Chanjo zinaweza kulinda mtoto dhidi ya kupata magonjwa hatari ambayo yanaweza kumdhuru au kumuua mtoto au mtu mzima. Chanjo hupunguza uwezekano kwamba mtoto wako ataeneza Ugonjwa. Chanjo ni muhimu kwa kila mtu na zinaweza kukulinda kutokana na magonjwa hatari. Pia ili utume maombi ya kadi ya kijani na uraia wako. Chanjo husaidia kufundisha mtu mfumo wa kujikinga dhidi ya vidudu.
Watoto hukabiliana na maelfu ya vidudu mwilini kila wakati. Chanjo husaidia kukinga maradhi, ulemavu na vifo vitokanavyo na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ikiwemo surua, homa ya ini. Kisayansi chanjo ni kitendo cha kupewa Kinga mwili kwa njia ya kuamsha vitoa Kinga viwe tayari kupambana na adui ambaye wanamjua tayari. Watoto waliopata chanjo huwa wamekingwa dhidi ya magonjwa hatari ambayo kwa kawaida huweza kusababisha mwili kuwa dhaifu. Watoto wana haki kupata chanjo.
Kinga ya utotoni ni muhimu sana hasa kwa ukuaji wa baadaye. Hivyo basi chanjo kwa mtoto, katika mwaka wake wa kwanza na mwaka wa pili ni muhimu sana. Kina mama wajawazito ni bora wao kupata chanjo ya pepopunda ili kujikinga wao wenyewe na watoto wao waliozaliwa. Wazazi wa walezi wengine wanapaswa kufahamu sababu chanjo ni muhimu. Ratiba ya chanjo inayotumika na mahali pa chanjo hutangazwa kupitia vyomba vya habari. Familia inafaa kujua chanjo ambazo wizara ya afya imependekeza. Wazazi wote au walezi wanapaswa kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya kuhusu muda wa kukamilisha chanjo zinazohitajika.
Chanjo hutokea katika maisha ya watoto kila mwaka. Watoto wakipata chanjo zote wao wanajikinga dhidi ya magonjwa hatari maishani wote. Kina mama wajawazito wote wanafaa kijikinga dhidi ya chanjo ya pepopunda kikamilifu. Hata kama mama aliwahi kupata chanjo hii kabla, anapaswa kupata ushauri wa mtaamu wa afya kuhusu kama bado anahitaji kupewa chanjo bado. Sindano mpya hazina budi kutumika kwa kila chanjo anayopewa Ugonjwa huweza huenea haraka watu wengi wanapokusanyika pamoja. Watoto wote wanaoishi katika maeneo yenye mkusanyiko mkubwa, hasa katika mazingira ya wakimbizi au ya watu waliojikusanya kutokana na janga fulani.Wanapaswa kupewa chanjo haraka, Ishara zinazoelekeza kuwa mtoto anaweza kuwa anaugua surua ni pamoja na kuongezeka kwa joto mwilini, upele mwingi na kikohozi kupitia kiasi.
Kumwaga kamasi na macho hubadilika na kuwa mwekundu. Tahadhari mtoto anaweza kufa kutokana surua. Watoto wote wanastahili kupata chanjo dhidi ya polio. Dalili za polio ni upele kwenye mguu au mikono na udhaifu wa kutumia kiungo kilicho athirika. Kwa kila mtoto mia mbili wanaoambukizwa maradhi ya polio mmoja atapata ulemavu wa maisha. Ratiba ya chanjo hutofautiana kulingana na nchi au sehemu ya nchi unayoishi. Ni muhimu kufuatilia ratiba ya chanjo kwa mujibu wa mwongozo wa taifa. Watoto wanastahili kupokea chanjo kwa umri unastahili kuwa na mpangilio. Kadi ya mtoto inafaa kuwasilishwa kwa mtoa chanjo kabla ya chanjo kutolewa rasmi.
Kifaduro huathiri njia ya kuingizia hewa na kusababisha kikohozi kinachoweza dumu wiki nne hadi nane na ni hatari sana kwa watoto wachanga. Wanawake wote wajawazito na watoto wachanga wanahitaji chonjo. Viini vya dondakuu mara kwa mara husababisha maambukizi ya njia ya kuingizia hewa na huenda ikasababisha shida za kupumua na hata kifo kwa watoto.
Watoto wote wanastahili kupokea chanjo ituayo Bacile Calmette Guerin vaccine. Hii huumpa mtoto Kinga dhidi ya aina zingine za kifua kikuu na ukoma. Wataalamu wa afya ni muhimu kutambua chanjo na kuzingatia jinsi ya kuwapatia watoto, mtoto anafaa kumalisha chanjo yake ili kuboresha afya kila wakati. Kila msichana na mvulana anapaswa kupata chanjo kamili. Kinga utotoni ni muhimu sana.
Watoto milioni moja nukta sita waathiriwa na uhaba wa chanjo. Nchi ilikosa kusambaza chanjo kwa mwaka mzima baada ya kushindwa kulipa deni la zaidi, dola za Marekani milioni kumi na tano, ambazo ni sawa na shilingi billioni mbili kwa muuzaji wa kitaifa, wizira ya afya imekiri kuwapo uhaba wa kitaifa wa chanjo, ila inahitaji kusamba chanjo kwa haraka. Kwa upande wake wizara ya afya ya Kenya, katika taarifa yake iliyotiwa saini na katibu wa afya inasema mikakati ipo ya kukabiliana na uhaba wa chanjo nchini Kenya.
Tahadhari imetolewa wakati ambapo dunia inakabiliwa na uhaba wa chanjo. Kupata taarifa, shirika hilo limeeleza kuwepo kwa ongezeko la wagonjwa wa Kipindupindu. Ugonjwa wa Kipindupindu husababisha mtu kuhara au hata kutapika na kusababisha upungufu wa maji mwilini wakati mwingine hata kifo iwapo mgonjwa hatatibiwa haraka. Ilikuwa furaha kwa wakenya baada ya wizara ya afya kutangaza kuwa imepokea chanjo, kwa hiyo watoto wote wafaa kupelekwa ili wapate chanjo. Afya ni bora kuliko mali kila siku.