16.8 C
London
Monday, September 16, 2024
HomeCommunityVYANZO VYA UMASKINI NCHINI KENYA

VYANZO VYA UMASKINI NCHINI KENYA

Date:

Related stories

Retirement: The Beginning of a New Adventure

Retirement is often viewed as the end of a...

Corruption in Africa: A Persistent Threat to Economic Growth and Development

Corruption remains one of the most profound challenges facing...

Top Strategies for Successful Marketing in the Digital Era

In the rapidly evolving digital landscape, businesses must adapt...

Strategies to Eliminate Debt and Achieve Financial Freedom

Debt can be a significant burden, affecting both financial...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes


Ufisadi ni maovu au uharibifu wa Mali ya umma. Suala la ufisadi limegonga vyombo vya habari. Kila mmoja anajiuliza maswali chungu nzima. Si ajabu ufisadi hupatikana si shuleni, afisini na hata kanisani. Vyanzo vya umaskini wa nchi ni ufisadi . Viongozi wengi wamepora Mali ya umma na husababisha vilio, Hela ambazo zimetengewe elimu ya bure au katika ujenzi wa Barabara zimefunjwa. Si kila mtu a afurahia ukosefu wa maendeleo na pesa za umma zimeporwa mwishowe kuleta umaskini na kero nchini.

Nchini kenya Kuna kaunti arobaini na saba .kila Kaunti Ina viongozi mbalimbali wakiwemo magavana , wakilishi wa wodi na hatimaye mwakilishi wa wanawake . Kule mjini Busia Kuna kilio tele kuhusu wahudumu wa afya kukosa mshahara. Pia walimu wa mtaala wa umilisi hawajalipwa . Wengine wa walimu wa mtaala wa umilisi yaani “J.S.S. ” bado wameajiriwa kwa kandarasi .
Ikiwa kungalikuwa na Uongozi Bora na ujasiri. Bila shaka hawa walimu wangekuwa wameajiriwa tayari. Uongozi mbaya imefanya walimu Hawa kuwa maskini kwasababu bado hawataweza kusaidia familia zao vyema. Malipo Yao ni duni mno. Hata hivyo si jambo la kufurahisha wananchi.

Nafasi adimu ya kazi. Tukizungumzia nafasi adimu ni ukosefu wa kazi kwa vijana. Nchini kenya Kuna baadhi ya vijana wengi wamesomea lakini nafasi za kazi ni chache mno. Elimu ya nane nne nne ilikuwa na manufaa na changamoto pia. . Nchini kenya waajiri wengi wanahitaji ujuzi wa mwanafunzi kuwa na maarifa zaidi ya ubunifu. Ukosefu wa ajira imesababisha wizi Kijijini na usalama ukawa tishio zaidi.

Utangamano ni hali ya kuishi kama jamii moja. Tusiwe na ubaguzi wa rangi, ukabila , tukirejekea mrengo wa siasa. Katika utafiti wa hivi majuzi Kuna baadhi ya makabila ambazo Zina umaarufu zaidi katika kupewa nafasi za ajira. Ni matumani yangu siku moja kati ya makabila arobaini na saba. Kila kibali itahusishwa katika ajira za kazi.
Nchini kenya ni Bora kupanga uzazi vyema. Ni vibaya kujifungua watoto wengi ambao hautaweza kuwapatia mahitaji maalum. Nchini kenya idadi ya watu inayoupiku uwezo wa uchumi ni hatari.

Tatizo hutokea wakati wazazi wengi wamepata ugumu wa kusomesha watoto wao. Jukumu la mzazi ni kumwelimisha mwanawe na awe na afya Bora kila mara. Watoto Hawa hushindwa kujitegemea . Nchi itakuwa wa walevi wenye kunywa pombe usiku kucha.
Maandamano ni Ile Hali ya kupinga jambo ambalo halikuwafurahisha moyoni inaweza kuwa kisiasa au elimu . Wananchi wengi huandamana barabarani kwa amani . Si ajabu kuona , Kuna baadhi ya wananchi ambao huchukua fursa hii kuharibu reli au afisi za serikali wakivunja glasi. Kutokana na hasira hii ya ubomozi , serikali itagharamika zaidi kufanya marekebisho . Hii huleta umaskini nchini mwetu.

Baadhi ya wakenya wanapitia Hali ngumu ya maisha. Hii hutokana na Hali ya gharama ya maisha kuwa ngumu sana. Bidhaa zimekuwa Bei ghali , hata wengi hula mlo mmoja kila siku.
Ni jambo la kushangaza baada ya kenya kupata uhuru wao.bado Hali ya uchumi ni tatizo ambalo bado halijapata jawabu au suluhu bado .
Kuchukua mkopo bila kuwa na mpangilio dhabiti . Mbona binadamu hupenda kuwa na fahari au sifa. Kuna baadhi ya wakenya ambao waliomba mkopo kwenye benki ili kuwania kiti Cha siasa. Viongozi Hawa wanapopoteza na Huwa masikini.

Ni Bora wananchi kupewa elimu kuhusu mkopo. Ili kupunguza umaskini nchini ni Bora wananchi wazindua njia mbadala kufufua uchumi badala ya kutegemea serikali kwa kila jambo maishani mwao.huku wakijiuliza tutalipa ushuru vipi?
Teknolojia ni maarifa ya kisayanasi yaliyowekwa katika matumizi kama vile viwandani, kilimo, ufundi au mawasiliano. Katika nchi iliyoendelea zaidi.
Si Bora uchumi kuegemezwa kwenye kilimo kinachotegemea mvua isiyotabirika. Hii ni maana kuwa mvua ikikosekana bila shaka watu watakufa njaa. Ili kupunguza umaskini ni Bora kutambua na kujua mbinu mbalimbali za kiteknolojia za kuzalisha chakula tele nchini kenya.

Magonjwa ni adui ya maendeleo nchini. Ni vyema wananchi wawe na bima la matibabu almaarufu “N. H.F. ” si ajabu kusikia serikali haijawekeza zaidi katika kuwasaidia wagonjwa wa saratani. Ikiwa mgonjwa anazidiwa zaidi, familia utalazimika kuuza shamba ili kigharamia matibabu. Pesa ikiwa kidogo kulipa Bali, wazazi wanalazimika kufanya harambee ili kuokoa maisha .
unywaji wa pombe haramu pombe ni kinjwaji kinacholenya . Katika gatuzi la muranga unywaji wa pombe imekuwa ni kero. Badala ya wananchi kujihusisha katika ujenzi wa Taifa, wao kila wakati wanakunywa pombe, mwananchi ndiye hujenga nchi.pia yeye ndiye kwa mara nyingi hubomoa nchi. tusibomoe nchi kwa kuwa sisi ndisi tunahitaji ujenzi wa Taifa Bora yenya maendeleo kote nchini.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_img