4.9 C
London
Sunday, December 22, 2024
HomeCommunityUKEKETAJI NCHINI KENYA

UKEKETAJI NCHINI KENYA

Date:

Related stories

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities In the...

Challenges Facing the Kenya’s Current Socio-Political Landscape

Kenya's current socio-political landscape is shaped by a series...

A Global issue about Female Genital Mutilation

Female Genital Mutilation (FGM), also known as female circumcision,...

Faida Ya Kupanga Uzazi

Upangaji uzazi ni muhimu sana katika familia, inahusu wanandoa...

Madhara Ya Vita Katika Jamii

Hali ya majonzi ilitanda katika kaunti ya Tana River....
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Ukeketaji ni dhuluma ambayo huendelezwa na baadhi ya jamii humu nchini . Licha ya serikali kujifunga kibwebwe ili kukabiliana na janga hili. Bado linatishia kuendelea kuharibu mustakabali wa vijulanga wa kike humu nchini , kule samburu ni kilio tele. Kuna viongozi wa kidini hapa nchini ambao hutegemea Mila na desturi za jadi katika jamii na ambao kisiri huunga mkono ukeketaji , hivyo basi huhujumu vita dhidi ya ukeketaji.

Pia ni Hali tofauti kabisa ambapo shughuli hiyo ambapo zamani iliendeshwa kisiri vichakani hasa huko mashinani leo, hii imekuwa biashara ya faida na ambapo kuna wauguzi ambao hulipwa ili kukeketa katika usiri wa vyumba vya kifahari na pia katika hospitali.Aidha Kuna wakuu wa kiusalamu ambao wamethibitishwa kuwa waaguzi wengine wamejiunga wa wale ambao wamekataa katakata katika jamii.Wengi hao wanachochowewa na tamaa ya kujipatia kipato .

Hii dhibitisho ya kutosha kuwa umaskini ni mojawapo ya vizingiti vikubwa katika vita dhidi ya ukeketaji. Hata hivyo, si umaskini tu Bali pia unyama kwa jinsi ya kike. Unyama huu unatokana na ukweli kwamba ukeketaji huu una madhara si haba kwa yule anayekeketwa kwa hivyo, mtu anayethamini hela anazopewa kushinda maisha ya mwenzake ni mwovu anayefaa kutiwa mbaroni na kuozea katika jela.Uchunguzi hivi karibu umedhihirisha kuwa idadi kubwa ya wale waliokumbatia ukeketaji huu ama hawajui Madhara yake au wanajitia tu hamnazo .

Kuna wale ambao, kwa kupofushwa na kauli kuwa mwacha Mila ni mtumwa. Wanajitolea mhanga kiasi Cha kuwakeketa hata wasichana wangali tumboni.Kumbuka kila mkenya afahamu kuwa njia za kitamaduni za ukeketaji Zina madhara si haba. Moja wapo ni ya kushangaza mno maishani.Uvujaji wa damu kiasi Cha kusababisha kifo ni mojawapo tu ya athari hizo, mtu ambaye hupasha wasichana tohara huitwa ngariba .

Ni Bora kufahamu kuwa ngariba hutumia wembe mmoja kuwapasha wasichana kadha tohara .Hali hii ikitokea kuwa rutuba ya kukuza maangamizi kupita kiasi. Ukeketaji wowote ule , uwe wa kale au sasa , humwathiri mhusika kisaikolojia . Dhuluma hii huweza kumfanya mhusika huyo asijichukie Bali pia jamii nzima iliyochangia kumletea madhara mno. Baadhi ya wale waliopitia ukatili kama huu. Wasiposaidiwa kupona majeraha ya moyoni . Huweza kulipiza kisasi kwa wenzao au hata kuishi maisha yaliyosheheni uchungu na maumivu ya ndani kwa ndani. Ni jukumu la kila mkenya kuthamini faida tunazopata kutokana na Mila na desturi zisizokuwa na umuhimu wowote zitupiliwe mbali .

Ukeketaji una faida gani? Wale waliokeketwa wanawashindia nini wale ambao hawajakejetwa ? Tukipiga suala hili darubini.Tutangamua kuwa ukeketaji haileti faida yoyote. Ni matatizo utokao kwa wanajamii wanadai kuwa mwacha Mila ni mtumwa je, hawajui kuwa Mila potovu ni mwasi endako Hana kiasi. Katika bibilia takatifu , tohara ambayo hutambuliwa ni ya wanaume . Wale ambao wanatekeleza ukeketaji ni kinyume Cha Sheria. Si jambo la haki Bali ni hatia. Nchini kenya Kuna baadhi ya jamii ambazo bado wanatekeleza unyama huu. Kwa mfano jamii ya kisii , Maasai na hata Kalenjin.

Pia wasamburu hawajawachwa nyuma.Rais William Ruto katika taarifa zake kwenye mtandao amekashifu vikali kitendo hiki. Ametoa hakikisho kuwa yule atapatikana akitekeleza ukeketaji nyumbani au mafichoni atiwe mbaroni mara moja.Baadhi ya machifu pia wamepewa jukumu la kuwanasa Hawa kina mama ambao hutekeleza uovu huu. Pia mafunzo kabambe imetolewa kuhusu athari ya ukeketaji wa wasichana. Kule kanisani viongozi wa kidini pia wamekuwa kipao mbele kupinga unyama huu. Mtoto ana haki mbalimbali kama kuelimishwa , kupewa lishebora na makazi Bora .

Ukeketaji ni kukiuka haki za watoto wote ni sawa tusiwabagua kwa msingi ya kijinsia. Wakati ngariba anatumia wembe mmoja kukeketa wasichana kadha , Bali na uchungu inaweza kusababisha maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi. Kwasababu si salama kutumia kiafya. Kila msichana anafaa kuwa na kuwa na wembe wake . Ni bora kutahadhari kabla ya hatari. Afya ni tija , hakuna ajuaye isipokuwa mwenye maradhi ni wazi kuzithamini afya zetu kila mara na kuepuka madhara.

Twapaswa kuhimiza serikali yetu kufanya kila iwezekanavyo kuhakikisha kuwa wanapopashwa tohara ni wale ambao Wana cheti maalum , ili kupunguza vifo, kwa mfano kule Uasingishu mahali vijana walipoteza maisha. Pia twastahili kubadilisha misimamo wetu kuhusu ukeketaji na kuzilinda kwa dhati . Haitoshi kupeleleka miswada bungeni Bali kuzingatia Sheria kwenye katiba.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img