Maji ni uhai katika maisha ya binadamu. Mfano wa vyanzo vya maji ni kama mito , maziwa , mabwawa, chemichemi na maji ya ardhini , ambavyo hutoa maji kwa vifaa vya maji ya kunywa na visima vya kibinafsi. Maji hutumika shuleni, afisini, hospitalini na hata msalani.
Siku ya maji duniani huadhimishwa machi tarehe ishirini na mbili . Kila mwaka . Katika usemi wake Antonio Guterras ambaye ni katibu mkuu wa umoja wa mataifa . Pia Guterras alisema ” miti yetu mji yetu” kwa hivyo bila kunywa maji si Bora kwa afya ya binadamu. Tunaweza kuchota maji tukitumia mitungi ,jerican , vibuyu na hata Kuna Lori ambazo husafirisha maji ” almaarufu clean water” ambayo hubebwa kwa gari. wakazi wa kaunti ya Mombasa wanalilia serikali kuhusu ukosefu wa maji . Pia sehemu mbalimbali katika kaunti ya Nairobi wakazi hawana maji.
Bidhaa hii imekuwa ghali mno. Kabla kunywa maji , ni Bora maji hayo yachemshwe ili iwe salama kwa matumizi. Bali na kuweka dawa, tunaweza kutumia kichujio kuondoa uchafu katika maji.maji husaidia kuzuia uwezekano wa kupata baadhi ya magonjwa kama vile saratani ya tumbo na kibofu Cha mkojo Wakati mtu hunywa maji kwa kiasi kinachohitajika.
Mtu mzima anashauriwa kunywa maji safi na salama kiasi Cha Lita moja na nusu, kwa siku au glasi nane kwa siku. Pia ongeza kiasi cha maji kama vile sharubati ya matunda mara kwa mara kila wakati.
Unywaji maji hupunguza hatari wa kupatwa na Ugonjwa wa moyo. Watu wanaokunywa glasi za maji zisizopungua glasi Tano kila siku, si ajabu wao hujiepusha na uwezekano wa kupatwa na Ugonjwa wa moyo. Isitoshe maji mengi husaidia kupunguza uzito kwani maji hayana mafuta Wala sukari.
Maji husaidia Katika uyeyushwaji wa chakula. Usafirishaji wa virutubishi na ufyonzwaji wa virutubisho mwilini.pia husaidia kupunguza uchovu wa mwili . Daktari hushauri watu kunywa maji kila wakati.
Je viungo vya mwili huweza kufanya kazi bila maji? Jawabu ni la au la ? Maji husaidia katika kutengeneza majimaji Yanayopatikana katika viungo vya mwili kama vile viwiko na magoti, hivyo basi husaidia viungo viweze kufanya kazi vizuri . Viungo vya mwili vinahitaji maji zaidi ya asilimia sitini ya uzito wa mwili wa binadamu ni maji. Hivyo basi maji husaidia mwili kufanya kazi vyema.
Ikiwa mtu atakuwa na shida ya kuenda msalani daktari huhimiza kuwa maji ni tiba ya ukosefu wa choo. Kunywa maji ya kutosha kila siku hukuepusha na tatizo la ukosefu wa choo mara kwa mara. Mtu anapokuwa katika Hali ya kuhara na kutapika . Anashauriwa kunywa maji mara kwa mara ili kuzuia upungufu wa maji mwilini. Suala la kutumia maji yaliyoongezewa chumvi na sukari ni muhimu wakati mtu anapokuwa anaendesha na kutapika . Unywaji wa pombe husababisha mtu kuenda haja ndogo mara kwa mara na hivyo kupoteza maji kwa wingi.
Hata hivyo dalili ya mtu kupungukiwa maji mwilini na kuumwa kwa kichwa. Daktari hushauri mja kunywa maji ya kutosha ukifanya hivyo bila shaka hautasumbuliwa sana na kuumwa na kichwa kila wakati.
Bali na matumizi ya viungo vya mwili , maji pia hutumika katika njia zifuatazo, wakulima hutumia maji kunyunyizia mimea yao.wakati wa kiangazi jua Huwa Kali kupita kiasi .kwa hivyo mimea huhitaji maji. Kiangazi ni wakati Kuna jua Kali sana na hata mimea hukauka kwa wingi.
Wanyama huhitaji maji katika harakati zao za mapumziko. Wanyama kama ng’ombe, mbuzi , kondoo , Bata hunywa maji . Kama binadamu samaki pia hupata makazi yake majini.akitolewa majini yeye hufa . Waswahili hawakukosea waliposema kuwa chura hupenda maji lakini si maji moto. Kwa hivyo baadhi ya wanyama hutumia maji kama makazi wanapoishi na kujistarehesha. Ukitembea maeneo ya hospitalini wagonjwa hutumia maji kunywa na pia kuosha nguo zao. Shuleni wanafunzi hutumia maji kupiga deki madarasa Yao, na kuosha vyoo vyao. Mazingira ukikosa maji hatakuwa ya kuvutia.
Magari ya umma Huwa chafu . Wakati Kuna vumbi nyingi huchafuka . Ili kufanya gari hizi Huwa ya kuvutia ni vyema kuviosha. Madereva hutumia maji kuosha magari haya.nyumbani kina mama hutumia maji kupikia chakula jikoni.
Mtu yeyote bila shaka hupenda meno yake yawe safi.maji hutumika kuoga ili tuwe safi na nadhifu. Waswahili hawakukosea waliposema kuwa maji ukiyavulia nguo yakoge Hauna budi kuyaoga.wasusi hutumia maji kuosha nywele zao kwenye ” salon” maji yakija Kasi yapishe kwasababu yanaweza kukusomba na kuua. Bila maji basi maisha hayatakuwa Bora. Maji hutumika kusafirisha mifugo na pia kumezea dawa na wagonjwa.