15.8 C
London
Friday, May 17, 2024

Mvua Ya Masika

Date:

Related stories

Why women struggle to take climate cases to court and how to correct it

By Pedi Obani A study in Nigeria and South Africa...

Calling off UN regional climate weeks exposes rich nations’ lack of goodwill

Funding these essential meetings would cost little to rich...

Don’t gaslight Africa: We need genuinely clean cooking solutions

The IEA summit, where oil and gas execs are...

Kenya: Adding up the costs of the floods amid an economic crisis

The devastation from the floods in Kenya have been...

Can We Use ChatGPT for Global Goods Software Development?

At IntraHealth, where our mission is to support health workers...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes


Gharama ya maisha ilibadilika kuwa ngumu Zaidi. Bei ya unga ilikuwa ghali mno.Wakenya wengi walilalamika kupita kiasi . Wazazi wengi walishindwa kuwapeleka Watoto wao shuleni. Kiongozi wa upinzani bwana Raila Amolo Odinga aliamua kuitisha maandamano. Wakenya wengi walijitokeza Barbarani ili kushiriki maandamano haya.


Hata hivyo wakenya walikuwa na matumani ripoti ya “NaDCO” almaarufu maridhiano itazaa matunda .Hadi sasa wanasubiri utekelezaji wa ripoti hiyo. Baada ya mchungaji mashuhuri Benny Hein kuzuru nchi ya kenya, kulikuwa na matumani chungu mzima. Mvua ya masika ilianza kunyesha . Wakulima walitia bidii kutayarisha mashamba yao kwa upanzi .Mtabiri wa hali ya anga bwana David Gikungu aliwaambia wananchi kuwa Kuna dalili ya mvua ya masika .


Mtabiri huyu alielezea dalili alizoziona ,katika utabiri wake alisema ukiona ardhi imekauka pamoja na mimea , ujue kuwa mvua iko karibu sana . Jua kali pia ni dalili ya mvua ukiona vipepeo weupe au ndege wa angani wakiruka kwenda upande mmoja , fahamu kuwa wamekwisha nusia harufu ya mvua. Watoto wa shule waliposikia maelezo haya kuhusu utabiri wa anga, walitaka kuhakikisha kutoka kwa walimu wao kuhusu jambo hili. Hii ni baada ya afisa wa polisi bwana David Cheshire kuaga dunia akiwaokoa wanawake wawili na mtoto mmoja. Ni jambo la kuhuzunisha kuwa mwili wa afisa huyu bado haujapatikana . Huku familia yake wakiiomba serikali kuhatarisha kumtafuta mahali alipo.


Wakati wa mvua umeme na mawingu ya mvua huzidi kuongeza.Upepo mkali nao huvuma na sauti ya radi ikawa kama inabisha mlangoni ili mvua ipate kunyesha.Hivyo basi mvua ikaanza kunyesha ulienea kila mahali. Mapaa ya nyumba yalikuwa mabovu Kisha yakaanza kuvuja . Kule Nairobi mvua ilinyesha kwa zaidi ya wiki mbili.


Katika mazingira hafifu , miti nyingi ziling’olewa na maji ya mvua. Mashamba mengi yalifunikwa na maji ya mvua . Mambo yalizidi kutisha , kwani mvua iliyokuwa imengojewa kwa muda mrefu , ilisababisha hasara kubwa kwa wakaji wa maeneo mbalimabali. Mambo yalizidi kuwa mbaya zaidi mvua hii ilibadilika kuwa ya gharika. Badala ya mvua kusaidia wananchi iliharibu mali ya watu kwa kiasi kikubwa. Mito ilifurika na madaraja kusombwa na maji ya mvua.


Iliwabidi wazazi kuwashauri watoto wao kukaa nyumbani mpaka wakati mvua hii itapungua kiasi. Watu huenda walikufa maji kwa kutofuata maagizo ya watabiri.Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Wakati mwingi mvua huja na dhoruba kali ambayo husababisha mabadiliko ya hali ya hewa . Mvua inaponyesha kupita kiasi husababisha mafuriko. Mafuriko ni matukio asili.Wakati mwingine hubadilika kuwa mawimbi. Wakati wa mvua ya masika watu hukadiria hasira chungu nzima . Watu pamoja na mifugo hupoteza maisha yao bila kutarajia. Zaidi ya familia elfu kumi na tano , zimeathiriwa , mifugo na mazao ya shambani imeharibiwa.


Katika kaunti ya kirinyaga. Mvua ilisababisha hasara kubwa .Maeneo ya mwea watu walikumbwa na mafuriko.Mifugo na mali iliharibiwa. Zaidi ya wakazi mia saba wa vijiji vitatu vya Mwea katika kaunti ya kirinyaga wamebaki bila makao .
Hii ni baada ya mto Thiba kuvunja kingo zake na kusababisha mafuriko katika kijiji hicho. Isitoshe familia mia nane katika maeneo ya Amboo Nyando zinahangaika baada ya mvua kunyesha kupita kiasi. Mvua husababisha mafuriko katika madaraja , Barabara hufurika kiasi Cha kutopitika . Tahadhari ilitolewa kuwa watu wahamia maeneo yaliyo salama salimini . Huduma muhimu kama vile uchukuzi wa vyakula hutatizika. Hii ni kwasababu barabara imeharibiwa. Imekuwa vigumu sana wagonjwa kufikia vituo vya afya ili kupata matibabu.


Katika kaunti ya Mombasa mvua iliyonyesha kupita kiasi ilisababisha maafa. Hii ni baada ya mto Ramisi kuvunja Kingo zake. Ni Bora kutahadhari kabla ya hatari . Wakulima walikuwa na matumani chungu mzima kuwa watapata mbolea na kuendelea na kilimo. Nchi Kenya ukulima ni uti wa mgongo. Mvua hii ya masika ilikumbwa na sakata ya mbolea.kule Garisa gari la abiria ilisombwa na maji, wananchi walinusurika kifo.
Walimu walifurika madukani ili kununua mbolea. Lengo kuu ilikuwa kuboresha mimea yao shambani. Hata hivyo mbolea hiyo haikuwa halali. Wakenya wengi walitoa malalamishi yao kuhusu mbolea ghushi. Ndani ya mbolea kulikuwa na kinyesi cha punda pamoja na mawe. Hata baada ya wakenya kutoa ushahidi wa kutosha , waziri wa kilimo Lintika Menturi anasema kuwa mbolea hiyo iko sawa katika kilimo.


Watu kadha wameshikwa na kupelekwa kortini , ni matumani kuwa suluhu itapatikana. Serikali imetoa taarifa kuwa wale ambao walinunua mbolea hii ghushi, watapatiwa mbolea nyingine. Rais William Ruto amewahakikishia wakulima watapewa mbolea bora. Si bora kutumia mbolea ghushi kwasababu huathiri udongo. Magonjwa malaria, dengi, huenezwa na maji mengi . Nchini Kenya hasa kule Lodwar kulikuwa na joto kupita kiasi. Huenda ujio wa mvua itawaletia baraka.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_img

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here