22.6 C
London
Friday, July 26, 2024
HomeCommunityFaida Za Mikoko Baharini

Faida Za Mikoko Baharini

Date:

Related stories

Kenya Railways Resumes Nanyuki Passenger Train Service after Three-Month Suspension

Kenya Railways has announced the resumption of the Nanyuki...

Medical Interns Protest Delayed Postings at Kenya’s Health Ministry

The medical, dental, and pharmacy interns in Kenya have...

Kenya Increases Bond Fee, Posing Hurdle to Uganda’s Fuel Import Scheme

Kenya has thrown a fresh hurdle on Uganda's direct...

Understanding the Phenomenon Behind July Rains and Hailstorms in Nairobi and Other Kenyan Regions

Kenya Meteorological Department on Sunday cautioned Kenyans to brace...
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes

Miti ya mikoko, majani, matunda, mzizi ,miche na mashina hutumiwa kutibu maradhi mbalimbali. Baadhi ya hali hizo ni pamoja na uponyaji wamajeraha, kuendesha, kisukari, uvumbe, maambukizi ya ngozi na kiwambo cha sikio. Pia inaweza kutumika kama dawa ya kuua mbu.

Mikoko ni aina ya miti au vichaka vinavyokua katika maji ya chumvi kwenye fuko za bahari kando ya tropiki. Miti hii inaaiinishwa katika aina tatu. Neno mikoko inatokana na neno la kireno mangue ambalo maana yake ni miti.

Katika kingereza mikoko ni “Glove” ambalo hutumika kwa miti au vichaka vinavyopatikana katika maeneo yenye kina kifupi kwenye mchanga wa matope. Mikoko husaidia aina mbalimabali za wanyama wanaovutia watalii na kuleta mapato kwa jamii .Miti ya mikoko hutumika kutengeneza bidhaa zinazotumiwa na jamii na kote ulimwenguni. Katika kaunti ya Mombasa mikoko hutumika kama miti yenye thamani zaidi.

Mikoko huwa mazalia ya samaki na huwa kama Kinga dhidi ya dhoruba, mmomonyoko wa ardhi na mafuriko. Pia husafirisha hewa mara tano zaidi ya misitu. Lengo kuu ya mikoko ni kuhifadhi kaboni ikiwa baharini. Ni bora kufahamu kuwa ni wazi kuwa upanzi au uhifadhi wa mikoko ni mojawapo ya suluhu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hasa katika mazingira ya baharini. kuendeleza kuipanda upya mikoko kutapunguza athari ya tabianchi na kuboresha maisha.

Mikoko inachuja maji ya chumvi na kuondoa asilimia tisini ya chumvi inayopatikana katika katika maji ya bahari na kuingia kwenye mizizi yake. Vilevile Mikoko husaidia kupunguza kasi ya mawimbi makubwa ya bahari ambayo yanaweza kufanya uharibifu katika maeneo ya pwani. Iwapo mikoko itaharibiwa, Kuna uwezekano wa kuwa na baa la njaa. Mikoko ndiyo mahali ambapo uzalishaji wa samaki hufanyika. katika kaunti ya kwale mikoko inatunzwa kwa ushirikiano na shirika la huduma za misitu nchini kenya. Kikundi Cha jamii pia huhifadhi misitu. Shirika la mazingira la umoja wa kinataifa imepiga jeki huhifadhi mikoko.

Miradi ya ufugaji samaki imepigwa jeki kwani wenyeji wamepata kuongeza mbinu nyingi ili kujipatia riziki badala ya kuendeleza uharibifu wa Mikoko. Aina ya samaki wanaofungwa ni pamoja na tilapia , mborode na kambakamba. Mikoko inaweza kuhifadhi hewa ya kaa kutoka angani na kuzalisha oksijeni kupitia kitendo cha mimea kiitwacho “photosythesis ” oksijeni inayozalishwa hutumiwa na mwanadamu na viumbe hai wengine katika mfumo wa upumuaji.

Siku ya kutunza mikoko duniani ni Julai ishirini iliidhinishwa na mkutano wa shirika ya elimu ya kisayanasi na utamaduni la umoja wa mataifa. Mikoko inaangamia kati ya mara tatu au tano kwa kasi kuliko uangamiaji wa misitu, hali hii husababisha athari kubwa kwa ikolojia na kwa uchumi wa jamii. Inakisiwa kuwa mikoko imepungua mara dufu kwa miaka arobaini iliyopita.
Kule baharini ni furaha ni kwa wavuvi pale wanapovua samaki wa kutosha. Ila pale samaki wanapokua haba baharini mvuvi hukosa amani na maswali mengi huibuka ni nini haswa kinachosababisha samaki kupungua kabisa.

Wavuvi wa kujiji Cha Dziphani ambao wapo katika kikundi kinachotoa ulinzi baharini “Bonje ” wametambua kuwa uharibifu wa mikoko ni mojawapo ya sababu samaki wamepungua. Upandaji upya wa mikoko katika maeneo yaliyoharibiwa unalenga kizazi kijaacho. Baadhi ya wavuvi wengi wamelazimika kuacha uvuvi na kutafuta njia mbadala ya kujikimu. Kikundi cha Bonje kinajumisha wavuvi , wachuuzi na kina mama.Wanaokaanga na kuuza samaki hupenda kuchoma na kuuza Miche huku wakipanda upya mikoko kwasababu wanatambua faida zake.

Katika ngazi za kimataifa, mojawapo wa miradi ya kwanza inayojihusisha na biashara halali ni uzalishaji wa gesi ya ukaa. Shughuli hii imewezeshwa na upandaji wa mikoko. Kulingana na mwenyekiti wa kikundi bwana Saidi Chirunga anasema uharibifu wa mikoko umetekelelezwa na wakazi wanaokata mikoko kwa matumizi yao ya kibinafsi pamoja na kusababisha mafuriko. Kwa mfano mvua wa Elnino mwaka iliyopita.

Mikoko pia hufanya kazi ya kukabiliana na mafuriko, tsunami, mawimbi baharini na mmomonyoko wa udongo. Mchanga wake huweza kumeza gesi ya ukaa na hewa ya ukaa na kupigana na kiwango kikubwa Cha kaboni. Bi konde alionyesha kuwa mustakabali wa wanawake na watoto katika eneo hilo la kwale utakuwa zaidi pindi mradi huo,utapokuwa na mafanikio wao ndio watakaoathirika zaidi na mabadiliko ya tabianchi. Kukata miti ovyo ya mikoko kwa ajili ya mbao na makaa ni hatari mno. Katika kaunti ya Kilifi watu wengi hutegemea makaa kwa upishi.Jamii ya K.D.F. wamepanda mikoko eneo la Dabaso hii ni juhudi za kuhifadhi mazingira . Tukitunza mazingira yetu bila shaka tutaishi maisha ya kujivunia , tusiharibu mikoko kila wakati bali tutafute njia mbadala ya kujipatia riziki.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_img

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here