10.6 C
London
Friday, October 18, 2024
HomeInternationalKENYAUSHURU WA AJABU

USHURU WA AJABU

Date:

Related stories

African Peacebuilding Network: Individual Research Fellowships

The APN and Next Gen program of the Social...

Applications for IOC Young Leaders Programme 2025-2028 now open

Applications for IOC Young Leaders Programme 2025-2028 now open Young...

Turmoil in Kenyan Politics; National Assembly Votes to Impeach Deputy President.

In a stunning development that has sent shockwaves through...

How Can African Women Bridge the Digital Gender Gap?

By Guest Writer There is a harsh reality in digital development:...

Man, 47, jailed for FGM in Nottingham

The UK is making strides in sending perpetrators of...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Ushuru ni pesa ambazo hutumika kujenga nchi. Bara la afrika Lina nchi kama Kenya, uganda na Tanzania mtawalia. Ili nchi iwe na maendeleo nchini ni Bora wananchi walipe ushuru. Kila mara ushuru huletea nchi faida chungu nzima kwa njia zifuatazo ; Ujenzi wa Barabara .Ni wazi kutambua kuwa watu wanaposafiri katika sehemu mbalimbali nchini, utaona ujenzi wa Barabara ikiendelea. Kuna barabara nzuri ya kupendeza na kuvutia kama ” Thika super highway” ikiwa kama wakenya hawatalipa ushuru, bila shaka nchi yetu itachelewesha maendeleo kabisa. Barabara nzuri itasaidia usafiri kuwa rahisi na bidhaa zitafika sokoni bila kuharibika.

Ubora wa shule, shule nyingi hapa nchini hufadhiliwa na serikali na pia kununua vitabu vya kusoma. Pia Kuna elimu bila malipo , lakini wazazi huchangia kwa sehemu kidogo, kwa kununulia Watoto wao sare na chakula Cha watoto wao. Elimu ni Hali ya kupata mafunzo darasani au hata nyanjani .
Huboresha hospital, jukumu la kila mkenya ni kulipia ada mbalimbali anapotembelea katika kituo Cha afya. Malipo haya hujumuishwa kama ushuru. Malipo haya hufanywa kwenye mitambo wa tarakilishi. Baada ya kulipa ushuru , mwananchi hupatiwa dawa na hata neti ambazo husaidia ugonjwa wa malaria . Si ajabu kufahamu kuwa ukilipa ushuru unajenga nchini iliyo na maendeleo chungu nzima.

Kilimo ni uti wa mgongo . Serikali ya kenya imefanya juhudi zaidi . Wananchi wameweza kupata mbolea kwa Bei nafuu. Katika Kaunti ya Uasi GIshu wakulima wengi wamechangamkia kilimo na kuzalisha chakula . Ingawa Bei ya unga bado imepanda kupita kiasi. Bado wananchi wanatia bidii katika shughuli za kilimo.
Wananchi wanaponunua mbolea kwa wingi, Pesa hizi bila shaka hutambulika kama ushuru. Pia kule sokoni wale ambao huuza bidhaa mbalimabali kama vile nguo, vyakula na vyombo vya nyumbani, hulipia ushuru kulingana na idadi ya bidhaa unazouza . Ingawa kulipa ushuru husaidia nchi, wakenya bado wanapitia matatizo mengi zaidi , wanafunzi waliotarajiwa kujiunga na kidato Cha kwanza, bado wamesalia nyumbani. Je, tatizo liko wapi? Bado wakenya wanajiuliza maswali mengi .

Gharama ya juu ya bidhaa , ni Hali ya kuvunja moyo unapotembelea maduka ya jumla . Bidhaa zinauzwa kwa Bei ghali mno. Bidhaa kama sukari, mafuta na hata unga imepanda bei , kwa kweli maisha imekuwa ngumu nchini kenya. Ukosefu wa chakula Cha kutosha . Unapotembelea Gatuzi la Turkana , baadhi ya wananchi wanafariki kwa kukosa chakula. Si ajabu kufahamu kuwa wananchi Hawa kutoka Turkana pia hulipia ushuru lakini wanafariki kutokana na njaa. Ni haki ya serikali kujali wananchi wao. Si kila mara kujihusisha katika siasa pekee. Jambo la ukosefu wa lishe bora imesababisha vifo na hata magonjwa.

Mafuriko ya maji ambayo hujaa au hufurika katika sehemu mbalimabali za nchi . Ni jambo la kuvunja moyo sana , ukitembelea maeneo ya Budalangi bado Kuna mafuriko ya ajabu , watu wametoroka makazi yao, wanaishi katika shule au kanisani. Wananchi Hawa wamejitolea kulipa ushuru lakini hawajapata zaidi yoyote . Wakati mvua hunyesha kwa Kasi mno. Nyumba za watu husombwa na maji haya. Kina mama na watoto ndio huteseka . Ni matumani yangu kuwa serikali itatatua shida hii kwa haraka mno.
Bei mafuta ,mafuta hutumika katika uchukuzi na hata kituo Cha mafuta magari huwekewa mafuta , kwa Bei ya juu mno. Mafuta ndiyo husaidia katika kila nyanja , ikiwa Bei ya mafuta itashuka bidhaa pia zitashuka Bei. Wananchi wengi wameshindwa kutatua kitendawili Cha Bei ya mafuta. Serikali ilipoondoa ruzuku mambo yalibadilika na maisha kuwa magumu.

Baada ya vuta nikuvute , Bei wa mafuta ilipungua kwa kuondoa shilingi Tano tu, Hali hii bado haijabadilisha maisha ya wakenya, bado wanateseka zaidi. Kila mkenya alikuwa na matumani raisi William Ruto atapunguza ushuru wa bidhaa, hadi sasa hivi ushuru unazidi kuongezwa ikiweno ili ya nyumba za Bei nafuu.safari za wabunge kuenda nchi mbalimbali ni kawaida kama Sheria .
Wananchi wanateseka lakini wabunge wanasafiri . Wagonjwa wa saratani bado wanalia hawajapata suluhisho. Nimesalia na maswali chungu nzima,” nani atakomboa Taifa letu? “Bado ninazidi kujiuliza maswali kila wakati. Ili kuboresha maisha ya wakenya nchini ni Bora Wabunge wangepunguza Safari za ng’ambo basi wananchi wangepunguziwa mzigo wa ushuru kidogo. Je, wakenya tulikosea wapi” bado ninajuta moyoni mwangu.

Ufisadi wa sekta mbalimbali . Kila mwananchi ana haki ya kupata hudumu Bora. Baada ya kusoma kwa bidii. Kupata ajira imekuwa ni tatizo. Kuna wanafunzi ambao walibahatika kwenda ng’ambo kufanya kazi ili kubadilisha maisha ya wazazi wao.
Kupata cheti Cha usafi imekuwa ni tatizo. Ilimbidi waziri wa usalama profesa kindiki kuingilia kati. Ilikuwa ni vita nikuvute ungalitoa hongo kwa haraka. Basi ungepata cheti chako haraka mno. Lengo kuu ilikuwa kupata ushuru wa kiwango Cha juu.
Heko kwa waziri kuondoa wananchi Katika minyororo ya ushuru zaidi, je ni lini ushuru na gharama ya maishi itapungua au kurudi chini.”bado mnajiullza maswali mengi kila wakati jua linapochomoza , wananchi wengi bado wanamatumaini kuwa siku njema itatimia siku moja .

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img