6.7 C
London
Thursday, December 12, 2024
HomeCommunityFaida Ya Kupanga Uzazi

Faida Ya Kupanga Uzazi

Date:

Related stories

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities In the...

Challenges Facing the Kenya’s Current Socio-Political Landscape

Kenya's current socio-political landscape is shaped by a series...

A Global issue about Female Genital Mutilation

Female Genital Mutilation (FGM), also known as female circumcision,...

Madhara Ya Vita Katika Jamii

Hali ya majonzi ilitanda katika kaunti ya Tana River....

Shiquo wa HiStyle: Revolutionizing the Business World with Unbelievable Prizes

In today's rapidly changing business environment, few have managed...
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes

Upangaji uzazi ni muhimu sana katika familia, inahusu wanandoa kupanga kuwa na udhabiti zaidi wa wakati watakapokuwa na watoto wao, inaweza kuwa nzuri kwasababu za kiafya, kiuchumi au kibinafsi. Iwapo wanandoa wana uwezo wa kudhibiti idadi ya watoto walio nao, nafasi kati yao kupunguza idadi ya watoto katika familia inamaanisha rasilimali zaidi kwa kila mtoto na wakati zaidi kwa wazazi kujitolea kwa kila mtoto.

Njia za upangaji wa uzazi imeleta tija katika familia nyingi. Mbali na umuhimu wake, bado kuna changamoto kubwa kwa vijana juu ya ufahamu wa elimu ya afya ya uzazi inayohatarisha mustakabali wa vijana wengi nchini kutokana na kuathirika kwa afya ya mwili na akili pale wanapopata afya bora, serikali kupitia wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsi wazee na watoto hushirikiana na wadau mbalimbali. Njia sahihi ya kuwawezesha vijana kufikia malengo yao ni kuambatanisha elimu ya uzazi wa mpango wa elimu ya mikopo na ujasiriamali kwa suala la changamoto za kiuchumi, limekuwa na mchango mkubwa na kupelekea ujauzito wa utotoni hususan kwa vijana wa kike, karibu njia zote zina madhara ambayo wanawake wanapaswa kuvumilia.

Ni vyema serikali kutilia mkazo elimu ya upangaji uzazi. Jambo hili bila shaka itasaidia wazazi kuwalea watoto wao kwa njia bora na yenye afya bora, watoto ni baraka lakini malezi ndio jambo la maana zaidi.

Makampuni ya dawa duniani kote pia huwekeza na kutafiti mbinu za kudhibiti uzazi, hasa kwa wanawake,mzigo wa kupanga Uzazi unabaki kwa wanawake pekee. Karibu katika nchi zote duniani, njia za kupanga uzazi hutumiwa hasa na wanawake, njia zote isipokuwa mbili za kupanga uzazi hutangazwa.

Asilimia sitini ya vijana hawatumi mbinu za kuzuia ujauzito kwa mujibu wa ripoti. Kenya inalenga kuhakikisha kuwa idadi ya akina mama wanaotumia mbinu za kisasa kupanga uzazi inaongezeka kutoka asilimia hamsini na nane hadi sitini na nne kufikia mwaka wa elfu mbili na ishirini na tano.

Huenda lengo la upangaji uzazi inaweza kukosa kufanikiwa iwapo serikali haitachukua hatua za haraka kukabili changamoto zinazosababisha akina mama kukumbatia mbinu za kiasili na upangaji uzazi.

Wanawake wanaweza kutotumia mbinu za kupanga uzazi kutokana na imani za kidini au wanaogopa matatizo mengine ya kiafya yanayosababishwa na mbinu hizo, lakini ukweli ni kwamba nusu ya akina mama wanaoenda katika vituo vya afya kusaka huduma za kupanga uzazi, hawaelimishwi kuhusu athari za pembeni, za sindano, tembe au vifaa wanavyowekewa.

Ni wazi kuwa katika kaunti za Pokot magharibi, Bungoma, siaya ,Nandi, kericho, Nyamira, Kiambu, Nairobi, Kitui na Kilifi ambapo ilibaunika kuwa asilimia arobaini na tatu ya akina mama wanaosaidiwa kupanga uzazi hawapewi elimu kuhusu matatizo yanayotokana na mbinu hizo za kuzuia ujauzito.

Baadhi ya madhara ya upangaji wa uzazi ni hedhi ambayo ilidumu kwa wiki mbili, chunusi zilizagaa usoni na maumivu ya kichwa, uchungu kwenye matiti, kichefuchefu, unene, kupindukia, kuzunguzungu na kubadilika kwa hisia.

Kila mbinu za upangaji wa uzazi ina faida na hasara zake. Kuna mambo mengi ya kuzingatia wakati wa kuchagua njia ya kupanga uzazi, kwa mfano ufanisi wake hutegemea gharama na jinsi ilivyo rahisi kutumia au hatua yako ya maisha.

Ikiwa haujui uzazi gani wa kutumia ona daktari wako, anaweza kukueleza faida na hasara za kila njia ili uweze kufanya uamuzi sahihi wako. Unahitaji agizo la daktari kwa aina fulani ya uzazi.

Uzazi wa mpango wa kudumu kwa wanawake, ingawa wataalamu wengi wa upangaji uzazi wa hiari hawako huenda usikue kamwe mara nyingi ni kwasababu ya mambo ambayo hatuna udhabiti juu yake, kuhama kwa idadi ya wanawake na wasichana wa umri wa kuzaa, dharura ya hali hewa, magonjwa yanaweza kutokea na kuathiri juhudi bora za wale wanaotoa uzazi wa mpango wa hiari, lakini watu wengi wakiitikia wito au huduma wanaamini kwamba hakuna ubaya katika kujitahidi kupata ukamilifu wa kuwa karibu iwezekanavyo.

Afya ya uzazi husaidia kila mara kujifunza na kuunda fursa za ushirikiano na kubadilishana ujuzi ndani ya upangaji uzazi na jumuiya ya afya ya uzazi.

Mambo muhimu katika kulenga mpango kamili wa upangaji uzazi ni wajibu wetu kuwa makini katika vipengele muhimu kwa mpango wa uzazi uliozinduliwa mwaka wa elfu mbili na kumi, ulionyesha ongezeko la asilimia kumi na mbili katika kiwango cha kisasa cha maambukizi ya njia za uzazi wa mpango miongoni mwa wanawake. Mafanikio ya programu yalichangiwa na ukweli kuwa ilishughulikiwa kwa wakati mmoja huduma.

Upangaji wa uzazi hivyo husaidia serikali katika kugawa rasilimali za kitaifa. Katika wakati wa historia ambapo ndoto za watu wengi zimetumia rangi na hofu ya janga la kimataifa labda inafaa kutumia muda juu ya ndoto nzuri badala ya ndoto mbaya, mahali pazuri pa kuanzia ni pamoja na vipengele kumi ya mafanikio ya uzazi wa mpango iliundwa zaidi ya miaka kumi iliyopita wakati huo ulikuwa. Ikiwa tutapanga uzazi basi familia itakuwa thabiti.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img