4.5 C
London
Sunday, December 29, 2024
HomeCommunityMadhara Ya Vita Katika Jamii

Madhara Ya Vita Katika Jamii

Date:

Related stories

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities In the...

Challenges Facing the Kenya’s Current Socio-Political Landscape

Kenya's current socio-political landscape is shaped by a series...

A Global issue about Female Genital Mutilation

Female Genital Mutilation (FGM), also known as female circumcision,...

Faida Ya Kupanga Uzazi

Upangaji uzazi ni muhimu sana katika familia, inahusu wanandoa...

Shiquo wa HiStyle: Revolutionizing the Business World with Unbelievable Prizes

In today's rapidly changing business environment, few have managed...
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes

Hali ya majonzi ilitanda katika kaunti ya Tana River. Hii ni baada ya mapigano kuzuka baina ya jamii mbalimbali. Gavana wa Tana river na mbunge walikamatwa na maafisa wa DC, kuhusiana na vita vya kijamii. Godhana ni nini katika historia? Godhana ni tajiri wa ng’ombe wakati wa Rigvedic. Chakula Kikuu cha Waarya kilikuwa maziwa ya ng’ombe ambayo yalitumiwa kutengeneza sifa kwa ajili ya dhabihu.

Kaunti ya Tana River inajumuisha maeneo kadhaa ya misitu, vichaka na mapori ambayo ni maeneo madogo ya makazi. Misitu huteuliwa kama hifadhi ya kitaifa. Vita katika jamii huharibu familia na mara nyingi huvuruga maendeleo ya mfumo wa kijamii na kiuchumi wa mataifa. Madhara ya muda mrefu ya kimila na kisaikolojia, wakati wa vita kina mama huwa wanateseka zaidi.

Aliyekuwa Waziri wa ulinzi Kithure Kithiki alitangaza maeneo kumi na mbili katika kaunti ya Tana River, kuwa hatari na yenye matatizo, ikiwemo mji wa Bura ambako mapigano yalikuwa makali zaidi. Mkuu wa polisi nchini Kenya bwana Douglas Kanja aliwataka wakazi ili wasalimishe silaha zao na kuepusha kuongezeka kwa ghasia.

Ni bora kufahamu kuwa matatizo yalianza pale ambapo serikali ya kaunti ilipotoa ardhi, kwa ajili ya kuwahifadhi watu waliokimbia makazi yao kutokana na mafuriko, pembezoni mwa mto Tana, ambao ni mto mrefu zaidi nchini Kenya.

Mapigano kati ya jamii kusini mashariki mwa Kenya yalisababisha vifo vya takribani watu kumi na nane katika muda wa wiki mbili zilizopita, polisi wanaendelea kushika doria ili kudumisha usalama zaidi. Wafugaji wa eneo hilo waliandamana, wakisisitiza kwamba malisho yao yatakaliwa na waliohamishwa. Hali ya kutilia shaka mno Tana River ni kuwa wakazi hawataki kusalimisha silaha zao kwa maafisa wa polisi kama ilivyotangazwa na aliyekuwa waziri wa usalama kithure kindiki.

Ni uchungu mno kusikia kuwa Mohamad Chorasaid, alimpoteza kaka yake katika machafuko ya kijamii, wakazi hao walitoa wito kwa inspekta wa polisi kuwahamasisha maafisa wote wa polisi katika kituo cha polisi cha madogo. Mohamed chora alikiri kuwa ndugu yake alipigwa risasi kwa mara ya kwanza mkononi, lakini ilikuwa vigumu kumuokoa kwasababu alikimbilia usalama wake, huku wakiendelea kumpiga risasi mara kadhaa, maafisa wa usalama wanawakabili watu kwa kuwaua mchana peupe, Wakazi hawana imani na afisa anayesimamia kituo cha polisi cha Sweleh Chereru pia walilalamikia utovu wa usalama ambao umekita mzizi katika kaunti ya Tana River.

Maeneo ya Tana River imeshuhudia changamoto za ardhi hasa baada ya serikali kuhimiza wakazi kutoa eneo la Mororo ambalo hukumbwa na machafuko ya mara kwa mara na kuwapeleka karibu na barabara ya Junction Bura mtawalia, machafu Tana River yamesababisha kuchomwa kwa nyumba ishirini Katika maeneo ya Bula Vango na ardhi ya K.B.C. kunyakuliwa. Wakazi wa maeneo hayo sasa wanalaumu asasi za serikali za usalama katika kaunti ya Tana River.

Ni vyema kwa wananchi kujulisha vyombo vya usalama kuhusu matukio yanayoweza kuvuruga amani na kuhatarisha maisha, kulingana na inspekta wa polisi, ni vyema idara ya upelelezi wa makosa ya Jinai D.C.I. kufanya uchunguzi kuhusiana na ghasia zilizosababisha maafa. Wito wa jamii ni kuendelea kudumisha amani, mkuu wa polisi alisema hali ya usalama itaimarishwa huku maafisa wa kudumu watapelekwa, maafisa wa huduma ya Taifa ya polisi ( N.P.S.) maafisa wa vikosi vya ulinzi na wale wa upelelezi wa makosa ya Jinai walipelekwa katika maeneo ya Tana River ili kurejesha hali ya utulivu na amani.

Katibu wa wizara ya usalama wa nchini mheshimiwa Raymond Omollo alisema matumizi ya pombe na dawa za kulevya pia huchangia vijana kujihusisha na vitendo hivyo vya wizi, ulaghai, utekelezaji wa mali na wizi wa mabavu kila wakati.Watu wanne walifariki baada ya machafu kati ya jamii mbili kuzuka.

Watu hawa wameuawa katika maeneo ya Elnigha kaunti ndogo ya Bangale. Katika kaunti ya Tana River, Kutokana na machafuko haya ilimbidi Gavana wa Tana River kuandikisha taarifa, vitengo vya usalama Kanda ya pwani vimeimarisha juhudi za kurejesha hali ya utulivu katika kaunti ndogo za Bangale na Tana kaskazini, kaunti ya Tana River.

Akihutubia wanahabari katika afisi ya naibu kamishana wa kaunti ndogo ya Bangale, mratibu wa eneo la Pwani Rhoda Onyancha alisema kuwa maafisa wa usalama wamekita kambi katika maeneo yanayokumbwa na mzozo ili kudumisha usalama wa wakazi wa maeneo mbalimabali.

Onyancha aliwahimiza wazee wa jamii hilo kila mara kukabiliana na silaha haramu mikononi mwa raia, akionya kuwa zoezi la kutoa silaha haramu litatekeleza iwapo watu hawatasalimisha silaha haramu kwa hiari.

Ni bora wazee wa kijamii kushiriki mazungumzo wakati wa kutatua migogoro na iwapo watashindwa kupata suluhu, wawaalike wazee wa jamii nyingine kuhakikisha maswala yanatatuliwa na hayaenei zaidi.
Onyancha aliyekuwa ameandamana na kundi la maafisa wa usalama, alikiri kuwa nia yake ni kusitisha ghasia kati ya jamii mbili ambazo zimeishi pamoja kwa muda mrefu. Chanzo halisi cha mzozo huo ni kwamba kulikuwa mtafaruku katika kituo cha maji cha Anole, ambapo jamii moja ilihakikisha maswala yanatatuliwa na hayaenei zaidi.

Kamishana wa kaunti ya Tana River Omar Beja amehimiza viongozi wa kaunti hiyo kushirikiana na serikali kuu ili kutatua mizozo ya ardhi, wapate hati miliki zao za ardhi.
serikali kuu inapania kuwasaidia wenyeji kupata hati miliki za ardhi na kuwataka viongozi kupata mafunzo bora kutoka kwa kaunti za wafugaji na namna wametatua tatizo la ardhi .

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img