3.1 C
London
Wednesday, January 22, 2025
HomeInternationalKENYAMABADILIKO BAADA YA UCHAGUZI

MABADILIKO BAADA YA UCHAGUZI

Date:

Related stories

Why Emotional Literacy Matters for Children

Building a Strong Foundation: Why Emotional Literacy is Essential...

Mind Management, not Time Management.

The Illusion of More Time: Why Mind Management Trumps...

Behaviour Management in Children

Understanding and Guiding Children's Behaviour: A Practical Approach Raising children...

What’s New in the Latest ChatGPT: Enhanced Features and Capabilities

The latest version of ChatGPT, powered by GPT-4, has...

The Silent Revolution: How Tech Schools Are Transforming Lives in Nairobi’s Slums

In the heart of Nairobi’s bustling informal settlements, a...
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes


Unapotembea barabarani nchini kenya, sio ajabu kusikia wakenya wakilalamika.Je, ni lini Bei ya unga itashuka au gharama ya maisha kurudi chini? Yote haya ni gumzo tu, jawabu ni kuwa Hali ya maisha imewakaba kooni , hata sasa wanategemea Mola kuwapatia suluhisho kamili. Si mafuta , si ushuru , si karo, si nauli yote ni shida mno.

Katika sehemu mbalimbali za nchi kila mmoja ana dukuduku moyoni. Kuna baadhi ya jamii ambazo hula mlo mmoja kwa siku au hata hukosa chakula mchana kutwa. Ikiwa rais Ruto ana nia basi ni Bora yeye pamoja na naibu rais bwana Rigathi Gachagua kutoa suluhisho kuhusu janga hili . Si kila mara kulaumu serikali iliyopita kwa masahibu yanayowakumba wakenya siku zote, ni wazi kuwa katika nchi ya kenya Sheria za kortini hazifuatwi. Si ajabu kusikia wakenya Tena wanajipanga kuandaa maandamano kuhusu gharama ya maisha.

Ni wazi kuwa vikao vya “Bomas of kenya” haijazaa matunda yeyote . NI kama kupigia mbuzi Gita. Baada ya sehemu mbili . Mrengo wa kenya kwanza na azimio, waliwakichezea wakenya mchezo wa paka na panya kila mara.
Je, serikali hii inamjali mkenya wa kawaida. Ikiwa tunalumbana kila siku ,ni vigumu sana kupata suluhisho ya muda . Kila wakati si Bora kudharau mahakama ikitoa uamuzi na hatimaye kutoa vitisho kuwa yule ambaye atapinga uamuzi , na kusema atapata Cha mtema Kuni. Seneta wa Busia mheshimiwa okiya omtata analakamika kuwa maisha yake imo hatarini. Hii ni baaada ya kupinga Makato ya ujenzi nyumba ya Bei nafuu.

Ushuru wa nyumba imebadilika kuwa kwenye njia panda. Hii ni baada ya Sheria kuhusu ushuru wa nyumba kupitishwa bungeni, bado wakenya wanazidi kubomoleawa nyumba zao usiku kucha. Katika kaunti ya Mombasa wakenya wamekosa makao dhabiti . Kwa vile nyumba zao zimebomolewa hadharani . Je, nani atamtetea mwananchi wa kawaida . Ushuru ni ada inayotozwa mwananchi ili kusaidia kujenga nchi.

Serikali imebadilisha ada ya stakabadhi muhimu. Ikiwa utapoteza kitambulisho chako, kuwa tayari kulipa shilingi elfu mbili , na ukitaka kupata kitambulisho kwa mara ya kwanza kuwa na elfu moja kugharamia ada hii. Hapo awali ilikuwa shilingi hamsini tu, pia wale ambao wangataka kupata pasipoti kwenda ughaibuni basi ni sharti watalipia shilingi elfu saba , ajabu ni kuwa hapo awali ilikuwa shilingi elfu nne mia Tano. Hii ni wazi kuwa mkenya wa kawaida lazima agharamia kupita kiasi.

Waziri wa elimu bwana Ezekiel Machogu amefanya mabadiliko katika chuo kikuu . Wanafunzi walikuwa wakienda kufanya kozi za ” certificate” almaarufu stakabadhi, na pia diploma. Kwa sasa ,kozi hizi zitafanywa katika vyoo vya ufundi almaarufu “TVET” lengo kuu ni kukuza vipaji na Talanta pamoja na maarifa.
Malipo ya “e citizen” serikali Ina Nia kuu kwa wakenya. Waziri wa habari na teknolojia bwana Eliud Owalo amezundua mambo mapya katika ” e citizen ‘” ada zote za serikali sasa zitalipwa kupitia mtandao huu . Wanafunzi pia wanaojiunga na chuo kikuu , wanashauriwa kutumia mitandao huu kulipa karo Yao kupitia mtandao huu.

Isitoshe ni Bora kufahamu kuwa Rais William Ruto amependekeza kuwa malipo ya karo yote yafanywe , kupitia teknolojia hii . Jambo hili limewakera wazazi na baadhi ya viongozi. Kuna wale wazazi ambao hulipa karo kupitia kuleta mazao kama mahindi shuleni, Kuna wale ambao ni wakulima ambao hupenda mboga , Kisha kuleta shuleni kama karo. Je, wao watalipa karo vipi? Maswali haya bado yanahitaji majibu kutoka kwa serikali.

Imekuwa ni safari ndefu mno kwa kiongozi wa upinzani bwana Raila . Amejaribu kuwania kiti Cha rais mara Tano bila mafanikio. Lakini hajawai kufa moyo. Kweli Mungu hawezi kusahau mja wake maishani. Usiweke siasa na chuki moyoni mwako. Sasa hivi rais William Ruto ameunga mkono Raila odinga kuwania nafasi ya kuwa mwenyekiti wa umoja wa kinataifa “AU” kule Ethiopia. Tayari Marais saba wamemhakikishia Raila kuwa watamuunga mkono Nia yake ya kuwa mwenyekiti mapya. viongozi wote wa serikali na upinzani wamejitolea mhanga wa wamefurahia na kumtakia ushindi katika azma yake .
Katika sekta ya elimu baadhi ya masomo yameunganishwa . Creative art , muziki na physical education. Sasa itakuwa ” creative art na michezo. Somo la sayansi ya nyumbani na kilimo itakuwa somo moja yaani kilimo na nutrition . Sasa wazazi hawatakuwa na gharama ya kununua vitabu vingi zaidi vya kusoma. Lengo kuu ya mtaala wa umilisi yaani” CBC” ni kukuza vipaji na Talanta kwa wanafunzi shuleni.

Waziri wa afya Susan Nahumicha amefanya mabadiliko katika sekta ya afya. Sasa bima ya afya imebadilishwa kutoka kwa ” NHIF” sasa ni “SNHIF” itakuwa ni shughuli kabambe kwa wakenya wanafaa kuanza kujiajiri upya Tena.
Katika chama Cha mawakili nchini ni furaha tele, baada ya kupiga kura siku ya alhamisi tarehe ishirini na Tisa Februari, sasa kiongozi mpya ni Faith Odhiambo. Tusisahau kuwa mabadiliko ndicho kitu ambacho hudumu Maishani mwa kila binadamu.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img