Ukosefu wa kazi katika nchi imekuwa tatizo kubwa kwa wananchi. Kama tungeweza kuketi na kuzingatia maneno ya viongozi wetu, tungetambua umuhimu wa kujiajiri kibinafsi. Viongozi hupatia matumani mengi baada ya uchaguzi, lakini wanapochukua hatamu ya Uongozi, raia ndio huteseka zaidi.
Je, tunawezaje kujiajiri? au kila mara kutegemea viongozi. Kusema kweli, kuna njia mbalimbali za kutimiza jambo hili. Nazo ni kama zifuatazo. Kuna wananchi wengi wenye mashamba au ardhi ya kutosha ambayo inapaswa kulimwa. Kuna misimu mbalimbali kama vile masika, kiangazi, kipupwe na kadhalika. Masika ni wakati wa baridi kali ilhali kiangazi ni wakati wa jua Kali sana kupita kiasi.
Mara nyingi utaona kuwa watu huacha mashamba yao Kijijini na kuenda mijini kutafuta kazi ya kuajiriwa. Ni bora wangerudi mashambani na kulima kwa kutumia teknolojia ya kisiasa. Vijana hawa hulia kuwa hawana kazi. Kisha wao hutegemea wanasiasa kila wakati. Ni bora wananchi kuzingatia kukuza mazao yafaayo kwa hali ya anga katika sehemu ambayo wanaishi. Si kupanda mazao bila kuwa na mpangilio. Udongo ufaa kupimwa ili ujue ni mimea ipi salama kupandwa.Kuyafuata maagizo ya maafisa wetu wa kilimo huleta manufaa.
Kama vile uzuiaji wa mmomonyoko wa udongo na kuongeza rutuba ardhini. Hali kadhalika, inamlazimu mkulima kupanda mimea kama mboga au miti ya matunda ambayo itamletea faida kubwa . Mkulima huyu anapofanikiwa anaweza kuwaajiri wafanyikazi na hivyo basi atakuwa amepunguza idadi ya watu ambao hawana kazi nchini kenya.
Kungojea kazi ya ofisi ni kupoteza wakati. Ikiwa Kuna wizara ambayo ina faida tele nchini ni ukulima. Ni vyema wazazi kuwazungumzia vijana kuhusu umuhimu wa ukilimo. Kama tujuavyo kilimo ni uti wa mgongo wa nchi.Wananchi wengi wamekuwa wakishawishika kwenda mjini. Wanaamini kuwa njia moja tu ya kujipatia fedha ni kufanya kazi za mishahara na baadaye watarudi mashambani kwa mapumziko tu.
Wanaacha ardhi zao na kukaa bila chote. Wazee ndiyo hujihususha na mambo ya kilimo. Jambo hili husababisha hasara kubwa.Watu wenye afya ya kutosha na nguvu hukimbilia mjini na kukaa huku kwa miezi mingi, huku wakitegemea jamaa na marafiki kuwatumia msaada. Kule mjini wanakubwa na fujo, familia kule Kijijini wanaishi maisha ya taabu hawana mbele wala nyuma.
Kando na ukulima, Kuna kazi nyingine tunaweza kuzifanya na kujipatia riziki. Kazi hizi ni kama ufundi wa namna mbalimbali na biashara, kwa kuhimiza mambo haya. Serikali yetu ikishirikiana na wananchi imejenga vyuo vingi vya kiufundi, biashara na ukulima. Katika vyuo vya kiufundi wananchi wanapewa ujuzi wa kazi za mikono kama ujenzi, useremala, ushonaji, ufundi wa mabomba, umakanika na sanaa ya uchoraji. Wanapohitimu wanaweza kujiajiri na kupunguza ukosefu wa kazi. Mjini Nakuru Kuna chuo Cha ufundi ambayo huitwa “Seisei institute ” wanafunzi wengi wamesomea mambo ya ufundi katika chuo hiki.
Kule viwandani shughuli mbalimbali hufanyika. Kuna mashine kubwa ambayo huipokea na kuichanuachanua pamba, huku ikitoa mbegu na uchafu kutoka kwa pamba. Kisha pamba hiyo hupitishwa katika mashine zingine ambazo huifinyafinya mpaka ikawa blanket refu la pamba tupu. Hii ni njia moja ya vijana kujiajiri ikiwa watapata kazi ya ofisi.
Blanketi hiyo hutiwa kwenye mashine zenye menomeno ambazo huchana nyuzi hizo za blanketi kuwa namna ya kamba Nene kidogo. Kamba hiyo hupitishwa kwa mashine ambazo huigawanya, katika nyuzi za unene mbalimbali. Nyuzi zenyewe huwa laini, nyembamba na zingine nene zinazotumiwa kufumia vitamba vyepesi au vizito.
Baada ya kufumwa fumwa, vitamba hivyo hupitishwa katika mitambo ambayo huvifua ili iwe safi. Kwa vile tutawezi kuwa na vitamba vya rangi ambao hupitishwa katika mitambo ya kutia rangi na maridadi mbalimbali. Baadaye vile vitambaa hukaushwa na kufungwa katika majora tayari kwa kuuziwa wenye maduka.
Hivyo basi, wananchi hununua majora haya na kushona mavazi kama mashati,marinda na suruali, kuna kazi ya karani ,yeye hupokea na kupiga simu pia hutunza barua,husoma, hupiga na kupokea simu afisini.Kiwanda ni mahali mafundi hutengeneza bidhaa. Katika viwanda Kuna vifaa kama cherehani, tarakilishi na tapuraita. Tarakilishi ni mitambo wa kielekroniki unaotumiwa kuhifadhi rekodi au ujumbe uliochanganuliwa.
Hakimu na tarishi hawa hufanya kazi tofauti. Hakimu pia huitwa jaji. Mahakamani Kuna kiongozi wa mashtaka na karani wa korti. Tarishi hupeleka na kuchukua barua kutoka posta. Mzegazega naye ni mtu ambaye huuzia watu maji mjini au Kijijini kule wakati. Ili kufanikisha malengo yetu maishani, ni bora kuchangamkia kazi za mikono, utafiti inaonyesha kuwa vyuo vya ufundi vina manufaa katika jamii. Mwanafunzi anapomaliza masomo yake anaweza kupata kazi kwa haraka. Si vyema kudharau vyuo vya kiufundi. Ni matumani yangu kuwa vijana wengi watajiunga na vyuo hivi.