Msaada wa teknolojia, teknolojia ya kisasa inawawezesha wanafunzi kuiba kwa njia rahisi na hali ya juu zaidi. Wanafunzi hupakua kwenye intaneti karatasi za mtihani pamoja na majibu ya kazi walizopewa kufanya nyumbani kisha kusambaza kwa wengine. Mara nyingi ni watu wachache tu wanaoshikwa kwasababu hiyo wengine hupata ujasiri wa kuiba mtihani.
Uvutano wa mifano mibaya,kuiba kumekuwa jambo la kawaida hata kati ya watu wazima, katika makampuni makubwa, siasa, michezo na mara nyingi hata nyumbani, ambako wazazi hudanganya kuhusu kodi au bima. Watu walio na mamlaka au wale wanapaswa kupigwa hawafai kusema uongo. Walimu wengi wanadai kwamba visa vya kuiba mtihani kutokea kwasababu ya kuzorota kwa maadili, visa hivi vimeongezeka kwasababu watu wanajifikira wenyewe tu na hivyo hakuna mtu aliye na maadili ya juu. Wanafunzi wanahitaji kupata alama za juu ili wakubaliwe katika shule nzuri. Hata wazazi fulani wameanza kuwa na maoni, kuwa ni lazima watoto wao wafaulu. Wazazi hupuuza au kukubali watoto wao wameiba mtihani shuleni, na hivyo kuathiri maadili ya watoto hata zaidi.
Ukosefu wa kujitayarisha, msisitizo wa kujipatia alama za juu kupindukia, kuongeza alama “A “katika taaluma yenye mafanikio na shinikizo kutoka kwa wazazi, ndio sababu ya kudanganya katika mtihani nchini kenya.
Wanafunzi wanafaulu sana kwa kuchanguliwa kwenda katika shule za hadhi ya juu. Lakini wakifika huko Utashanga kama kweli walifauli kwenye mtihani. Wao huendeleza tabia ya wizi na udanganyifu wa mtihani, jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya elimu nchini kenya. Hali hii hufanya nchi kuwa na madaktari wasiokuwa na ujuzi zaidi kutekeleza kazi zao kikamilifu.
Mwalimu anatamani wanafunzi wake wapate na kifaulu ili kujenga jina lake, na kutengeneza soko la ajira yake na mshahara mnono. Shule za kibinafsi huwapatia walimu na wanafunzi masharti makali mno. Jambo hili husababisha udanganyifu katika mtihani wa kitaifa. Kwa kufaulisha au kufaulu kupata kiwango cha juu cha alama, bila shaka wamiliki wa shule watagombania kumpata mwalimu huyo, ili afundishe shule zao kwa gharama yoyote.
Pia msimamizi wa Mtihani naye anaweza kuwa tayari kupokea kiasi kikubwa cha fedha ili kuruhusu, mianya ya wanafunzi kupewa majibu ya mtihani, huku askari anayesimamia usalama naye akipewa chochote kunyamazia pilikapilika zote za kupeana majibu. Haya ndio maeneo makubwa ambayo yanaweza kuwa chanzo muhimu cha, kuwepo vitendo vya udanganyifu na wizi wa mtihani. Kila Wakati mtihani unapokaribia wanafunzi huwa na wasiwasi. Pia Kuna baadhi ya shule ambazo hutumia njia ovu katika kufukia kufaulu katika mtihani wao. Ufisadi wa hali ya juu kupita kiasi ni kwamba walioaminiwa kuweka Siri katika mtihani hiyo. Mashindano miongoni mwa shule hufanya wanafunzi kudanganya katika mtihani.
Uzembe wa wanafunzi katika kujiandaa masomoni. Ili kufaulu katika mtihani wako, ni bora kufanya maandalizi ya mapema. Kuna baadhi ya wanafunzi ambao huwa na wasiwasi ikiwa watafeli mtihani. Kwa hivyo wanatumia njia ya mkato ili kupita mtihani.
Bali na kudanganya katika mtihani, kuna madhara ya udanganyifu wa mtihani wa kitaifa kama vile matokeo ya mtihani kwa jumla huathiri vikali kwani viwango vingine vya alama huwekwa juu sana.
Kwa wale ambao wanaojiunga na chuo kikuu, alama zao huwa zinakuwa za juu mno. Watu wengine huishia jela kwa kujihusisha na udanganya wa mtihani wa kitaifa. Wale ambao hupatwa na hatia baada ya uchunguzi kufanywa wao hufungwa jela. Wale watahiniwa ambao waliohusika katika udanganyifu hukosa matokea yao ya mtihani. Ni jambo la kuvunja moyo kuwa wanafunzi wasio na hatia huathirika kwa matokea ya mtihani Taasisi.
Matokeo mabaya baada ya kudanganya hufanya wanafunzi wengine hujitoa uhai. Wazazi wamekosa Imani kwa taasisi ya kushughulikia mtihani nchini, hii ni baada ya taasisi hii kuwa na matatizo mengi baada ya mtihani kufanywa. Kunatokea malalamishi mengi wakati wanakosa matokeo yao. Wengine wanawekewa alama za masomo ambazo hawakufanya. Ili kuzuia udanganyifu wa mtihani suluhisho zifuatazo zinaweza kusaidia.
Wanafunzi ni Bora kulenga kupata alama kulingana na uwezo wao. Wazazi wasiweze kulazimisha watoto wao kupata alama za juu zaidi, watoto huwa na uwezo tofauti. Wazazi wanafaa wawe na matajio ya matokeao ya Mtihani kulingana na uwezo wa watoto wao. Shule zishindane kulingana na kiwango Cha masomo. Mfumo wa elimu inafaa kufanywa marekebisho ili usiegemee kupita mtihani pekee, bali uangazie vipawa vya wanafunzi katika nyanja mbalimbali. Kama vile michezo Sanaa, nyimbo.Wasimamizi wa shule, wasimamizi na walimu kwa jumla wanafaa wawe macho Wakati wa mtihani.
Pia hatua Kali zichukuliwe kwa wale watakaojihisisha na udanganyifu wa mtihani. Mtihani inafaa kuchukuliwa kwa uzito zaidi, tuwe na lengo na kuwa makini. Ujio wa C.B.C. imepiga jeki udanganyifu wa mtihani kwa vile ujuzi ndio hutambuliwa. Heko kwa waziri wa elimu Ezekiel Machogu.