3.5 C
London
Friday, November 22, 2024
HomeInternationalKENYAKwa nini Watu Hujitoa Uhai Nchini

Kwa nini Watu Hujitoa Uhai Nchini

Date:

Related stories

Why Africa is Still Poor?

Africa, rich in natural resources and cultural diversity, paradoxically...

Kenya’s Journey Toward a Cashless Economy

Kenya has been at the forefront of the digital...

Mau Mau: Mukami Kimathi’s swansong to a city at war

By Jaclynn Ashly 72 years after the Declaration of Emergency...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Kujitoa uhai ni Hali ya kujiua. Watu hupitia mengi maishani kulingana na Hali ngumu ya maisha. Kwa hivyo Jambo hili huwafanya kuwa na msongo wa mawazo. Njiani utaweza kumpata mtu anaongea peke yake barabarani. Hali ya maisha imekuwa ngumu mno,ili kujiondoa katika aibu , utawapata watu wengine wanaamua kujitoa uhai, hata shuleni utawapata wanafunzi, wanajitoa uhai. Hata shuleni utawapata wanafunzi, wanajitia kitanzi ikiwa amefali mtihani na anaogopa kuwa mwalimu au mzazi alikuwa na matumaini kuwa atapata alama za juu zaidi. Si ajabu kusikia kule kazini pia utasikia mtu amejitia kitanzi ikiwa mwajiri ana uhusiano mbaya na mwajiriwa.

Hata hivyo, Kuna mambo kadha ambayo husababisha mtu kujitoa uhai mara kwa mara kama vile, wataalamu wanasema kuwa kujitoa uhai hakufanyiki bila sababu, utafiti unaonyesha kwamba takribani asilimia tisini vijana wanajitoa uhai Wana matatizo ya kiakili . Chanzo Cha tatizo hilo huaminika kuwa shinikizo la kiakili, ikiwa ndio tatizo la kwanza Bali na ghasia ama utumizi wa dawa za kulenya. Kuna unyanyapaa unaohusishwa na mtu kujitoa uhai.

Ni muhumu kufanya utafiti ili kubaini hali hii ikiwa mtu alikuwa mgonjwa Kisha akawa mwendawazimu , ili kujitoa katika hali ya aibu na kuhagaika maishani , ataamua heri ajitoa uhai kutokana na unyanyapaa.
Utakuta kwambu kiwango ambacho wakenya wanajiua ni kubwa sana. Tuna visa vya watu Kuwaua wengine hasa wanafamilia, wapenzi wa kike na kiume . Kuua kiholela. Suala la kujiua ni tatizo humu nchini, sio tu katika idara ya polisi. Katika kaunti ya Bomet Kuna mwanamume ambaye aliamua kuua watoto wake wote Kisha yeye pia kujitoa uhai. Sababu za kujitoa uhai hakueleza familia yake.

Ahadi za Uongo hufanya wanafunzi kujitoa uhai. Wazazi wa siku hizi wanakwepa kuwajibika kufuatilia mambo ya watoto wao na kuwaelezea kweli kuhusu hali ya kiuchumi inayowakabili kwa wakati huu. Epuka kumdanganya mtoto ama kutoa ahadi za Uongo isioweza kutekeleza na kama ikitokea umechelewa au huwezi kutekeleza kwa wakati huo, zungumza na mtoto na kumweleza hali halisi, kama ni suala la shule mweleze hatua ulizochukua katika kukabiliana na Hali ya Maisha.

Ni muhimu kufahamu kuwa utafiti unaonyesha kwamba vifo vya kujitoa uhai hupatikana kwa wingi katika vijana wa umri kati ya maika hadi ishirini na Tano katika mataifa yenye mapato ya chini mno. Kwa jumla wanaume wengi hufariki kwa kujitoa uhai ukilinganisha na wanawake. Wakati wanandoa hukosa uaminifu kati Yao husababisha kifo. Mwanamke mmoja katika kaunti ya Kisumu aliwashangaza wengi sana, kwa kujitoa uhai.

Inasemekana alichukua hatua hiyo kutokana na tabia ya mumewe kuwa na uhusiano wa kipamenzi nje ya ndoa.
Mary AKinyi alijitia kit
anzi karibu na nyumba ya mwakilishi wa wodi , Nerea OKombo na kuacha ujumbe kuwa kifo Chake kilitokana na tabia za mume kushiriki ngono nje ya ndoa.

Katika kaunti ya Mombasa msichana wa umri wa miaka kumi na minne alijitoa uhai baada ya kuagizwa kurudia darasa. Watu wengine pia huamua kujitoa uhai Wakati wamepoteza ajira kazini. Jambo hili humfanya mtu kukosa matumani maishani.
Watu wengi hujitoa uhai baada ya kukumbwa na matatizo na kushindwa kukubali msongo wa mawazo. Mafarakano ndani ya nyumba na baadhi ya watu kuwa dhaifu katika jamii husababisha Hali ya kujitoa uhai.

Baada ya kuona dalili za mtu kutaka kujiua ni jukumu la jamii kumsaidia mtu huyo ili kumwepusha na kujiua hata kama yeye mwenyewe haelezi kinachomsibu. Inafaa kumchukua mtu huyo na kumweleza ukweli kuhusu anavyoonekana ili kuepuka kujitoa uhai. Wazazi wakifanya hivyo tutaepuka au kuzuia kifo. Wanasaikolojia, wazazi na viongozi wa dini wanasema kuwa pengo limeachwa na makuzi ya watoto Hali inayosababishia watoto kuchukua uamuzi wa kujitoa uhai. Kila jambo huanzia nyumbani vile wazazi wameamuandaa mtoto, namna gani mtoto anadhani akikosa kitu Fulani basi lazima ajiue. Ni vyema mzazi kutoa ushauri na maelekezi kila mara kunapotokea jambo.

Kwa bahati mbaya watu wengi hawana ufahamu kuhusiana na kujitoa uhai, wanasita kuzungumzia suala hilo la kujitoa uhai. Wengine wanaweza kutojali au kutoa maneno ya kuumiza mtu kimakusudi. Ni Bora kuwa mwangalifu kuhusu nani unayemwambia kuhusu kujitoa uhai. Pia ni Bora kuchagua kazi kulingana na nia au lengo. Kuna baadhi ya maafisa wa polisi ambao hujiunga na taaluma hiyo kwasababu wanasaka kazi na mshahara lakini wanabaki kuvunjika moyo. Hali hii huweza kutokea ikiwa Kuna mahitaji mengi lakina pesa ni kidogo, bila shaka afisa huyu huamua kujitoa uhai au kujitia kitanzi, ili kupunguza hali ya kujitoa uhai, ni vyema kupunguza hasira, tumjue mwenyezi Mungu na tuwe tayari kueleza jamii au rafiki wa karibu shida zetu kila mara

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img