10.8 C
London
Saturday, May 11, 2024
HomeInternationalKENYAMLIPUKO WA GESI EMBAKASI

MLIPUKO WA GESI EMBAKASI

Date:

Related stories

Road to Wembley: A Tale of Triumph and Turmoil in the 2023/2024 Champions League

The 2023/2024 UEFA Champions League has been a spectacular...

The Harmonious Tapestry; Exploring the Interplay of Music and Identity

Music, the universal language that transcends borders and unites...

Achieving Your Fitness Goals; The Essential Guide to Effective Training

Fitness and training are integral components of a healthy...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes


Mlipuko ni kitendo au tukio la kulipuka , upanuzi wa vurugu au kupasuka kwa kitu kwa wakati wa ajali , kwa baruti au “boiler” . Mlipuko husababishwa na upanuzi wa haraka wa gesi kutoka kwa athari za kemikali au vya kuwasha.
Ni Bora kufahamu kuwa dalili za mlipuko zinaweza kuwa na kelele kubwa sana au mfulilizo wa kelele na mitetemeko , moto, joto au Moshi , glasi inayoanguka au uchafu au uharibifu wa jengo. Mlipuko wa kawaida ya kemikali ni Ile inayosababishwa na uchomaji wa mafuta ya hidrokaboni inayoweza kuwaka . Hii ni mlipuko ya mwaka na Ina sifa ya uwepo wa mafuta yenye hewa kama kioksindikaji. Mlipuko wa mwaka pia huhusisha vumbi wakati kitu kuchomwa.

Mwaka ulipoanza kila mmoja alikuwa na ndoto ya mafanikio. Wengine walikuwa na ndoto ya urubani , hata hivyo mlipuko wa gesi katika eneo la mradi , kaunti ya Nairobi , ilizima ndoto ya wakenya wengi , vifo, hasara na majonzi ilitawala kwenye vinywa vyao wengi wakitazama wapendwa wao wakiaga Dunia ana kwa ana . mlipuko wa gesi mji mkuu wa Nairobi Kenya ilisababisha vifo vya watu tatu mwanzoni na kujeruhi watu mia tatu mtawalia .
si ajabu kusikia mlipuko mkubwa ikitokea . Ni Bora kufahamu kuwa kulikuwa uharibifu wa Hali ya juu katika eneo ya mlipuko wa gesi uliotokea ghafla watu wengi wakijeruhiwa hata watoto wachanga walifariki Dunia kighafla bila kupata fahamu.

Moto si kitu Cha kufanyia mzaha . Mlipuko wa gesi katika eneo ya mradi ilisababishwa na Lori lililokuwa limebeba mitungi ya gesi , ambalo lililipuka katika eneo ya embakasi mwendo wa saa moja na nusu . Kisha kulikuwa na moto mkubwa sana katika maeneo hayo. Moto huo ulitokea alhamisi usiku wa manane ambapo iligharimu maisha ya watu wengi kujeruhiwa , bila wao kupata fahamu.

Mlipuko ilisababisha uharibifu wa magari kadhaa na Mali za biashara ikiwemo biashara ndogo ya ” mama mboga” ziliteketea na kuwa majivu. Serikali ya kenya Kwanza bila shaka walikariri kuwa watasaidia katika shughuli za wapatia fidia waathiriwa Hawa .
Isitoshe walisema watafanya uchunguzi ili kubaini chanzo Cha mkasa huo. Kutokana na maafa haya , wakazi wa eneo la mradi maeneao ya mashariki mwa Nairobi walielezea jinsi walivyoshuhudia matukio ya kutisha jinsi chuma ilivyoruka ikiwa pamoja na mitungi ya gesi kulipuka kwa Kasi mno na kuathiri uchukuzi.

Si ajabu kufahamu kuwa mamlaka ya kuthibiti kawi kenya, almaarufu “EPRA” mwanzoni ilikataa kutoa kibali Cha ujenzi wa kiwanda Cha gesi kule Embakasi.kiwanda Cha kuthibiti kawi nchini kenya inasema , ilipokea ombi la ujenzi wa kiwanda hicho tarehe kumi na Tisa mechi mwaka wa elfu mbili ishirini na tatu, lakini maombi haya yote yalikataliwa baada ya kuomba leseni na kushindwa kutimiza usalama wa wakazi wa miradi.
Waathiriwa wanadai kuwa Lori lilivuja kwa muda wa saa moja . Kisha likasababisha janga la mlipuko . Wachungaji walimiminika katika eneo la mkasa ili kubainisha ukweli wa mkasa.

Jackline karimi alipata majeraha ya moto kwenye mkono wake wa kulia hadi mabegani na mguu wake wa kulia .Ifahamike kuwa jackine alimwona mwanamke mmoja akiwaka moto , lakini hangeweza kumsaidia, kila mtu alikuwa akikimbilia usalama wake.
Mlinzi wa jengo Hilo kule embakasi , alichukua jukumu la kugongea watu mlango kwa hasira na kuwaamuru wakazi watoke nje . Mlinzi huyu wa kibinafsi na utu na alipenda kazi yake kwa udi na uvumba. Serikali ilituma timu za kukabiliana na Mikasa ili kusaidia juhudi za timu za msalaba mwekundu na st John ambulance.

Rais William Ruto alihusisha kisa Cha mlipuko wa kisa Cha gesi kama ufisadi , ukosefu wa uadilifu na uroho wa maafisa wa serikali waliohusika kumpatia mhudumu leseni kuendesha biashara hiyo haramu.
Mbunge wa embakasi Babu owino pamoja na kiongozi wa upinzani Raila odinga waliwatembelea waathiriwa hospitalini ili kuwafajiri . Raila alisema kuwa ni Bora serikali kuwapatia makazi katika nyumba za Bei nafuu . Pia mamlaka ya kitaifa ya kusimamia mazingira ( NEMA) imewataka maafisa wanne wajiuzulu kutokana na maafa iliyotokea kule embakasi.

Walionusurika katika mkasa huo wa embakasi wangali wanahangaika na hawana mbele wa nyuma huku wakitafuta usaidizi kutoka kwa marafiki, na waafadili wema. Baadhi ya wanafunzi bado wamesalia nyumbani.
Mbunge wa embakasi mheshimiwa Babu owino anasema huu ndio wakati mwafaka kwa mahasla kufurahia nyumba za Bei nafuu chini ya mpango kabambe wa Rais William Ruto . Mshukiwa wa mlipuko wa gesi Nairobi alipandishwa kizimbani ili kujibu mashtaka.
Ni ombi langu kuwa serikali itawafidia waathiriwa wote wa mkasa wa gesi. Heko kwa mheshimiwa Babu Owino kuwapatia waathiriwa elfu arobaini na Tano ili waendeleze maisha Yao ya baadaye.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_img

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here