19.2 C
London
Friday, May 17, 2024
HomeHealthBima Ya Taifa

Bima Ya Taifa

Date:

Related stories

Why women struggle to take climate cases to court and how to correct it

By Pedi Obani A study in Nigeria and South Africa...

Calling off UN regional climate weeks exposes rich nations’ lack of goodwill

Funding these essential meetings would cost little to rich...

Don’t gaslight Africa: We need genuinely clean cooking solutions

The IEA summit, where oil and gas execs are...

Kenya: Adding up the costs of the floods amid an economic crisis

The devastation from the floods in Kenya have been...

Can We Use ChatGPT for Global Goods Software Development?

At IntraHealth, where our mission is to support health workers...
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes

Bima hulenga kumkinga mwananchi au mwanachama dhidi ya janga lisilotarajiwa kwa mfano kinga juu ya ajali ,kulazwa hospitalini ,moto, mafuriko wizi na kadhalika. Mara nyingi matokeo haya yasipokigwa hurudisha nyuma maendeleo ya mtu au familia nzima.

Bima ya afya ni mpango wa kifedha unaowezesha watu kulipia gharama za huduma ya afya wanapougua , kuwa na majeraha au wanapokuwa na mahitaji mengine ya afya .Bima hii ya afya imetengwa ili kutoa ulinzi wa kifedha na msaada kwa gharama zinazohusiana na huduma ya afya ikiwa ni pamoja na kutembelea daktari au kulazwa hospitalini.

Ili bima ya afya iweze kuwa hai na kutoa huduma kwa ubora basi wachanjiaji hutakiwa kuwa wengi kuliko watumiaji wa huduma. Bima ya afya inaweza kuwa si lazima bali kwa hiari. Dhima ya bima afya ilipata umaarufu zaidi baada ya vita vya pili vya dunia, wakati nchi nyingi zilianzisha mifumo ya ustawi wa jamii na huduma za afya za bure au manufaa kwa raia wao.

Mchangiaji hutoa kiasi cha pesa wakati akiwa mzima wa afya, kwa awamu ya kipindi ambacho atapata shida ya afya. Na hivyo kupunguza uwezekano wa kutumia pesa ya mfukoni. Ni vyema kufahamu kuwa Bima ya afya ilianza katika Karne ya kumi na tisa.Kama njia ya kuwalinda wafanyikazi dhidi ya ajali na magonjwa kazini.Baadaye ,bima ya afya ilienea katika nchi nyingine kama Australia au nchi za Asia na Afrika.

Lengo kuu ya bima ni kumrejeshea mwanachama hali ya afya ,kipato cha maisha na ustawi pindi anapopatwa na janga au anapopoteza kitu chake cha thamani hasa ikiwa amelipia michango ya marejesho.Kiasi Cha mchango hutegemea mambo mbalimbali kama jinsia, umri , hali ya afya ,aina ya bima na faida zinazotolewa .Bima humsaidia mhusika kufanya yafuatayo pindi anapikumbwa na matatizo. Kuna bima ya kulipia mtu anapolazwa na mgonjwa yasiyo ya kulazwa ,kulipia gharama za vipimo tu na bima inayomlipia mgonjwa pesa taslimu.

Vijana wote wanahitaji bima ya afya kama Wana afya .Bima muhumu zaidi kwa watu wazimu ni bima ya ulemavu wa muda mrefu.Hii ni kwasababu unaposafiri barabarani ajali inaweza kutokea. Kwa hivyo bima hii itakusaidia.Bima ya gari ni muhimu sana ina faida chungu nzima inakulinda, inalinda abiria wako, na inakuokoa kutokana na dhima za kisheria endapo gari lingine litagongwa na gari lako.Kwa mfano ikiwa gari la “Easy Coach” ambalo lilihusika katika ajali kule Mamboleo, kama ulichukua bima hii, bila shaka watafaifaidi chungu nzima.

Mwezi wa nne imekumbwa na ajali chungu nzima, ni bora kwa wananchi kuchukua bima haraka.Bima tatu kuu ya maisha ni kama vile Bima ya maisha ya muda, bima ya maisha yote na bima ya kudumu.Rais William Ruto alipitisha bima mpya ya afya kuwa Sheria oktoba mwaka wa elfu mbili ishirini na tatu.

Rais William Ruto anadai kuwa ni lazima wakenya wote walio na umri wa zaidi ya Miaka kumi lazima wajisajili , kwa hazina ya bima ya afya ya jamii(SHIF) waziri wa afya Susan Nahumicha tayari ametangaza Sheria hiyo kwenye gazeti la serikali.Kila mkenya anahitajika kuonyesha uthibitisho wa uanachama ili kupata hudumu za Serikali.

Bima inakuza ukuaji wa uchumi nchini.Bima humwezesha kupunguza hasara, utumizi wa kifedha na kukuza shughuli za biashara.Matokeao ya biashara hiyo mara nyingi husaidia kwa ukuaji wa uchumi na maendeleo,kwa hivyo bima Ina jukumu muhimu katika ukuaji endelevu wa uchumi.Kifurushi Cha manufaa kinajumuisha , kukaa hospitalini kwa uchunguzi wa huduma ya afya , utaratibu na matibabu ikijumuisha ushauri na ada za daktari , gharama za kitanda, huduma ya uuguzi , uchunguzi wa maabara na radiolijia , dawa zililzoagizwa pamoja na mavazi husika.

Ni bora serikali kuboresha mfumo ya huduma na bidhaa za bima kwa wateja kidijitali na kuhakikisha upatikanaji wa huduma hizo wanazozipata kirahisi kwa wakati.Wakenya wengi wanateseka zaidi , hii ni baada ya madaktari kugoma.Kuna baadhi hospitali za kibinafsi ambazo hazikubali kadi za N.H.I.F wao wanadai kuwa kadi hizi hazijalipwa .

Wagonjwa wa saratani wanapitia hali ngumu ya maisha . Gharama ya matibabu yao ni ya juu na kadi ya N.H.l .F. haiwezi kulipia gharama hii.Mara nyingi wao hulazimika kuchukua mkopo au harambee . Matumani yao ni kuwa ujio wa “SHIF” itashughulikia matibabu yao kwa mapana na marefu.Hata hivyo waziri wa afya Susan Nahumicha yuko mbioni kupigia upato kadi hii .

Je, unadhani Sheria hizi za N.H.I.F. zinamfaidi mwananchi wa kawaida au unadhani walengwa hasa ni kina nani ? Iwapo mtu alichelewa kulipa kadi hii alitozwa asilimia hamsini ya kiwango kulipa kila mwezi na yule atakayekosa kulipa kwa muda wa mwaka mmoja, pia atalazimika kuanza kulipa upya .Kadi hii ya N.H.I.F pia ilikuwa na masaibu mengi kama vile walio katika ndoa hawaruhusiwi kuadhikisha mke wa pili na iwapo utakuwa na mke mmoja na Watoto zaidi . Natumai suluhisho itapatikana kwa kadi hii mpya ,wakenya wakijitayarisha kujisajili upya ili wapate matibabu.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_img

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here