6.9 C
London
Sunday, December 22, 2024
HomeInternationalKENYATeknolojia ya ajabu Nakuru

Teknolojia ya ajabu Nakuru

Date:

Related stories

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities In the...

Challenges Facing the Kenya’s Current Socio-Political Landscape

Kenya's current socio-political landscape is shaped by a series...

A Global issue about Female Genital Mutilation

Female Genital Mutilation (FGM), also known as female circumcision,...

Faida Ya Kupanga Uzazi

Upangaji uzazi ni muhimu sana katika familia, inahusu wanandoa...

Madhara Ya Vita Katika Jamii

Hali ya majonzi ilitanda katika kaunti ya Tana River....
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Teknolojia ni maarifa ya sayansi yaliyowekwa katika matumizi au mitambo kama vile viwanda , kilimo na hata ufundi wa vyuma.

Riziki maishani
Maarifa ya teknolojia huwasaidia watu wengi kujipatia mapato katika jamii . Teknolojia huwa na hasara lakini kwa kiwango kikubwa huleta manufaa katika jamii.
Katika Gatuzi la Nakuru , mhandisi mmoja aliyeitwa Peter Kinyua , Aliye na miaka thelathini na Tisa aliwashangaza wengi kupitia uvumbuzi wa teknolojia mpya. Kinyua ni mzazi na ana watoto wawili anaishi mtaa wa mambili .

Ajira kwa Vijana
Kupitia ujuzi wake amewajiri vijana kumi na wawili katika maakazi yake. Kinyua ni mwana mziki na pia ana bidii ya mchwa. Kwa Mara nyingi binadamu hajafahamu umuhimu wa kufunza mazingira . Kila wakati baada ya kunywa maji au soda baridi , watu huamua kutupa chupa za plastiki na kuvitambua kuwa vitu visivyo na thamani yoyote.

Kupata Riziki
Mhandisi hitajika bwana kinyua, aliamua kutumia ujuzi wake kuvumbua mtambo wa kujipatia riziki . Vijana Hawa kumi na wawili walimsaidia zaidi kukusanya chupa za glasi na kuvigawanya katika sehemu ndogondogo , Kisha vikawa Kama unga wa sima . Juhudi zao zilifanikishwa kupitia kwa mashine ambayo iliwasaidia kukamilisha lengo lao kamili.

Kutengeneza “marbles” bano.
Nia kuu ya bwana kinyua ilikuwa kutunza mazingira. Baada ya kukusanya chupa za glasi . Ujuzi wake ulikuwa kupeleka katika mashine na kuvitumia chembe hizo kutengeneza vifaa mbalimbali.
Aliweza kutengeneza malighafi zinazotumiwa katika ujenzi . Moja wapo ni “marbles” ambazo kwa Mara nyingi hutumiwa na watoto katika shughuli zao wanapocheza.

Kutengeneza matofali
Kupitia machine hiyo aliweza kutengeneza matofali za kujenga nyumba. Jambo hili iliwatia wakaji moyo. Ilikuwa siku njema kwake kinyua , wakati wa kongamano la ugatuzi alipoeleza kuhusu ujuzi wake, hapo ndipo aliweza kukutana na na seneta wa Uasi Ngishu bwana Jackson Mandago pamoja na aliyekuwa waziri mkuu bwana Raila na kuwaelezea teknolojia ya ajabu.

Vifaa Kwa Kuingiza Hewa “ventilation”
Kwa Mara nyingi vijana humu nchini wanalia hakuna kazi lakini bwana Kinyua aliamua kujiajiri yeye mwenyewe kupitia teknolojia . Nyumbani kwetu, , Kuna sehemu ambazo huitwa “ventilation” .kupitia glasi hizi yeye hutengeneza vifaa ambazo zinaweza kuingiza hewa jikoni .sehemu hizi huachwa pia kutoa Moshi jikoni. Aliwahimiza vijana kufikiria zaidi kukuza talanta , kuliko kutegemea malipo bila jasho.

Kutengeneza Vifaa vya Jikoni
Ukistaajabu ya Musa, utaona ya firauni , kwa miaka nyingi , watu wengi walijua na kurembesha nyumbani kwao. Ni Jambo la kufurahisha wakati bwana Kinyua anatumia glasi hizi kutengeneza “kitchen tops” vifaa vya jikoni Kama vifuniko . matumaini yake ni kuwa teknolojia hii itasambazwa katika Kila Gatuzi.
Katika ujuzi huu aliweza kutengeneza “slab” hii ni mabamba ya jiwe ya vigae vya udongo mwekundu na Mara nyingi hufunikwa na chokaa.

Kutengeneza lami
Glasi hizi huweza kutangeneza lami halisi. Lami hii huwa nyeusi Kama makaa na hupatikana baranarani. Mahali ambapo Kuna mashimo mengi barabarani lami huziba shimo hizo. Kwa hivyo teknolojia hii imewasaidia wasafiri kurembesha Barabara na kupunguza ajali.

Baadhi ya chagamoto bwana Kinyua hupitia

Ukosefu wa Ajira
Bali na kuvumbua teknolojia hii Nakuru , bwana Kinyua alikiri kuwa na matatizo chungu mzima .na idadi ya “chokoraa” ilikuwa 440 mwaka wa 2019. Ukosefu wa gari la kubebea malighafi . Yeye hutumia tukutuku ambayo hubeba mzigo kidogo mno. Ombi lake ni kuwa serikali ya gatuzi la Nakuru ni vyema kumpiga jeti katika shughuli zake za Kila siku.

Ukosefu wa Mashine.
Mashine ambayo Kinyua hutumia ni kidogo zaidi . Kazi yake huchukua muda mrefu kukamilika. Jambo hili limempatia kiwewe, hata hivyo watu wakichangamkia ujuzi wake, kwa mapana na marefu. ana ndoto ya kununua mashine kubwa yenye uwezo wa kufanya kazi kwa haraka na kujipatia faidi nyingi.

Ukosefu wa Nafasi
Gatuzi la Nakuru Ina machupa ya plastiki nyingi Sana. Kwake Kinyua kupata bidhaa hizi ni rahisi, tatizo lake kubwa ni ukosefu wa nafasi ya kuhifadhi chupa hizi. Anatumia marafiki zake kukusanya chupa Mia mbili kwa siku , sehemu ambapo yeye hufanyia kazi ni ndogo mno. Juhudi zake ni kutia bidii ya mchwa ili siku moja apate kiwanja Cha kuhudumia wananchi wote.

Kurahisisha Kazi
Teknolojia imerahisisha kazi huko ofisini. Wakati wa zamani , wafanyikazi walikuwa wanatumia makaa kuandika na wakati wa upasuaji watu walifariki , Heko kwa teknolojia ya kisasa kupunguza idadi ya vifo.
Ni matumaini yangu kuwa jamii na serikali itampiga jeki bwana kinyua katika juhudi zake za teknolojia ya ajabu. Gatuzi la Nakuru itakuwa na manufa tele. Tuchangamkia teknolojia na kubadilisha maisha yetu katika jamii. Mabadiliko ni kitu ambacho hudumu milele.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img