10.5 C
London
Saturday, November 16, 2024
HomeCommunityATHARI YA UONGOZI MBAYA NCHINI

ATHARI YA UONGOZI MBAYA NCHINI

Date:

Related stories

Why Africa is Still Poor?

Africa, rich in natural resources and cultural diversity, paradoxically...

Kenya’s Journey Toward a Cashless Economy

Kenya has been at the forefront of the digital...

Mau Mau: Mukami Kimathi’s swansong to a city at war

By Jaclynn Ashly 72 years after the Declaration of Emergency...

Youth Employment turn in Online Work

In a digital revolution, many young people are finding...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes


Imekuwa jambo la kutiliwa shaka. Iwapo utatembea mjini. Bila shaka utasikia wakenya wanajiuliza maswali mengi mno. Viongozi tuliowachagua walipotelea wapi? Ikiwa wapo je, mbona wakenya wanalalamika? Walisahau majukumu yao ama bado wanajipanga.
Athari ya Uongozi mbaya ni Hali ambayo husalia kwa muda baada ya mtu au kitu kufikiwa na jambo Fulani. Hata hivyo mfano wa Uongozi mbaya ni kama ifuatavyo.

Katika gatuzi la Busia , kutokana na usimamizi mbaya wa zahanati kukosa hazina ya dawa, Hali ya kutoweza kukabiliana na idadi ya wagonjwa ambao wanahitaji matibabu inaongezeka.
Vifo vya wagonjwa wengi vinatokea kwasababu serikali kuu inasema kuwa dawa zimeagizwa na ilhali hazijaagizwa . Mara nyingi wagonjwa wanalalamika kununua dawa nje ya hospitali kwa duka ambazo humilikiwa na madaktari wakuu . Mnyonge Hana haki Bali anasalia akiteseka kila mara.

Nchini kenya katika michezo , Kuna timu nyingi sana kama vile Gor Mahia , fc leopards na pia harambee stars. Uongozi mbovu unashindwa kusaidia timu hizi kufukia malengo Yao. Uongozi unapokuwa duni, unaweza kugundua sifa nyingi mbaya zinaaza kuchipuka ndani ya timu kwa ujumla.
Wafanyikazi wengi wanaanza kuthamini viongozi.wanabishana kati Yao wenyewe na wanaweza hata kuachana. Viongozi maskini huwanyamazisha wafanyikazi na wanajali tu maoni Yao wenyewe. Wanaweka hisia zao na ego juu ya mafanikio ya timu.

Viongozi hawawajibiki , kazi Yao ni kukusanya tu Kodi. Ni jukumu la viongozi kuhakikisha kuwa soko ni safi kwa kusafishwa vyema. Licha ya wananchi kutoa Kodi soko bado ni chafu sana . Ni jambo la kusikitisha kuwa unakatwa Kodi ya nyumba , katika mshahara wako, ilhali wewe mwenyewe huna nyumba . Kuna wale wamebakia na mwaka mmoja kustaafu , lakini Bado serikali inawanyanyasa kwa kuwakata Kodi ya nyumba bila kujali maisha Yao ya baadaye.

Baada ya kila uchaguzi viongozi huwashawishi wananchi ahadi nyingi ili wawaunge mkono . Serikali ya kenya Kwanza ilitoa ahadi tele kwa mama mboga na vijana . Wananchi walikuwa na matumani tele. Pindi tu baada ya kuchukua hatamu za Uongozi.

Hali hii yote ni ahadi hewa . Unafiki wa dini unaendelezwa nchini kenya. Nia ya dini ni kuhubiri neno kwa wakristo. Wale ambao wanashida mbalimbali huenda kanisani ili wapate usaidizi wa kiroho. Maovu yanaendelezwa kwa jina la dini. Makanisa yamegeuka kuwa tapeli zaidi . muhubiri tata, Paul Mackenzie na kanisa lake almaarufu ” new life international” imesababisha vifo vya waamini wake kule shakahola. Jambo hili ni athari ya Uongozi mbaya makanisa.
Wasomi wanashidwa kuyadhibiti maisha Yao . Baada ya vijana wengi kufuzu kutoka chuo kikuu, wanatarajia serikali itabuni nafasi zaidi za kazi. Kule mjini Mombasa Kuna kijana aliamua kujitoa uhai, kwasababu ya ukosefu wa ajira . Pia Kuna baadhi ya vijana wameamua kuchoma vyeti vyao vya masomo. Wengine wameshindwa kuudhibiti uraibu wa pombe , Kisha wanalala kwenye mtaro Barabara.

Katika gatuzi la Mombasa Kuna tatizo la ardhi. Viongozi wanapokea hongo kwa mabwenyenye , waliokuwa wamejenga sehemu zilizotengewa ujenzi wa hospitali kuu. Ni majabu viongozi Hawa hawajajenga zahanati . Maandamano katika miji kadhaa ya kenya yaliyoitishwa na upinzani , chini ya kinara wa mrengo wa chungwa raila odinga yanadhihirisha Uongozi dini.
Maandamano haya ni kuonyesha hisia zao kwa masuala kadha wanayoyadai kutoka kwa serikali ni wazi kuwa serikali imeshidwa kuwasaidia wakenya kukabiliana na Hali ya kupanda kwa gharama ya maishi nchini.

Si ajabu kusikia mtu mmoja ameuawa mpaka sasa kwa kupigwa risasi wakati polisi waliokuwa wakikabiliana na maelfu ya waandamanaji katika mji mkuu wa nairobi.pia ni jambo la kushangaza mno, benki zimefunngwa , biashara na hata watoto wameogopa kuenda shuleni, wao wanahofia usalama wao . Masaibu haya yote yanadhihirisha athari ya Uongozi mbaya nchini. Viongozi wa dini wanafaa kuvalia njuga suala hili ili kukomboa jamii.
Ukosefu wa maji jijini. Kwa miaka mingi umekumba Jiji la Nairobi na viunga vyake. Wapi viongozi tuliowachagua? Kazi wa Nairobi wanazidi kujiuliza maswali mengi akilini ili kukabiliana na huu. Serikali ya kaunti imeweka mfumo kadhaa mgao uliolenga mitaa kadhaa.

Katika gatuzi la makueni , masuala yanayoikumba eneo hili ni pamoja na njaa na ukosefu wa mvua . Inaponyesha sehemu nyingi za makueni sio ya kutegemea . Kaunti hii Huwa na uchache wa vyakula . Ni wazi kuwa viongozi wa makueni wamepuuza mahitaji wa wakazi Hawa waliowachagua na kuchangia Uongozi mbaya, Huku wananchi wanateseka .

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img