16.8 C
London
Monday, September 16, 2024
HomeBusinessEconomyJINSI YA KUFUFUA UCHUMI NCHINI KENYA

JINSI YA KUFUFUA UCHUMI NCHINI KENYA

Date:

Related stories

Retirement: The Beginning of a New Adventure

Retirement is often viewed as the end of a...

Corruption in Africa: A Persistent Threat to Economic Growth and Development

Corruption remains one of the most profound challenges facing...

Top Strategies for Successful Marketing in the Digital Era

In the rapidly evolving digital landscape, businesses must adapt...

Strategies to Eliminate Debt and Achieve Financial Freedom

Debt can be a significant burden, affecting both financial...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Uchumi ni mapato na matumizi ya watu katika nchi au Mali na fedha ambazo zinaptikana kutokana na shughuli za watu. Pindi tu baada ya uchaguzi wa mwaka ya elfu mbili ishirini na mbili.Maisha ya wakenya ilibadilika mno na gharama ya maisha ilikuwa juu zaidi.

Hata hivyo Kuna baadhi ya mbinu zifuatazo zinazoweza kutumiwa ili kufufua uchumi nchini kenya. Kubadilisha mawazo wakati wa kuchagua kazi au kutobagua kazi. Kazi za viwango vya juu kama uhandisi, urubani, unahodha na mwanasheria nyakati nyingi hufanywa na wageni kutoka ng’ambo , wao hupata malipo ya Hali ya juu. Ni Bora serikali kugeuza Hali hii ili wanyeji wachukua kazi hizi , na kupata kiasi kikubwa Cha mshahara, wakifanya hivyo bila shaka uchumi utaimarika vyema.

Kuongeza idadi ya vyama vya ushirika nchini . Vyama vya ushirika vinapaswa kuongezwa nchini kenya ili wananchi waungane pamoja kwa Nia ya kujiendeleza na hapo ndipo watafaifaidi nchi Yao .kila mwananchi anafaa kutekeleza wajibu wake ipasavyo. Isitoshe serikali inaweza kufufua uchumi iliyosambaratika kwa kununua hisa za makampuni ya nje kwa kufanya hivyo itaendeleza uchumi kwa vile itakuwa na kibali Cha kufaidika kutokana na faida zinazopatikana kutoka kwa kampuni hizo kila wakati.

Kupunguza ufisadi nchini kenya.ufisadi ni utumiaji vibaya wa Mali ya umma au shirika kwa Nia ya kuharibu. Kuna baadhi ya viongozi ambao Nia Yao si maendeleo Bali ufujaji wa Mali ya serikali kila wakati.
Viongozi ni lazima wawe mfano nzuri katika harakati za kuboresha uchumi.viongozi wenye nadhifu mbalimbali katika serikali kama vile Gavana, seneta, wakati mwingine si mfano Bora .wengi wao hujiingiza katika ufisadi ili wajinufaishe .kwa mfano aliyekuwa Gavana wa Nairobi mike sonko alikabiliwa na kesi ya ufisadi,Kisha akapoteza wadhifa wake. Uchumi wa nchi haiwezi kuendelezwa kwa njia ya uporaji wa Mali ya umma.

Utulivu na amani nchini.utulivu wa nchi ni jambo la busara . pindi tu baada ya uchaguzi wa mwaka wa elfu mbili kumi na ishirini na Mbili, kulikuwa na maandamano nchini kenya. Wakenya waliamua kuenda barabarani ili kudai haki zao. Maandamano haya yaliyoitishwa na kiongozi wa upinzani bwana Raila Amolo Odinga .kulikuwa na vita zaidi na barabara kuchomwa.Nchi yoyote yenye rabshabsha miongoni mwa wananchi wake haiwezi kupiga mbele kiuchumi.utulivu Huwapa wanchi nafasi ya shughulikia wajibu wao wa kujenga Taifa dhabiti.

Jambo hili hufanya serikali kutumia pesa nyingi kununua zana za vita kama bunduki , vitoa machozi,ili kukabiliana na waandamanaji.Hii ni uharibifu wa Mali ya umma. Kwasababu pesa hizi zingeweza kutumiwa katika kuboresha uchumi.
Wananchi hujitegemea kibinafsi na i wanafaa kujitegemea kwa kila jambo linaloweza kuifaidhi nchi kwa jumla.si lazima uajiriwe serikalini au kungojea nafasi za kazi zinazotangazwa kwenye gazeti.

sekta ya jua Kali ni mfano Bora wa kuiga ili mwananchi ajitegemee.Jambo hili litafanya serikali kukosa kutaabika kutafuta kazi kutoka nchi za ughaibuni. Kama vile rais William Ruto anavyojitahidi kutembea mataifa mbalimbali kwa Nia ya kutafutia vijana kazi.
Kuna benki nyingi nchini kenya ambazo hupatia watu mkopo, riba ni pesa za ziada apatazo mtu aliyekopesha watu fedha. Ikiwa serikali itafutilia mbali riba basi uchumi utaimarika.Jambo hili litawashawishi watu wengi kutumia mikopo ya aina hii ili kuinua maisha Yao na kuendeleza na kuendesha uchumi wa nchi zao .kuekeza ni njia Bora ya kuweka akiba.kama vile waswahili husema kuwa akiba hauozi.

Badala ya nchi kuomba mikopo ni afadhali kutafuta wafadhili au wahisani . Si vyema kuomba pesa ambazo nchi haitaweza kulipa haraka.wahisani katika nchi wataelewa. Kenya Ipo katika nchi ambayo haijastawi .Jambo la kudai malipo kwa kutoza riba ya juu hudhoofisha uchumi zaidi .Huu ni ukoloni mamboleo ambao haufai kamwe.

Kudharau kazi ya ukulima, ukulima ni kazi ya kulima shamba na kupanda mimea Kisha kuvuna mazao.katika ukulima unaweza kutumia vifaa kama plau, trekta.wakenya wengi hawaithamini kilimo kwa ujumla. Ukuzaji wa vyakula huwachiwa watu wasio na tegemeo jingine.mwelekeo huu ukibadilishwa kwa kiwango Cha juu, bila shaka uchumi itabalika.

Uchumi wa nchi hudhoofika kwasababu ya uvivu.ni bora kutia bidii katika kilimo kwasababu ndio uti wa mgongo. Ni nyema kutegemea rasilimali iliyopo nchini badala ya kijikita katika kutegemea nchi za ng’ambo.Bidhaa nyingi ambazo hununuliwa kutoka ughaibuni hugharimu serikali fedha nyingi mno.uchumi Bora huleta matumani kwa wazazi kwasababu, wataweza kukidhi mahitaji Yao vyema. Kulipa karo ya wanafunzi itakuwa rahisi hata usaf iri hatakuwa na changamoto.wakenya wengi hawataenda Saudi Arabia kutafuta kazi za nyumba, ili kusaidia familia zao . Wakenya Hawa huteseka sana na wengi kupoteza maisha Yao .

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_img