12.5 C
London
Saturday, May 18, 2024
HomeCommunityAthari ya Kelele Katika Jamii

Athari ya Kelele Katika Jamii

Date:

Related stories

Why women struggle to take climate cases to court and how to correct it

By Pedi Obani A study in Nigeria and South Africa...

Calling off UN regional climate weeks exposes rich nations’ lack of goodwill

Funding these essential meetings would cost little to rich...

Don’t gaslight Africa: We need genuinely clean cooking solutions

The IEA summit, where oil and gas execs are...

Kenya: Adding up the costs of the floods amid an economic crisis

The devastation from the floods in Kenya have been...

Can We Use ChatGPT for Global Goods Software Development?

At IntraHealth, where our mission is to support health workers...
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes

Kufanya kazi katika mazingira ya kelele kunaweza kusababisha matatizo ya kiafya na kiusalama kwa wafanyikazi Kijijini, tatizo linalojulikana, kwa wengi ni kupoteza uwezo wa kusikia.Ni vyema kutambua athari ya kelele ndipo uchukua hatua katika suluhu kabambe.

Katika kaunti ya Nairobi kuna magari ambayo huweka sauti ya juu zaidi . Muziki ikiwekwa katika sauti ya juu wateja hupiga kelele,huku wakiwakemea madereva. Pia Kuna baadhi ya makanisa ambazo huwa na tabia ya kuweka sauti ya juu mno.Ingawa muziki huburudisha jamii lakini Kelele kupita kiasi si bora katika afya ya binadamu.
Kuathirika kwa mtoto aliyeko tumboni. Mwanamke mjamzito anayefanya kazi katika mazingira ya kelele ana uwezekano mkubwa wa kuathiri mfumo wa usikiaji wa mtoto aliye tumboni na hivyo basi kuzaa mtoto akiwa na matatizo ya kusikia.

Msongo wa mawazo, kelele kubwa maeneo ya kazi husababisha matatizo kama maumivu ya kubwa. Kupoteza utulivu na kukosa usingizi kazini. Matatizo haya kwa muda mrefu huwa yanazaa msongo wa mawazo.Iwapo tatizo la msongo wa mawazo halitashughulikuwa mapema lnaweza kupelekea kuwa na matatizo mengine ya akili .Mjini Nairobi watu hufurahia muziki wa juu wakati wa usafiri bila kutambua kelele Ina kero.

Ajali kazini, kelele kupita kiasi katika mazingira ya kazi inaweza kuharibu mawasiliano baina ya wafanyikazi hivyo kushindwa kusikia milio ya dharura inayoashiria hatari kama vile honi ya gari , milio ya hatari ya moto,hali hii inayoweza kupelekea kupoteza maisha kutokana na ajali .

Kelele huathiri mfumo wa kusikia.Hii inaweza kusababishwa na kelele kubwa inayopelekea kuziba sikio .Kwa njia ya kusafirisha mawimbi ya sauti au kuharibika kwa “Ear cell” ndani ya “cochlea” ambayo hupatikana ndani ya sikio.

Tatizo hili linaweza kusababishwa na kelele katika mazingira kwa muda mrefu , dalili ya kwanza ya tatatizo hili ni kukosa kusikia sauti zenye mawimbi kupita kiasi. Kelele husababisha “Tinnitus” hii ni hali ambayo hujitokeza kwa mfanyikazi aliefanya kazi katika mazingira ya kelele kwa muda mrefu.

Katika Hali hii Kuna milio wa sauti zisizoeleweka anapokuwa katika eneo tulivu lisilokuwa na kelele. Milio wa risasi huharibu usikivu,Wapo watoto waliopata uziwi baada ya kusikia kelele na watu wazima waliopoteza uwezo wa kusikia kutoka na kelele za kimazingira na zile zilizosababishwa na matumizi ya spika za masikioni .

Kuna sehemu mbalimbali ambazo kelele husikika kama vile kanisani, kilabuni na pia katika sherehe kama harusi.Watu lazima washangilia wakati ndoa zinafungwa kanisani.Ni bora kufurahia Sherehe lakini sauti isiwe ya juu zaidi kupita kiasi kwa vile italeta madhara ya afya kwa binadamu.

Sauti zisizofaa kwa muda mrefu na zilizo juu sana kutoka kwa trafiki barabarani. Reli au shughuli za burudani huathiri afya na ustawi wa binadamu. Hali hii ni pamoja na kukerwa mno na kukosa usingizi, Hali inayopelekea magonjwa ya moyo mbaya zaidi .Kutoweza kusikia vizuri na kudorora kwa akili ya binadamu husika.

Kelele zinazozidi viwango vya juu Zina athari kubwa kwa jamii , athari zinazotajwa ni pamoja na waathiriwa kukusa usingizi, matatizo ya usikivu , kuongezeka kwa mapigo ya moyo kusiko wa kawaida na kupelekea shinikizo la damu na hata Mimba kuharibika. Sauti asilia zinaweza kuwa na manufaa mbalimbali ya kiafya.

Wapingaji wa miji wanapaswa kutoa kipaumbele kwa upunguzaji wa kelele kwenye vyanzo vyake, kuwekeza kwenye njia mbadala za usafiri na miundomsingi ya mjini inayounda madhari chanya. Kelele husababisha kupoteza au usumbufu wa usingizi na mipigo ya moyo yasiyo ya kawaida hutokea haraka au poleple.

Ni Bora wamiliki wa maeneao ya sherehe, nyumba za kuabudu na studio mtaani kuzingatia sherehe na miongozo ya kudhibiti kelele. Vilevile Kelele kupita kiasi Zinaathiri jamii. Kelele zimeainishwa kwa njia nne tofauti. Mambo unayosikia siku nzima yanaweza kuwa Kelele isiyokoma, kelele ya vipindi, kelele ya msukomo au Kelele ya chini ya mara kwa mara.

Kwa kuelewa uainishaji huu. Utaelewa vyema hatua unazoweza kuchukua ili kulinda usikilizaji wako wa muziki. Kelele ni sauti isiyohitajika inayotumiwa na haifa katika mazingira. Tofauti ya kelele na sauti ya kawaida hutokea wakati ubongo unapokea na kutambua sauti.

Kelele ya mazingira ni kelele inahusishwa na shughuli za binadamu wakati anapoimba, katika tamasha za muziki lazima utasikia Kelele, hata katika wimbo wa kitamaduni watu hushughulika na utasikia kelele kwa umbali.

Maeneo ya shule au hospital yanahitaji kuwa na utulivu wa kutosha. Kwasababu wagonjwa wanahitaji kupona haraka.Kule shuleni nayo shughuli za masomo huendelea.Mchezoni wachezaji walioshinda hutumia kelele kumshangilia timu yao, kama vile waswahili husema kelele za mwenye nyumba hazimkatazi mgeni kulala .

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_img
Previous article
Next article

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here