16.3 C
London
Monday, June 24, 2024
HomeCommunityUGONJWA WA UKIMWI

UGONJWA WA UKIMWI

Date:

Related stories

Empowering Kenyan Women, How Female Entrepreneurs are Driving Economic and Social Change.

In the vibrant entrepreneurial landscape of Kenya, a remarkable...

Bridging the Divide, Kenyan Youth Transcend Ethnic Boundaries.

In a country as diverse as Kenya, where over...

Burden of Excess, The Detrimental Impact of Over taxation on Citizens.

As governments around the world grapple with the ever-increasing...

Guardians of the Land, Kenya’s Resilient Pastoralist Communities.

Across the vast, rugged landscapes of Kenya, a rich...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Iwapo utakuna na vijana mtaani wakitambea huku na kule , utashangaa wanawaza Nini. Mara nyingi wanajiuliza kuhusu janga la Ukimwi. Si ajabu kisikia wanachoogopa zaidi ni Ugonjwa huu . Wengine husema Ukimwi si Ugonjwa wa kawaidia , wanadai hutokana na ushirikina au uchawi.
Je, Ukimwi ni nini, Kuna wale ambao wameugua Ugonjwa huu? Na je, Ugonjwa wa Ukimwi huambukizwa kwa njia zipi kule mtaani au mjini. Ukimwi ni ukosefu wa Kinga ya mwili unaompata mtu aliyeambukizwa virusi ambazo, husababisha mtu kuishi kwa na maradhi mbalimbali . vijana kwa wazee wanaweza kupatwa na Ukimwi . Ni bora kutahadhari kabla ya hatari.

Hata hivyo ni wazi kuwa Ugonjwa huu husambazwa kwa njia mbalimbali . Kama vile kujuana kimwili na mtu aliye na virusi . Inafahamika vyema maambukizi yaliyo katika mstari wa mbele ni kutokana na mapenzi ya kiholela . Vijana wengi hujihususha katika ngono kabla ya
kupata jiko. Hata wanandoa hufanya mapenzi ya kiholela. Jambo hili huchangia maambukizi.
Kutiwa damu iliyo na virusi vya Ukimwi . Majeruhi ajalini wanaovuja damu wanaweza kuambukizana . Madaktari na wauguzi wasipotumia vifaa safi wanaweza kueneza maambukizi. Ni bora tusisahau waganga na wagaanguzi wawachanjao wateja wao kwa kutumia wembe kuukuu zilizotumika mara kadha wa kadha.

Kudungwa sindano kiholela . Kuna njia nyingine ingawa ni nadra mno. Daktari au muuguzi kwa bahati mbaya aweze kujidunga kwa sindano aliyomdungia mwathiriwa . Waathiriwa walioathiriwa hulaumiwa kwa makosa yasiyo Yao. Ni vyema daktari kuwa makini zaidi wakati anahudumia mgonjwa wake.
Kutumia nyembe pamoja. Hali kadhalika maghulamu wanaweza kuambukizwa wanapopashwa tohara na ngariba. Jambo hili hutokea kisu kimoja kikitumiwa kwa wateja wengi. Iwapo mmoja wao ana virusi bila shaka Kuna uwezekano wa maambukizi mkubwa . Katika tamaduni nyingi kupasha tohara ni jambo la kawaidia . Idadi kubwa ya jamii bonde la ufa na hata magharibi hupenda kupasha tohara . Ni ajabu hivi majuzi vijana wengi wameripotiwa kuaga Dunia.

Kutoka kwa mzazi hadi kwa mtoto anayezaliwa . Ikumbukwe kuwa kunao wanaoambukizwa bila hiari. Kundi hili husahaulika na wengine wanaposhutumiwa wao pia huathiriwa na kutwezwa huko. Baadhi Yao hujichukia kiasi Cha kujitia kitanzi huku wengine wakijisononekea hadi kaburini. Kundi hili linajumlisha vimalaika . Wanaoambukizwa wakiwa bado tumboni mwa mama zao na wanaobakwa . Katika shughuli zetu zote na kuwaona kuwa ndugu. Tunapofanya hivyo jamii yote itatangamana kama familia moja.

Ukimwi umewateka nyara vijana, sasa hivi wamekosa la kufanya. Asilimia sitini na tano Wana Ukimwi. Vijana wengi hawana ajira. Ni bora serikali kutangeneza ajira katika sekta kama udaktari , walimu na wakili . Wakifanya hivyo vijana watakuwa na kazi ili kukosa nafasi ya mapenzi ya kiholela.
Epukana na mapenzi ya kujuana kimwili.mapenzi Bora ni ya wale ambao wamefunga ndoa kihalali . Tukifanya hivyo familia itaishi kwa furaha na amani.
Usipewe au kukata ngozi yako kwa vifaa vilivyotumiwa na wengine. Kila mtu awe makini zaidi. Wakati madaktari wanapasha tohara. Vifaa vya matumizi viwe mpya . Tusitumia kifaa moja kwa kila mtu. Kila kijana apashwe tohara kwenye hospitali siyo nyumbani.

Wale ambao wameambukizwa Ukimwi wasife moyo. Ni bora watambua namna ya kuishi baada ya kuambukizwa. Siri ni kugundua na kupongeza wanasayansi kwa kupunguza makali ya virusi vyenyewe. Tiba ya uele huu haijapatikana , usipewe damu ambayo haijakaguliwa vyema kama inavyostahili . Katika ndoa ni vyema kuwa mwaminifu kwa mke au mume wako. Baadhi ya wanaojinyonga kutokana na maradhi hushirikishwa na kulaumiwi kuwa wao ni katili , watu wasio na utu.
Uvumi unaposambazwa au inapobainika bayana kuwa binadamu ameambukizwa wengi. Wengine husema kuwa ukimwa si kweli , idadi ya walioambukizwa ni kubwa mno. Haifai kuwatenga wale waliougua Ukimwi. Virusi vya Ukimwi , vinapunguza uwezo wa mwili wa mgonjwa kupigana na vidudu vya maambukizi. Swala linalowafanya wagonjwa Hawa kutodhibiti maambukizi ya magonjwa mbalimbali. Katika Hali ya kawaida , mwili wa mtu kama huyo unaweza kujikinga dhidi ya viini kama hivyo.

Maambukizi haya kawaida hujitokeza pindi kukiwa na nafasi duni ya Kinga mwilini. Ni asilimia hamsini hadi sitini ya wagonjwa wa kifua kikuu nchini kenya wameambukizwa Ukimwi. Mmoja kati ya watu wawili au watu wenye virusi vya Ukimwi hupata kifua kikuu.
Baada ya kufahamu jinsi Ugonjwa wa Ukimwi huambukizwa. Ni bora kila mtu kufahamu suluhu.hakuna jambo ambalo halikosi suluhisho ya kudumu. Kinga ni Bora kuliko tiba. Kwa wale ambao wamehasiriwa ni Bora tubadilishe mtazamo wetu. Tuwapende na kuwajali mno . Waziri wa afya Susan Nahumicha anatia bidii kuboresha sekta ya afya nchini kenya kila mara.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_img

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here