kusababisha mtu kufungwa jela nchini kenya kwa mujibu wa Sheria kwenye Baraza la mjini wa Nairobi. Kwa mfano ikiwa mwananchi atafanya uchafuzi wa mji au kutupa takataka ovyo ovyo kwa mujibu wa Sheria. Kukojoa mtaani bila shaka atachukuliwa hatua Kali za kisheria. Katika sehemu mbalimbali mtu akikula peremende si vyema kutupa takataka bila mpangilio.

Katika jumba mbalimbali ambazo zimepakwa rangi ya kupendeza, si vyema kukojoa ili kuharibu rangi hiyo , wakati unapotembea mjini utapata mabango yameaandikwa ili kutoa onyo Kali kwa wale ambao wanakiuka sheria.
Ukitembea mjini utapata mabango ya kukuelekeza mahali pa kutupa taka. kwa mfano utapata maandishi kama” usitupe takataka hapa” au ” usikojoe hapa “ukikiuka Sheria bila shaka utachukuliwa hatua Kali za kisheria .
Kuna Sheria ambazo huzingatiwa ili kuanzisha biashara mbalimbali mjini Nairobi. Mtu hawezi kuamka asubuhi na kuanza kujenga mahali popote bila kufuata Sheria husika , ni vyema kufungua biashara baaada ya kupata idhini pahali panaruhusiwa na Sheria za mji.

Bila kuwa na leseni biashara yako itakuwa katika hatari ya kufungwa. Hii ndio maana kila mama ambaye huuza nguo mjini Nairobi kule barabarani, hawana amani , kila mara wao hufukuzwa na askri wa mjini, almaarufu, ” kanjo”.
si ajabu kusikia kisa Cha mtoto aliyemwagiwa njugu zake chini, na”kanjo” Kisha kesi hii ikatatuliwa na Gavana wa Nairobi bwana Johnston sakaja.
Uchukuzi ni Hali ya kubeba abiria na mzigo kutoka sehemu moja hadi nyingine kule mjini Nairobi. Wasafiri wanaweza kutumia magari, pikipiki au hata garimoshi kama vyombo vya usafiri kuelekea sehemu mbalimbali za humu nchini ili kutimiza malengo Yao maalum.

Si Bora magari haya kufuata njia ya mkato. Wakati mwingi magari haya hukwepa kulipa ada , magari haya hayafai kupitia katika maeneo yasiyoruhusiwa huenda yakasababisha ajail, kwa vile ajali Haina Kinga.
Biashara haramu . Ni baadhi ya biashara ambazo haziruhusiwi kulingana na katiba ya nchi au Baraza la mji. Kwa uuzaji wa pombe haramu, baada ya kutoa onyo Kali kule kirinyaga, na Gavana Mheshimiwa Ann Waiguru, maafisa wa polisi walitiwa mbaroni walikunywa pombe haramu. Ilikuwa huzuni kupita kiasi watu kumi na saba walipozikwa kwasababu ya pombe, baa nyingi sasa zimefungwa kwa mujibu wa Sheria. Kila bidhaa kabla kuuzwa ni Bora iidhinishwe na shirika la ” kebs” ili iwe salama kwa binadamu.

Ujenzi wa nyumba bila idhini ya wataalamu wa gatuzi. Ni jambo la kuvunja moyo unaposikia majengo Yanaporomoko mjini Nairobi. Ikiwemo ghorofa ya hadhi ya juu kote mjini. Ni Bora kutafuta muhandisi aliyehitimu kabla kujenga nyumba ya kuishi au biashara yako. Majengo yakiporomoka wananchi wengi hupoteza Maisha.
Katika mji wa mkuu wa Nairobi , wakazi hawaruhusiwi kufuga mifugo kama ng’ ombe ,mbuzi, kondoo na hata punda. Wanyama Hawa wanaweza kugongwa na gari au kusababisha vifo, kwa kugonga watu kwa bahati mbaya . Kwa hivyo Sheria lazima ifuatwe kwa ukamilifu.
Uuzaji wa bidhaa ghushi. Bidhaa ambazo haziruhusiwi kuuzwa kwa mara nyingi si halali . Bidhaa hizi huenda zikasababisha madhara kwa afya ya binadamu.

Mamlaka ya ushuru ya kenya almaarufu “keb” ilifanya msako wa bidhaa za harumu. Hata hivyo ilinasa zaidi ya Vipande elfu ishirini na Tano ya stempu ghushi na chupa za maji ya kunywa. Bidhaa hizi zilipatikana katika kiwanda Cha kujaza maji katika eneo la viwanda , kaunti ya Nairobi. Jambo hili linadhihirisha kuwa bidhaa ghushi zimekuwa zikiuzwa katika maeneo ya bonde la ufa Huwa walengwa wakiwa wakulima wanaojiandaa kwa upanzi.
Ikiwa mwananchi atakiuka Sheria kwa kutofuata maagizo. Bila shaka Sheria itachukua mkondo wake. Kule kirinyaga , mhudumu wa baa alichukuliwa hatua Kali mno. Ingawa alikamwatwa mara kumi na mbili na kuachiliwa. Siku za mwizi ni arobaini. Hii ni baada Ya watu kumi na saba kuiaga Dunia.

Inadaiwa kuwa pombe hiyo ambayo wanakijiji walikunywa ilikuwa na kemikali ya ethanol ambayo ni hatari kwa binadamu ni wazi kuwa mhudumu wa baa hiyo alipokunywa leseni na kufunguliwa mashtaka. Pombe haramu ni kero katika eneo ya kati. Naibu rais RIgathi Gachagua anatia bidii ya mchwa ili kupunguza athari ya pombe.
Kufunguliwa mashtaka. Kule Embakasi kulitokea mlipuko wa gesi katika eneo la miradi . Mlipuko ya kemikali ile inayosababishwa na uchomaji wa mafuta . Waathiriwa wa mkasa wa embakasi wanasema waliona Lori ikivuja kwa muda wa saa moja .

Kisha likasabisha janga la mlipuko wa gesi na mathara . Mshukiwa wa mlipuko wa gesi apandishwa kizimbani ili kujibu mashtaka. Pia maafisa ambao walitoa lesini kwa huyu muhudumu watafunguliwa kesi kujibu mashtaka.
Magari kufungiwa kwa muda Fulani. Ni Bora dereva kuzingatia Sheria Bora za barabarani. Pia si kila gari huruhusiwa barabarani kuendesha . Ikiwa gari itasababisha ajali.
Kama vile kule Londiani dereva wa gari alisababisha vifo vingi mno. Watu wengi waliaga Dunia na kuvunjika viungo vya mwili. Dereva huyu alikamatwa na polisi Kisha gari lake kufungiwa kwa kituo Cha polisi . Poleni kwa familia walipoteza wapendwa .

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_img

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here