8.8 C
London
Monday, December 30, 2024
HomeKENYAKenyan EducationCHANGAMOTO ZA ELIMU MJINI LAMU NA JINSI YA KUBORESHA ELIMU.(SWAHILI)

CHANGAMOTO ZA ELIMU MJINI LAMU NA JINSI YA KUBORESHA ELIMU.(SWAHILI)

Date:

Related stories

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities In the...

Challenges Facing the Kenya’s Current Socio-Political Landscape

Kenya's current socio-political landscape is shaped by a series...

A Global issue about Female Genital Mutilation

Female Genital Mutilation (FGM), also known as female circumcision,...

Faida Ya Kupanga Uzazi

Upangaji uzazi ni muhimu sana katika familia, inahusu wanandoa...

Madhara Ya Vita Katika Jamii

Hali ya majonzi ilitanda katika kaunti ya Tana River....
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Elimu ni ngao ya maisha katika kitongoji Cha lamu. Matatizo ni hali ngumu ya maisha katika sekta ya elimu. Baadhi ya matatizo yanayoikumba elimu lamu ni Kama ifuatavyo:
Umbali wa shule . Katika mji wa lamu shule nyingi hupatikana katika maakazi duni zaidi, Barabara ni changamoto, hata wazazi wanahofia kuwapeleka watoto wao shuleni. Magaidi wa alshabab wamewatia uoga walimu Kisha wakatorokea makwao. Shule Kama katsaka kairu, mande na kiwayu hazina madarasa. Chaluma alisikitika zaidi wakati wa hatamu ya waziri wa elimu mwendazake bwana magoha.

Ukosefu wa walimu . Walimu ndio nahodha katika elimu . Shule ya boni Haina walimu na pia miondo misingi . Katika ripoti ya bwana kalume kazungu ameelezea Jambo hili kwa mapana na marefu .

Tishio la usalama .ukosefu wa usalama imewafanya wazazi kuhamisha watoto wao katika shule zingine Bora zaidi . Mwenyekiti wa shirika la “kepsha” mjini lamu, bwana josesph Agutu alikiri, dhahiri shairi, kuwa wanafunzi wengi wanaogopa kwenda shuleni. Hii ni kwasababu ya ukosefu wa usalama wao dhabiti . Huenda hawataki kupoteza maisha .
Janga la mafuriko, idadi ya wanafunzi mia sita wamelazimika kutoenda shuleni. Wakati wa mvua ya masika inaponyesha, mafuriko huwatia tumbo joto wakose amani. Katika sehemu ya makowe shule nyingi zimefungwa Hadi hali ya kawaidi irejelewe katika mtaa wa mokowe.

Mimba za mapema. Katika shule ya Hardy hit Hindi , wasichana sita walipachikwa uja uzito . Wazazi wao walikerwa Sana. Ajabu ni kwamba hawataendelea na masomo. Hamu ya masomo itakatizwa na majukumu ya kulea uja uzito. Suluhisho Bora zaidi ni kusalia nyumbani Hadi wakati watakapojifungua . Jinsi ya kike imedunishwa kwa kukosa elimu na nasaha Bora.

Matokeo duni katika mtihani wa kitaifa. Walimu wakuu wanajutia hali hii. Wanafunzi wengi hupuuza Sheria za shule , wengine hawana maadili Bora, kinachosalia ni mgogoro Kati ya walimu na wanafunzi . Tabia hizi zote zimechangia matokea duni katika kaunti ya lamu.

Ukosefu wa madarasa. Ni Jambo la kutia aibu zaidi . Serikali imekosa kujenga majilisi pamoja na maabara. Shule ya boraimani imekosa majilisi. Walimu wamelazimika kusomea chini ya mti. Mazingira Bora huchangia matokeo mazuri, hata hivyo walimu Hawa hawawezi kutimiza malengo yao kikamilifu.

Dawa za kulevya. wanafunzi wengi wanabugia zaidi dawa za kulevya . Ajabu ni kwamba wazazi wao hawana sauti. Jukumu la ulezi imewachiwa walimu shuleni. Baadhi ya wazazi lamu mashariki wametekeleza wajibu wao Kama wazazi . Hii ni ishara tosha kuwa watoto Hawa Uhuru zaidi kupita mipaka na kubugia dawa hizi. Walimu pia wamedharauliwa na wanafunzi, kwasababu , walimu wengi si waaji wa lamu , wametoka sehemu mbalimbali za nchi.

Umasikini . wanafunzi wengi wanapenda masomo mjini lamu, lakini ukosefu wa chakula imewafanya kuchukia kwenda shuleni . Mara nyingi wanajuta kuwa watakula Nini? Jambo hili limewakoseha amani na kusitisha masomo. Kule lamu mashariki shule ya faza kizingiti peke ndiyo Ina maabara. Mwalimu wa biolojia bwana moris, anasema ni ndoto mwanafunzi kupita mtihani, ikiwa Hana ufahamu kuhusu maabara na vifaa Kama “spatula”.
Baada ya kufahamu changamoto hizi, yafuatayo ni suluhisho. Mkurugenzi wa elimu lamu bwana mwanyoha ndegwa amewahikiza wazazi kuchukua jukumu, ili kuwapatia ushauri nasaha watoto wao. Hii ni baada ya kufahamu kuwa wazazi hawana wakati na kizazi Chao. Wao huona kuwa ni jukumu la walimu kuwa mlezi siku zote .
Serikali imehimizwa kuanzisha mradi wa kuwapatia watoto chakula shuleni. Watoto wana kiu ya kuhudhuria masomo lakini hawana maji pamoja na lishe Bora. Katika eneo ya lamu mashariki , serikali inahimizwa kujenga maabara na madarasa yakutosha. Wanafunzi wanahitaji msala , kwenda haja kichakani si suluhisho Bora

Imebainika kwamba wazazi wengi hawana muda na watoto wao. Sheikh shabib alikiri kuwa matatizo ni mengi , ni Bora wazazi kutoa maoni zaidi. Wanapofanya hivyo, tabia na mwenendo ya watoto itabadilika.kikundi kinachosimamia shule za upili , kinachoongozwa na kaviho hamisi imetoa ombi kuwa ni Bora kuwasaidia watoto waliowapoteza wazazi wao .mwalimu mkuu lamu mashariki anaiomba serikali kuongeza walimu tano wasaidia watahiniwa.
Shirika la “ngec” inaoongozwa na bwana lichuma inahimiza serikali kuwasaidia watoto waliokumbwa na janga la tana Delta, wazazi wao walipofariki. Walimu wanafaa kutoa ushauri nasaha na mwelekeo kwa watoto wa kike.jambo hili litazuia janga la mimba za mapema. Wasichana Hawa hupata uja uzito katika umri mdogo Sana. Jambo hili limewakera wazazi mno.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img