14.8 C
London
Wednesday, October 16, 2024
HomeCommunityKibarua Cha Nacada

Kibarua Cha Nacada

Date:

Related stories

African Peacebuilding Network: Individual Research Fellowships

The APN and Next Gen program of the Social...

Applications for IOC Young Leaders Programme 2025-2028 now open

Applications for IOC Young Leaders Programme 2025-2028 now open Young...

Turmoil in Kenyan Politics; National Assembly Votes to Impeach Deputy President.

In a stunning development that has sent shockwaves through...

How Can African Women Bridge the Digital Gender Gap?

By Guest Writer There is a harsh reality in digital development:...

Man, 47, jailed for FGM in Nottingham

The UK is making strides in sending perpetrators of...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Sikuwai tambua kuwa pombe ina madhara mengi maishani, nilipokuwa shuleni maeneo ya Lukore kaunti ya kwale, masomo yangu yalitiwa doa kwa kuwa mraibu wa pombe kila mara kwa mara. Hata hivyo nilitembelea kituo cha “Nacada'” ili kufahamu zaidi kujua hali yangu. Je, Nacada ni nini? niliwaza moyoni mwangu.

Kazi ya Nacada ni kuelimisha watu kuhusu jinsi ya kujiepusha na matumizi mabaya ya dawa za kulevya. Kuwafanya watu wawajibike kuhusu dawa. Wizara ya afya imeandaa kanuni zinazolenga kupiga marufuku uuzaji wa pombe katika mkahawa, maduka ya jumla na maeneo mengine ya umma. Kanuni hii itaathiri pakumbwa biashara ya pombe endapo itapitishwa na kuanza kutekelezwa.

Hii ndio maana hatua hiyo imepingwa na wadau kama vile chama cha wamiliki wa baa au danguro nchini. Nacada iliamuru kuondolewa kwa mabango ya matangazo ya vileo karibu na taasisi za masomo. Matangazo hayo yana uwezekano wa kuleta hisia potovu kuhusu sifa na athari za kijamii kuhusu kinywaji hiki ,sheria ya kudhibiti vinywaji na vileo inatoa dhima kisheria katika maeneo yaliyopigwa marufuku na serikali ya Kenya.

Mamlaka ya kitaifa ya kampeni dhidi ya matumizi mabaya ya pombe na dawa za kulenya, Nacada ni shirika la kiserikali la “Semi Autonomous” chini ya wizara ya mambo ya ndani na uraibu wa serikali ya kitaifa kulingana na agizo la utendaji.
Faini isiyozidi elfu mia tano au kifungo jela kisichozidi miaka mitatu au vyote kwa pamoja. Mamlaka ya kitaifa ya kampeni ya kupambana na matumizi ya vileo na dawa za kulevya imetangaza msako mkali nchi nzima ili kuzifunga baa na vituo vinginevyo vya kusambaza vileo vilivyo karibu na taasisi za masomo.

Naibu wa rais Rigathi Gachagua amekuwa mstari wa mbele kuunga mkono shughuli za Nacada. Mienendo ya wazazi kunywa pombe mbele ya watoto wao ndiyo chimbuko la visa vya matumizi ya pombe na mihadarati miongoni mwa wanafunzi wa shule za msingi na upili. Mazingira ya nyumbani yamegeuka kuwa hatari kwani wengi wa wanafunzi wanakiri kuiga uraibu wa kutumia pombe na dawa za kulevya kutoka kwa wazazi na wakubwa wao nyumbani, ongezeko la visa vya watu kunywa pombe nyumbani baada ya kufungwa kwa baa imekita mizizi.

Wanaharakati wa kukabiliana na uraibu wa dawa za kulevya kanda la Pwani inatoa wito kwa jamii kushirikiana ili kudhibiti utumizi huo wa mihadarati. Katika kaunti ya Elgeyo Markwet kituo cha kurekebisha wakazi waliolemewa na pombe pamoja na dawa za kulevya kilijengwa. Kituo hicho kina wataalamu wa kutosha na hutoa huduma kwa wakazi katika kituo hicho ambacho kinaweza kuwahudumia watu thelathini kwa wakati mmoja. Kaunti ya Elgeyo sasa ina wataalamu wawili wa tiba ya akili na wauguzi kadhaa waliosomea saikolojia na magonjwa mengine ya akili. Vijana wengi ambao walidanganywa na wanabiashara wa pombe haramu hatimaye waligeuka kuwa waraibu sugu.

Ushirikiano wa serikali za kaunti katika kutokomeza zimwi la matumizi ya pombe haramu na dawa za kulevya utasaidia vijana. Shirika la Nacada limeanza mipango wa kufualilia watu ambao wamepitia vituo kama kwa kufanya hivyo itawasaidia kupata ujuzi na kuanzisha mipango ya kujipatia riziki.

Matumizi ya dawa hizi za kulevya ni moja kati ya vitisho vitano vya usalama wa kitaifa ambavyo hujumuisha ugaidi, ujambazi na wizi wa mifugo itikadi za Kale za kitamaduni, kidini na kisiasa na mabadiliko ya tabianchi. Serikali imeimarisha uwezo wa shirika la kupambana na matumizi ya dawa za kulevya, Nacada hupiga vita upatikanaji wa pombe haramu mihadarati na dawa zingine za kulenya kama njia ya kupiga jeki mpango wa maendeleo wa kitaifa ili kuboresha uchumi wetu. Je, Nacada ina sifa gani? inakidhi matakwa ya sura ya sita ya katiba ya Kenya kuhusu Uongozi na uadilifu.

Cheti cha ujuzi wa kompyuta kutoka taasisi inayokubalika. Ustadi katika matumizi ya kompyuta, uwezo wa kufanya kazi chini ya shinikizo na kuweka kipaumbele. Mwenyekiti wa Nacada alidai kuwa barabara ya Salgaa inafaa kurekebishwa ili kupunguza visa vya ajali katika eneo hilo. Hii ni baada ya watu wanne kufarika kwenye barabara, hivyo katika visa viwili vya ajali mwishoni mwa wiki. Ni vyema jamii izinduke na kupata mwamko pamoja na uhamasisho kuwa uraibu sio uhalifu, vile vile jamii inapaswa kuhamasishwa kuhusu matumizi ya dawa hizi.

Nacada ni mfano bora kwa vijana kwa kutoka mashauri na uelekezi. Ikiwa serikali itafanya bidii kusaidia vijana na mirada mbalimbali, kama vile rais William Ruto aliahidi kurudisha kazi kwa vijana. Ikiwa ndoto hii itatimia vijana watakuwa na majukumu zaidi na kusahau dawa hizi. Uraibu ni adui ya maendeleo nchini.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img