15.8 C
London
Friday, May 17, 2024
HomeInternationalKENYAAthari Ya Plastiki Katika Mazingira.

Athari Ya Plastiki Katika Mazingira.

Date:

Related stories

Why women struggle to take climate cases to court and how to correct it

By Pedi Obani A study in Nigeria and South Africa...

Calling off UN regional climate weeks exposes rich nations’ lack of goodwill

Funding these essential meetings would cost little to rich...

Don’t gaslight Africa: We need genuinely clean cooking solutions

The IEA summit, where oil and gas execs are...

Kenya: Adding up the costs of the floods amid an economic crisis

The devastation from the floods in Kenya have been...

Can We Use ChatGPT for Global Goods Software Development?

At IntraHealth, where our mission is to support health workers...
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes

Unapotembea barabarani kila mara ni lazima utaona chupa za plastiki nyingi zimetupwa ovyovoyo. Chupa hizi hupatikana katika maeneo mbalimabali kama vile sokoni, kanisani, na barabarani. baada ya kunywa maji ili kukata kiu, utawapata wakenya wanatupa chupa hizi bila kujua athari yao katika mazingira. Kule pwani wavuvi wa baharini wanalia kuhusu athari ya chupa katika mazingira. Mazingira ni vitu ambavyo hutuzunguka kama vile milimani, mito maziwa na bahari.

Plastiki ni maunzi sintetiki ambayo haitokei katika mazingira ya kiasili. Inatengenezwa kwa kuunganisha molekuli nyingi ili kuwa nyororo na ndefu. Nchini kenya mifuko ya plastiki ilipigwa maarufu sokoni, yule ambaye anapatikana akitumia mifuko hizi bila shaka atachukuliwa hatua kali za kisheria. Jambo hili linawafanya wanabiashara kuwa na wasiwasi wakiwa sokoni.


Hata hivyo mifuko ya plastiki Ina madhara ifuatayo Katika mazingira. Miongoni mwa madhara ya plastiki kwenye mazingira ni kuchochea mazalia mbu waenezao malaria, hii ni kwasababu ardhi inakosa kuwa na rotuba. Ikiwa Kuna mafuriko mengi jambo hili husababisha malaria. Wakati chupa hizi zinatupwa haziozi na inaweza kusababisha saratani, endapo itafungiwa chakula Cha moto. Kule sokoni kina mama wanalilia serikali kubadilisha nia ya kupiga marufuku mifuko hizi za plastiki. Serikali ya Kaunti pia imetilia mkazo jambo hili ili kuhamasisha jamii.

Nchini Kenya wanabiashara hupenda kutumia mifuko ya plastiki kwasababu wanadai kuwa ni bei rahisi. Miongoni mwa madhara ya plastiki ni kwamba haziozi, jambo linalosababisha isambae maeneao mbalimbali na kuhatarisha maisha ya viumbe hai, maeno ambayo yanayoathiriwa ni uchafuzi wa plastiki ni baharini, ziwani na Nchi kavu. Ikiwa samaki amekutwa na chembechembe za plastiki halafu ukala huyo samaki utakuwa na saratani. Ndiyo maana watu wengi wanapata saratani bila kufahamu chanzo Chake.


Plastiki zinazotupwa ovyovoyo na kusambaa majini (Baharini na ziwani) kadri uchumi unavyokua na matumizi ya plastiki ndivyo yanavyozidi kuwa. Mifuko ya Plastiki bila kujali unene wake, hairuhusiwi kuingizwa, kusafirisha, kutengenezwa na kutumika. Katika Nchi ya Uganda, mifuko ya plastiki pia imekuwa tishio kwa wananchi.

Wananchi wameagizwa kutumia majani ya mgomba yaliyotumika ili kubeba bidhaa zao. Nchini Uganda mrundiko wa taka za mifuko wa plastiki huathiri huduma za maji. Viumbe vya ardhini na majini huathiriwa na plastiki hizo au kuwadhuru wanyama au ndege baada ya kumeza plastiki hizo. Sheria mpya ya mazingira nchini kenya imepigwa marufuku kutengeneza kuuza au hata kutumia mifuko ya plastiki.

Mfuko wa plastiki hukusanyika kandokando ya barabara na maeneo yasiyotumika na kuathiri mazingira na wanyama. Makampuni mengi yamepigwa marufuku kuzalisha, kununua au kutumia mifuko ya plastiki. Ni bora serikali kutoa njia mbadala ili kuepusha uharibifu wa mazingira na pia afya za binadamu. Wananchi ni bora kufahamu ni vyema kutahadhari kabla ya hatari.

Plastiki ina aina hamsini na mbili za saratani. Vilevile usinywe chai kwenye vikombe vya plastiki, usile chocolate chenye moto kilicho ndani ya mfuko wa plastiki kwa mfano vibanzi au chipsi. Isitoshe usipashe chakula kwenye “Microwave” kwa kutumia vyombo vya plastiki. Wanaharakati wa mazingira nchini kenya wanashikillia dhana kuwa Kenya ina Sheria muafaka za kudhibiti uchafuzi wa Plastiki,kwa kutilia mkazo utekelezaji.


Wananchi wanafaa kujua kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira safi. Tarehe tano Juni huwa siku ya mazingira duniani. Lengo kuu ya siku hii ilikuwa kutoa suluhisho kuhusu uchafuzi wa plastiki katika mazingira. Maadhimisho haya yalifanyika mjini Abidjan Cote D’Ivoire kwa ushirikiano na uholanzi. Plastiki hutengenezwa kutoka kwa fueli ya visukuku jinsi inavyozalisha madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Mifuko mingi ya plastiki imetengenezwa kwa msimbo wa resin ya polyethylene aina mbili za mifuko ya plastiki ni kama vile polyethylene na polypropen. Nchini Kenya waziri wa mazingira huitwa Soipan Tuya.
Mifuko ya plastiki ni mchangiaji mkubwa wa Dampo. Marufuku ya mifuko ya plastiki itakuwa afueni kubwa kwa shinikizo la taka zinazoendelea kwa Sasa. Mifuko ya plastiki hufuata njia ya mifereji ya maji. Mfumo wa maji taka huwa na harufu mbaya katika mazingira. Watu wengi wanatupa mifuko yao ya plastiki kwenye takataka au kuacha vikipeperushwa na upepo. Kuzipiga marufuku itafanyika kuzisimamisha kuchafua mazingira.
Malighafi inayotumiwa kutengeneza plastiki hutolewa kutoka kwa gesi asilia na mafuta ya petroli.

Hivi ni vyanzo visivyoweza kurejeshwa na uchimbaji na uzalishaji wao hutoa gesi chafu zinazochangia mabadiliko ya kitaifa. Tukizingatia athari ya mafuriko ya plastiki basi tutaishi bila kuathiriwa na magonjwa, serikali inafaa kutoa njia mbadala ili kuwasaidia wafanyibiasha, mjini Nairobi Gavana Johnstone sakaja ameweka mikakati ya kukusanya takataka.


Kuna baadhi ya malori ambayo hutumika kukusanya takataka. Uvundo hutokana na takataka iliyotupwa kwa kiwango kikubwa. Watu wengi hawafamu kuwa chupa za plastiki ni takataka, ingawa wanadai kuwa Ina manufaa, lakini huwa na madhara kwenye mazingira.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_img

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here