6.2 C
London
Saturday, April 27, 2024
HomeKENYAKenya EconomyBuriani Rita Tinina

Buriani Rita Tinina

Date:

Related stories

Tamasha Ya Muziki.

Wakuza mitaala wa humu nchini wamejadili vilivyo jinsi ya...

Kenyan Doctors Reject Government Offer, Strike Continues Over Internship Issue

In a recent development, the doctors' union in Kenya...

Delegates Convene for Talks on Plastic Pollution

Delegates during the official opening of the Third Session...

Government and Doctors Nearing Deal as Talks Extend to Tuesday

In an encouraging update, Head of Public Service Felix...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Mwanahabari ni mtu ambaye huwajulisha watu kuhusu matukio Fulani katika jamii . Kuna wanahabari wa studio na pia nyanjani,wote Hawa ni muhimu katika jamii kwa ujumla. Mwanahari anaweza kutayarisha habari kwenye chumba Cha habari. Kabla habari haijasomwa hewani Kuna yule ambaye huhariri habari hiyo bingwa huyo hujulikana kama mhariri ili kuondoa makosa habari hiyo, kila wakati.

Ilikuwa siku ya Jumapili tarehe kumi na saba machi biwi la simanzi ilitanda nchini kenya, hii ni baada ya mwanahabari mkongwe Rita Tinina kuaga Dunia . Alikuwa mwanahabari katika kituo cha “N.T.V.” kwa muda wa muongo mmoja . Ajabu ni kuwa Rita Tinina alipatikana amefariki nyumbani kwake, baada ya kula chakula Cha jioni .polisi walithibitisha kauli hii, na kusema alipoenda kulala hakuamka Tena.

Waandishi wa habari wamekuwa wakimiminika nyumba kwa mwendazake huku kileleshwa , na katika makafani ya “umash” baada ya kupokea taarifa kuhusu kifo Chake mwanadada huyu. Mwanahabari huyu mashuhuri alisifiwa kwa ukakamavu na ushupavu wake kwa kuchapa kazi na alikuwa mfano wa kupigwa kwa wengi katika tasnia ya habari nchini kenya.

Pindi tu habari kuhusu kifo Chake mwanadada huyu Rita Tinina kutangazwa . Wanahabari kadha wa kenya walimiminika mtandaoni huku wakitoa rambirambi zao kwa mapana na marefu.zubeida kananu koome aliajiriwa kama mfanyikazi wa kudumu na kuwa ripota wa shirika mashuhuri “K.T.N.” mwaka wa elfu mbili na saba , Kisha kupandishwa cheo mwaka wa elfu mbili kumi na mbili.zebeida alikiri kufanya kazi na Rita Tinina wakati wa kutoa taarifa kuhusu kesi za mahakama ya I.C C. Huko the Hague akiwa na Rita Tinina na waandishi wa habari wengine.Rita Tinina: Hakuna Majeraha ya Yaliyopatikana Kwenye Mwili wa Mwanahabari,  Ripoti ya Polisi Yasema - Tuko.co.ke

Frida mwaka mtangazaji wa kiswahili ambaye huanda kipindi Cha bunge la sato kila Jumamosi alisema kuwa walishiriki chapisho akikumbuka nyakati zake za mwisho akiwa na nyota huyu Rita Tinina.kweli ni wazi kuwa kifo hakina huruma.isitoshe tarehe kumi machi Jumapili walikuwa na mkutano na mwendazake Rita Tinina katika ofisi ya “nation media'”
Rita Tinina ambaye alitarajiwa kuwa kazini katika kituo Cha ‘N.T.V” hakuripoti .jambo hili liliwashangaza wengi mno huku wakimsubiri kazini. Kisha walipofanya utafiti wa kina, Rita Tinina alipatikana ameaga Dunia nyumbani kwake kule kileleshwa .pole kwa familia na jamaa pamoja na marafiki kwa jumla.

Marehemu Rita Tinina alikuwa na umri wa miaka arobaini na sita .amemwacha mtoto wake msichana mwenye umri wa miaka nane . Bwana Joe Ageyo aliwashangaza wengi na kusema kuwa maisha ni mafupi mno. Eti mtu anaweza kuwa hai leo lakini kesho anafariki dunia.

Polisi wanadai kuwa mwendazake alikuwa na malalamishi kuwa ni mgonjwa kwa muda wa siku Tano .mwili wake haukuwa na majeraha yoyote. Huenda alifariki kupitia Ugonjwa wa kifafa almaarufu ” epilepsy” kauli hii ilithibitishwa na dadake .Kisha familia iliomba utulivu wanapozidi kuomboleza na kuanda mazishi ya Rita Tinina.

zubeida mwanahabari wa K.TN.alilemewa na hisia huku akimsifia Rita Tinina kwa ujuzi wake kazini akiwa mananabari tajika na waliwahifanya kazi naye kwa miaka mingi sana.ni siku ya machozi kwa waandishi wa habari.

Baadhi ya wanahabari wa kituo Cha N.T.V. walimwomboleza marehemu wakiwemo Nina Shaban , Bernard Ndong , lofy matambu , frida mwaka .si rahisi kupoteza rafiki wa dhati.
Maisha ni kigeugeu .ni Bora kuwa na jina Bora maishani.mtindo wa uandishi na kuripoti bila shaka ulikuwa mojawapo ya nyakati Bora zaidi za wakati, wetu kama mwandishi wa habari wa masilahi ya binadamu.Rita Tinina angeelezea Hadithi nyingi kwa urahisi wa kitaaalum.N.T.V .

Itakosa bingwa huyu milele. Aliyekuwa waziri mkuu na kiongozi wa upinzani bwana Raila odinga kwenye taarifa zake alisema kuwa anakumbuka siku zake za kwanza akiwa N.T.V.alikuwa anajitolea sana kwa uandishi wa habari na kuliacha alama isiyoweza kufutika katika nyanja ya vyombo vya habari nchini kenya.

Mwanahabari huyu alianda taarifa kuhusu jamii ya” Yaku ” ambao walikuwa wanaishi katika kaunti ya Laikipia.rais William Ruto katika taarifa zake alimtaja marehemu kama mwandilifu na mtu aliyependa kazi yake kila wakati.waziri wa habari na teknolojia bwana Eliud Owalo pia alishangazwa na kifo Cha mwanahabari huyo.

Dadake Rita Tinina Hellen aliarifiwa kuhusu tukio Hilo na mmoja wa wfanyikazi wenzake . Dada huyo alipofika nyumbani kwa mwendazake, alijaribu kupiga simu za dharura lakini wahudumu wa afya walithibitisha kwamba tayari Rita Tinina alikuwa amefariki. Makazi ya Rita Tinina ilikuwa ” Brooklyn apartments” eneo la kileleshwa.ni jambo la kuvunja moyo kwa kumpoteza mwanahabari mashuhuri kwa Hali tatanishi. Bali na kusoma habari wanahabari huelimisha jamii kuhusu elimu , utamaduni, siasa na hata lishebora. Nawatakia marafiki na jamaa ya marehemu Rita Tinina nguvu na amani moyoni katika wakati huu mgumu wa majonzi.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_img

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here