7.9 C
London
Friday, October 4, 2024
HomeInternationalKENYAGiza la Mshangao Nchini Kenya(In Swahili).

Giza la Mshangao Nchini Kenya(In Swahili).

Date:

Related stories

Man, 47, jailed for FGM in Nottingham

The UK is making strides in sending perpetrators of...

Vumbi Ni Hatari Katika Afya yetu?

Vumbi ni hali ya chembe zinazopeperuka hewani za asili...

Fahamu Zaidi Alama Za Barabarani

Alamu za barabarani huweza kuwa nguzo muhumu kwenye kando...

Hofu Yatanda Kufuatia Mlipuko Wa Mpox

Ugonjwa wa Mpox husababishwa na virusi vya "Monkey Pox"...

Je, Kamusi Inatofautiana Vipi Na Vitabu Vingine?

Shuleni ni mahali ambapo wanafunzi huenda ili kupata elimu....
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Sitasahau siku ya Jumatano tarehe kumi na tatu Desemba . Nilidhani kuwa Ni Mimi pekee , kumbe kote Nchini kulikuwa na giza . Nilijikaza kutumia genereta lakini ajabu ilikuwa ukosefu wa mafuta. Jambo hili liliwanshangaza wakenya Sana. Waziri wa kawi Davis chir chir hakutoa taarifa yoyote kuhusu janga hili kwa haraka.

Nchini Kenya katika anga tua(airport) la Jomo Kenyatta wasafiri wa kuenda ng’ambo waliteseka Sana. Kila mahali kilikuwa na giza totoro. Shughuli za siku zilikamilika mapema Sana , kwa hivyo wananchi walienda nyumbani mapema Sana . Ukosefu wa umeme uliwafanya wasafiri kuchelewa kufika nyumbani, kwasababu wengine hawangeweza kuendelea na Safari yao. Ilimbidi waziri wa Barabara bwana Kipchumba Murkomen kuwaomba wakenya msamaha kutokana na ukosefu wa umeme. Jambo hili lilimkasirisha Sana moyo, aliamua kufanya mabadiliko ya haraka katika wizara hii.

Airport at night

Kuna baadhi ya viongozi waliopoteza ajira bila kupata taarifa zaidi. Baadhi ya wakenya walikadhiria hasara kubwa. Kuna wale ambao Ni wafanyibiashara wa kuuza nyama , nyama hii huhifadhiwa kweye ghokofu(refrigerator). Umeme ulipotea kwa masaa kadha , nyama hiyo iliharibika .
Wateja ambao walikuwa kwenye mkahawa hawangeweza kunywa chai kwenye giza. Iliwabidi kufunga Safari na kuelekea nyumbani. Hata Kuna baadhi yao ambao hawakulipa pesa na walipoulizwa wengi walitoroka na kuwa wakali kupindukia.

Pia ilikuwa ni huzuni kwa wauzaji wa samaki kwa kuwa waliopoteza wateja na huku samaki zao kuharibika. Fundi ambao hutumia umeme katika shughuli zao walikosa umeme na wateja. Je Ni Nani atatulipia hasara tuliokadhiria,mmoja wa mfanyibiashara aliuliza kwa uchungu zaidi. Duka za jumla zilikosa wateja wengi Kama siku za kawaida. Kila mmoja aliwaza na kuwazua jinsi siku hiyo itakavyokamilika .

Nao wauzaji nguo walikosa nafasi bora kupima nguo kabla ya kununua. Katika soko la Gikomba ilikuwa Ni majonzi tela, huku “Eastlergh,” hali ilikuwa vivyo hivyo tu. Soko ilifungwa mapema, siku yao haikuwa ya kawaida . Askari walipatwa na wakati mgumu giza hii ilichangia utovu wa usalama mjini. Baadhi ya vijana walifurahia Sana kwa kuwa walijinyakulia mapato zaidi bila kutoa jasho.
Katika vyombo vya habari Kama vile Radio, citizen , ktn . Mawasiliano ilikatizwa . Wakenya hawangeweza kupokea taarifa za habari. Wananchi wengi walikazimika kulala mapema. Ni Jambo la kusikitisha kuwa giza hilo lilidumu kwa masaa kumi na nne.

Si ajabu kusikia kuwa wagonjwa waliteseka , Kuna wale ambao walikuwa katika chumba Cha upasuaji . Shughuli hizi kwa Mara nyingi huhitaji umeme . Si makosa kusema kuwa siku njema huonekana asubuhi. Lakini siku ya wagonjwa ilikuwa ya taabu nyingi na uchungu zaidi. Pesa ambazo walilipa kwa huduma hizo hazikufanya kazi kwa ukamilifu. Madaktari malijaribu juu chini kutumia genereta kutimiza wajibu wao.
Mashine zote za hela almarufu “ATM” zilikosa kutoa huduma zao. Wale ambao hawakuwa wamenunua vyakula walijuta Sana na kulala njaa. Mashine hizi ziligubikwa na giza totoro. Shughuli zote zilisitishwa na jumba hili likasalia mahame. Hali hii ilisababisha mgogoro Kati ya wasafiri na abiria. Wengine wao walijitetea hawana nauli kwenye simu zao au hata mfukoni. Ilikuwa ijumaa ya mahangaiko na hasara nchini Kenya.

Wale kina mama wenye biashara ya salon walikosa wateja, kazi yao haikuza matunda Kama kawaida. Ilikuwa Ni vigumu wao kukamilisha kazi zao za ususi. Kuna baadhi ya wateja wao ambao walikosa kwenda kazini. Tatizo Ni kuwa nywele zao zilikuwa hazijakamilika kusukwa. Pia kuchemsha maji ya kuosha vywele hizo ilikuwa Ni changamoto mkubwa.
Mary Atieno mfanyibiashara anayemiliki kibanda Cha saluni jijini Nairobi , alisema kuwa alipata hasara kutokana na kupotea kwa nguvu za umeme. Kila Mara yeye huingiza takribani shilingi 3000 , pia Charity Kilei anayemiliki duka la kuunda keki jijini alipoteza wateja.

Wakenya bado wako gizani hii Ni kwasababu Hadi Leo hawajafahamu kilichosababisha giza Totoro . Uchunguzi bado unafanywa kwa kina. Baadhi ya wafanyibiashara waliopoteza kulingana na hitilafu ya umeme , wanaiomba. serikali kuwafidia. Iliwabidi wengine kupiga moyo konde na kununua genereta Ni matumaini yangu kuwa kitendawili Cha umeme kupotea kitateguliwe haraka.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img